Mh Kessy analipuka Bungeni

Mh Kessy analipuka Bungeni

Nasema tena, kwa mtindo wa serikali 2 tutaendelea kubeba jiwe zito la Zanzibar!
 
Safari hii hatutaki maandamano ya kwenda viwanjani kusikiliza matamko, tamko limeshatolewa kwenye mkutano mkuu pale Mlmn City. Tunataka mtwambie twende na viboko Dodoma tukawatimue wanaokula kodi zetu bure kwa kisingizio cha kutunga katiba yao, na kuyatupa mapendekezo yetu.
 
Mimi nahisi huyo kesi ni chakubimbi,kabla ya kuituhumu zanzibar ni mzigo ilikuwa atueleze iko wapi tanganyika kwenye bunge la kutunga katiba,afahamu tu kuwa katiba ni ya tanganyika na zanzibar.
 
kessy ana kila dalili za kutumiwa na baadhi ya watu wa zanzibar ambao hawataki muungano. Kessy chimbuko lake ni pemba na mie nawajua ndugu zake wa karibu ambao wako zanzibar na ni weupe kuliko yeye.

Watu wale wapenzi wa muungano wajihadhari sana na maneno ya hatari ya kessy. Anatoa maneno ya chuki na sio hoja pekee

watu wa aina hii wanaweza pachikwa kotekote na maadui wa mungano

kelele!
 
^Muungano kwani lazima? Kwa taarifa yako Zanzibar wengi ni mlengo wa mamlaka kamili. Everyone has the God given right to determine his/her destiny and in this judgement there no partiality.
 
Hebu tueleze basi kwa nini tusizingatie maneno ya Kessy? Unaweza kutoa hoja ya kutufanya sisi tuamini maneno yako badala ya Kessy ambaye ametoa mfano kutoka kwa Gavana wa BOT Ndulu?

siasa ina sura nyingi. Kwa nini kaomba radhi pamoja na" kielelezo" cha BOT
 
Hapa aliwashika ccm pabaya
Watanganyika wapenda pesa kuambiwa kuwa wazanzibari hawachangii bali wanabebwa wamecharuka.
Huu si ukweli,bali sisi tumedhulumiwa mno na Tanganyika kiasi hata wakitulipa itacukuwa miaka 50 ndio watamaliza deni tunalowadai.
Tokea 1964 misaada tokanje wanakula pekeyao.
Uvuvi wa bahari kuu ambayo ni eneo la zanzibar wanafanya Tangannyika na makampuni wao ndio wankodisha na pesa zote wanakula peke yao.
mapato yote ya wizara za muungano na ajira nyingi wanakula peke yao.
Ni iaka yahivi karibuni tuu ndio wameanza kutowa 4.5% wakti share yetu BOT ni 11.5%
Lakini kwa sababu kessy kapasua jipu hatunabudi kufuta usaha.
 
Kaongea ukweli. Haka kakisiwa ni mzigo. Tuna option 2, 'kukazamisha' tu au kukasukumia huko madagasca. Ni zigo tulilojitwisha na tunatakiwa kulitua.
 
kiswahili kinakupiga chenga baadhi ya maneno ya Kessy yana uungwana gani. hakuna hoja tena hapa kesy kaomba radhi kwa baadhi ya maneno yake na huo ndo UUNGWANA

Mbona yule aliyekuwa akipiga kelele kama mwehu bila kibali cha kiti hakuambiwa aombe msamaha,naye mbona alitumia maneno ya kibaguzi kwa kumuta Kessy mwarabu na hapa sio kwao.Kessy amesema jambo la ukweli,hawa ni akina vyako vyangu na vyangu si vyako.Haya mambo ndio ya Scotland ,pia huko Barcelona na sababu za kutaka kujitenga zinafanana na za hapa hapa watu kuwa na identity yao na pia kuona upande mmoja unawanufaisha wengine ili hali wao hawanufaiki chochote,na kama hapa kwetu hata huko Hispania na Uingerza watawala wanatumia kila mbinu ili Scotland na Catalunya wasijitenge,huko Uingereza serikali inatumia makampuni makubwa kutishia kuwa yatajitoa huko Scotland iwapo watapiga kura ya ndio ambayo ni kujitoa.Dunia imebadilika na si lazima wote tukubaliane ndio ,hiyo sio demokrasia na sio kusema walewanaosema hapana hawana akili au hawana uzalendo,tujadili hoja na alichokisema Kessy kina mshiko.
Na mwisho tujadili hali ya soko la mahindi ambalo nikilio na hasara kwa wananchi,leo hiihatujui cha kufanya na mahindi ,mahindi yapo nje serikali imeshindwa kununua,hiyohela ya Bunge la katiba afadhali tungenunulia mahindi kwa ajili ya siku zijazo,pia sidhani kama kweli serikali ilijiandaavya kutosha na hali hii ya soko la mahindi ,leo tunazembea wakati Mungu katujalia,lakini muda si mrefu utasikia kuna njaa,hatuna mipango madhubuti,je kwanini serikali isiruhusu tu watu wauze mahindi nje ya nchi?Nakumbuka miaka ya nyuma wakati Mzee Watrioba alipokuwa waziri mkuu alitilia sana umuhimu wa kujenga maghala ya vyakula,naaminitungekuwa na maghala ya kutosha yale mahindi yanayopigwa jua nje yangekuwa yamehifadhiwa sehemu inayostahili,lakini tatizo kipaumbele chetu kipo kwenye Mabugando na mambo mengine yasiyo na tija.Ni wakati sasa umefika pale tunaposema kilimo kwanza basi iwe pia na maghala kwanza.Warioba alijitahidi kuelekeza nguvu zake kuwashauri viongozi kusimamia ujenzi wa maghala huko vijinini,bahati mbaya alipoondoka ndio ukawa mwisho wa hiyo kampeni,tutamkubuka Warioba kwa hilo pia pamoja na ile reli ya Manyoni hadi Singida wakatihuo kukiwa na shida ya usafiri kati ya Manyoni na Singida.
 
Hakuna mwenye clip tushuhudie?


Mzee mimi nishalalamika lakini hakuna Kituo cha TV wala taasisi wanaoweka video za Bunge la katiba youtube wakati mtu unaweza kurekodi hata kwa simu na ku-upload youtube bure.
 
Mimi nahisi huyo kesi ni chakubimbi,kabla ya kuituhumu zanzibar ni mzigo ilikuwa atueleze iko wapi tanganyika kwenye bunge la kutunga katiba,afahamu tu kuwa katiba ni ya tanganyika na zanzibar.

Vilaza wengine matatizo kweli, yani ushaambiwa Zanzibar inalelewa kama mke alafu alafu unauliza Tanganyika iko wapi? Ngonjeeni mpupumuliwe kisogoni ndio mtajua Tanganyika ipo wapi.
 
Big up Kessy. CCM Zanzibar waache unafiki. CCM Zanzibar ndio vinara wa kudai Zanzibar bila bara hoi.
 
Back
Top Bottom