Mbona yule aliyekuwa akipiga kelele kama mwehu bila kibali cha kiti hakuambiwa aombe msamaha,naye mbona alitumia maneno ya kibaguzi kwa kumuta Kessy mwarabu na hapa sio kwao.Kessy amesema jambo la ukweli,hawa ni akina vyako vyangu na vyangu si vyako.Haya mambo ndio ya Scotland ,pia huko Barcelona na sababu za kutaka kujitenga zinafanana na za hapa hapa watu kuwa na identity yao na pia kuona upande mmoja unawanufaisha wengine ili hali wao hawanufaiki chochote,na kama hapa kwetu hata huko Hispania na Uingerza watawala wanatumia kila mbinu ili Scotland na Catalunya wasijitenge,huko Uingereza serikali inatumia makampuni makubwa kutishia kuwa yatajitoa huko Scotland iwapo watapiga kura ya ndio ambayo ni kujitoa.Dunia imebadilika na si lazima wote tukubaliane ndio ,hiyo sio demokrasia na sio kusema walewanaosema hapana hawana akili au hawana uzalendo,tujadili hoja na alichokisema Kessy kina mshiko.
Na mwisho tujadili hali ya soko la mahindi ambalo nikilio na hasara kwa wananchi,leo hiihatujui cha kufanya na mahindi ,mahindi yapo nje serikali imeshindwa kununua,hiyohela ya Bunge la katiba afadhali tungenunulia mahindi kwa ajili ya siku zijazo,pia sidhani kama kweli serikali ilijiandaavya kutosha na hali hii ya soko la mahindi ,leo tunazembea wakati Mungu katujalia,lakini muda si mrefu utasikia kuna njaa,hatuna mipango madhubuti,je kwanini serikali isiruhusu tu watu wauze mahindi nje ya nchi?Nakumbuka miaka ya nyuma wakati Mzee Watrioba alipokuwa waziri mkuu alitilia sana umuhimu wa kujenga maghala ya vyakula,naaminitungekuwa na maghala ya kutosha yale mahindi yanayopigwa jua nje yangekuwa yamehifadhiwa sehemu inayostahili,lakini tatizo kipaumbele chetu kipo kwenye Mabugando na mambo mengine yasiyo na tija.Ni wakati sasa umefika pale tunaposema kilimo kwanza basi iwe pia na maghala kwanza.Warioba alijitahidi kuelekeza nguvu zake kuwashauri viongozi kusimamia ujenzi wa maghala huko vijinini,bahati mbaya alipoondoka ndio ukawa mwisho wa hiyo kampeni,tutamkubuka Warioba kwa hilo pia pamoja na ile reli ya Manyoni hadi Singida wakatihuo kukiwa na shida ya usafiri kati ya Manyoni na Singida.