Mh. January Makamba anamdanganya nani?

Mh. January Makamba anamdanganya nani?

mizambwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2008
Posts
4,421
Reaction score
1,792
Ni siku chache zilizopita nimeona katika vyombo vya habari mh. January Makamba akilalamika na kutuhumu Jeshi la polisi kuwanyanyasa wananchi wasio na hatia. Alikuwa ameenda kuwapa pole wananchi wa Bumbuli tanga ambao walitendewa kama alivyoagiza PM wa Tanzania (Nasema mtapigwa tu, kwani serikali tumechoka) Ilikuwa ni katika mgogoror kati ya wananchi na mwekezaji katika kiwanda cha chai.

Na leo tena amekuja na hii mpya kuhusu Kodi mpya ya huduma za SIM CARDS:-
======================================================================================================

Dar es Salaam. Kuna kila dalili kwamba Serikali inajipanga kufuta kodi ya Sh1,000 kila mwezi kwa wamiliki wa laini za simu baada ya kuwapo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi, taasisi na baadhi ya kampuni za simu nchini.

Hiyo inatokana na kauli ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba aliyoitoa jana akisema kwamba wizara yake ilipinga tangu awali mpango huo kabla ya kupitishwa na kuwa sheria na kwamba anaamini itaondolewa. Kauli hiyo ya Makamba imekuja siku moja baada ya chama tawala, CCM, kukaririwa na vyombo vya habari kikiitaka Serikali kuangalia vyanzo vingine vya mapato badala ya tozo hiyo.

Akizungumza kwa simu jana Makamba alisema: “Sikubaliani na hili suala na kupita kwake ilikuwa ni kuzidiwa nguvu. Lakini najua haliwezi likatekelezeka ni lazima litabadilishwa kwa kuangalia eneo lingine la kutoza kodi.”

Alisema msimamo wa wizara yake katika suala hilo ni tofauti kwani imekuwa ikijitahidi kuhakikisha gharama za mawasiliano zinapungua... “Wizara hatukubaliani na kodi hiyo. Nia yetu ni kupunguza gharama za kupiga simu kwa kuwa ni kitu kinachowezekana.

“Nia yetu ni kushusha gharama iwe sifuri kabisa, kitu chochote kinachopandishwa bei sisi hatukubaliani nacho kwa kuwa ni kuwaumiza wananchi wetu hasa wa vijijini. Bidhaa ambayo inatakiwa kushuka ni mawasiliano hivyo lazima iwe hivyo.”

Jana, Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alisema kwamba Serikali inapokea maoni ya wadau mbalimbali ili kuona namna ya kufanya marekebisho ya tozo hiyo. Hata hivyo, alisema uamuzi wa kuanzisha tozo hiyo haukuwa wa Serikali bali ulipitishwa na kukubaliwa baada ya kujadiliana na Kamati ya Bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge.

“Hayo yalipendekezwa na Kamati ya Bunge siyo Serikali. Tena walipendekeza vyanzo 67 vya kodi likiwamo hilo la kadi za simu. Walipendekeza tukate Sh1,450 kwa mwezi, lakini sisi Serikali tukashusha hadi Sh1,000 yaani kila mwananchi akatwe Sh33.3 kwa siku na mapato yatakayopatikana yatakwenda kuboresha miradi ya maji, umeme vijijini na barabara,” alisema Dk Mgimwa.

====================================================================================================

My take: Ni serikali ya CCM pamoja na Wabunge wa CCM ambao walipiga kelele na kuipitisha bajeti kandamizi. Wabunge wa CHADEMA siku ya kupitisha bajeti walikuwa ARUSHA.

Sasa Makamba ana nia gani kusema haya ikiwa na yeye ni kiongozi wa CCM na anajua issue yote??

Au anawadanganya wananchi wake ili wamuone kuwa anawatetea???

Ni PM wa serikali ya CCM aliyeruhusu wananchi kupigwa na POLISI kama walivyotendewa Bumbuli:-

Je, Makamba hajui kuwa askari POLISI wamepewa rungu na Mh. PM kupiga tu kwani serikali ya January Makamba wameshachoka???

