gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,305
- 3,327
Upo usemi wahenga hupenda kusema na hapa nanukuuu,
"Miruzi mingi humpoteza mbwa".
Dhana ya usemi huo wa wahenga walimtizama mbwa anapokua mwituni kuwinda wanyama kama itatokea mabwana zake ni zaidi ya mmoja wote wanamwita kwa mruzi wakiwa pande tofauti mbwa huyu hubaki kuduwaa katikati asijue pa kwenda na hatimaye kitoweo kinakosekana.
Ni vema mh raisi akawatambua wana UKAWA vinginevyo asipokua makini atabaki kuduwaa asijue chakufanya.
Chukulia kelele za sasa anazolalamikiwa mh Rais kwakumteua Mtela Mwampamba kwenye teuzi za jana kama vile ameteua mtu asiye na vigezo huu ni wendawazimu.
Ni hawa hawa walimcheka Mwampamba alipokosekana kwenye teuzi za ukuu wa wilaya lakini ni hawahawa wanapiga kelele leo baada yakuteuliwa kwake kwenye teuzi za DAS.
Humu jamvini kulikua na uzi ulianzishwa lengo likiwa kufuatilia na kuhesabu kila Mh kikwete anaposafiri kwenda nje ya nchi huku UKAWA wakipiga kelele kwamba safari zile hazikua na tija lakini ni hawa hawa leo wanamtaka Maguli asafiri nje ya nchi.
Ni hawa hawa walipiga kelele juu ya ufisadi uliokithiri nchini lakini ni hawahawa wanalalamika wanaotumbuliwa kwa ufisadi utumbuaji haufuati haki zabinadamu.
Ni vema mh raisi akachukua mfano huu wa mbwa mawindoni na sasa asikie yeyote achape kazi.
Kama mh atawasikiliza UKAWA hii nchi itapoteza kitoweo kwani wapiga kelele wanapiga hovyo na wanachokipinga leo kesho wanakikubali.
Mwacheni rais afanye kazi hizi kelele sasa ni too much hakuna jema kila jambo malalamiko.