TAFAKARI KAMA uNA AKILI TIMAMU UTAELEWA.....

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
anasema tuwalaumu wabunge kwa tozo ya 1000.yeye mbona ni mbunge pia
 
January ni mnafiki. Nimemueleza ukweli Facebook akaniblock hahaha! Ukweli unauma.
 
nilishawah kumwambia kule tweeter kuwa sio tu unaibu waziri,hata utendaji wa kata haumfai,jaman january ameshindwa-kudeliver pale wizarani
 
ni siku chache zilizopita nimeona katika vyombo vya habari mh. January makamba akilalamika na kutuhumu jeshi la polisi kuwanyanyasa wananchi wasio na hatia. Alikuwa ameenda kuwapa pole wananchi wa bumbuli tanga ambao walitendewa kama alivyoagiza pm wa tanzania (nasema mtapigwa tu, kwani serikali tumechoka) ilikuwa ni katika mgogoror kati ya wananchi na mwekezaji katika kiwanda cha chai.

Na leo tena amekuja na hii mpya kuhusu kodi mpya ya huduma za sim cards:-
======================================================================================================

dar es salaam. Kuna kila dalili kwamba serikali inajipanga kufuta kodi ya sh1,000 kila mwezi kwa wamiliki wa laini za simu baada ya kuwapo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi, taasisi na baadhi ya kampuni za simu nchini.

Hiyo inatokana na kauli ya naibu waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia, januari makamba aliyoitoa jana akisema kwamba wizara yake ilipinga tangu awali mpango huo kabla ya kupitishwa na kuwa sheria na kwamba anaamini itaondolewa. Kauli hiyo ya makamba imekuja siku moja baada ya chama tawala, ccm, kukaririwa na vyombo vya habari kikiitaka serikali kuangalia vyanzo vingine vya mapato badala ya tozo hiyo.

Akizungumza kwa simu jana makamba alisema: “sikubaliani na hili suala na kupita kwake ilikuwa ni kuzidiwa nguvu. Lakini najua haliwezi likatekelezeka ni lazima litabadilishwa kwa kuangalia eneo lingine la kutoza kodi.”

alisema msimamo wa wizara yake katika suala hilo ni tofauti kwani imekuwa ikijitahidi kuhakikisha gharama za mawasiliano zinapungua... “wizara hatukubaliani na kodi hiyo. Nia yetu ni kupunguza gharama za kupiga simu kwa kuwa ni kitu kinachowezekana.

“nia yetu ni kushusha gharama iwe sifuri kabisa, kitu chochote kinachopandishwa bei sisi hatukubaliani nacho kwa kuwa ni kuwaumiza wananchi wetu hasa wa vijijini. Bidhaa ambayo inatakiwa kushuka ni mawasiliano hivyo lazima iwe hivyo.”

jana, waziri wa fedha, dk william mgimwa alisema kwamba serikali inapokea maoni ya wadau mbalimbali ili kuona namna ya kufanya marekebisho ya tozo hiyo. Hata hivyo, alisema uamuzi wa kuanzisha tozo hiyo haukuwa wa serikali bali ulipitishwa na kukubaliwa baada ya kujadiliana na kamati ya bajeti inayoongozwa na mbunge wa bariadi magharibi (ccm), andrew chenge.

“hayo yalipendekezwa na kamati ya bunge siyo serikali. Tena walipendekeza vyanzo 67 vya kodi likiwamo hilo la kadi za simu. Walipendekeza tukate sh1,450 kwa mwezi, lakini sisi serikali tukashusha hadi sh1,000 yaani kila mwananchi akatwe sh33.3 kwa siku na mapato yatakayopatikana yatakwenda kuboresha miradi ya maji, umeme vijijini na barabara,” alisema dk mgimwa.

====================================================================================================

my take: Ni serikali ya ccm pamoja na wabunge wa ccm ambao walipiga kelele na kuipitisha bajeti kandamizi. Wabunge wa chadema siku ya kupitisha bajeti walikuwa arusha.

Sasa makamba ana nia gani kusema haya ikiwa na yeye ni kiongozi wa ccm na anajua issue yote??

Au anawadanganya wananchi wake ili wamuone kuwa anawatetea???

Ni pm wa serikali ya ccm aliyeruhusu wananchi kupigwa na polisi kama walivyotendewa bumbuli:-

je, makamba hajui kuwa askari polisi wamepewa rungu na mh. Pm kupiga tu kwani serikali ya january makamba wameshachoka???

Tafakari kama una akili timamu utaelewa.....

Mizambwa
inaniuma sana!!!

kama ungekuwa unapitia tweets basi ungegundua kuwa january makamba aliiongea kauli hii mapema sana kwenye mitandao ya kijamii.ila jana ilikuwa marudio tuu na aliwasihi wananchi wawabane wabunge wao kwanini walipitisha kodi hii. Pia alisema wizara yake ilipinga kodi hiyo japo baadae alikuta imepitishwa na wabunge makada
 
Dawa ni kuwapiga chini wabunge wote wa chama cha mafisadi! hawafai hao wote wanafiki,ni kama familia ya mganga wa kienyeji mke anaroga Baba anajidai kuagua but the truth is wote ni wachawi
 
January anablock mtu yoyote anayemchallenge... he is weak, spoilt and hypocrite

Inasikitisha sana kuona vijana ndio wanaongoza unafiki na upuuzi wa ku-swing serious matters kama vitoto vya kindergatten

anenisikitisha sana
 
Wakati wao ndo vijana pale Mjengoni nilitarajia watatupigania vijana wenzao lakini imekuwa kinyume wao ndo wapo kwenye front line kutuua
 
hili swala la kdi za simu naona wanasiasa wanataka kuliteka na kujichukulia umaarufu wa kisiasa kwani kauli zao za kupinga zimekuja baada ya kuona wananchi wamekuja juu ni kama wakati ule sheria za mifuko ya hifadhi ya jamii inapitishwa mpaka sasa sijaona mbunge makini kama aliyekuwa Dr Slaa kwani alikuwa anapitia kipengere baada ya kipengere
Wakati wa bunge la bajeti wabunge wa chadema hawakuwepo wakati wanatambua kuwa ni kikao muhimu kuliko vyote hivyo hawana cha kujitetea
Makamba ni naibu waziri kuna kitu kinaitwa uwajibikaji wa pamoja hivyo asijifanye yeye aznajali wananchi au ni mzuri zaidi mbona mpaka sasa ameshindwa kusimamia mtambo wa kukagua gharama za simu uletwe ili hayo makampuni yalipe kodi stahili badala yake anabwabwaja hii ndio akili ndogo kuongoza kubwa
 
kama ungekuwa unapitia tweets basi ungegundua kuwa january makamba aliiongea kauli hii mapema sana kwenye mitandao ya kijamii.ila jana ilikuwa marudio tuu na aliwasihi wananchi wawabane wabunge wao kwanini walipitisha kodi hii. Pia alisema wizara yake ilipinga kodi hiyo japo baadae alikuta imepitishwa na wabunge makada

we ndio hamna kitu kabisa,yan nilifikiri unavyomtetea alitweet mapema ni kabla haijapitishwa kumbe ishapitishwa yy ndo anajishaua...aende zake kule
 
Na hii ndio matatizo ya kura za NDIOOOO na SIOOO!
Kila mtu atajifanya hakukubaliana nalo,
Ila zingekuwa zinapigwa kura za kueleweka wanafiki wangejulikana

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
hili swala la kdi za simu naona wanasiasa wanataka kuliteka na kujichukulia umaarufu wa kisiasa kwani kauli zao za kupinga zimekuja baada ya kuona wananchi wamekuja juu ni kama wakati ule sheria za mifuko ya hifadhi ya jamii inapitishwa mpaka sasa sijaona mbunge makini kama aliyekuwa Dr Slaa kwani alikuwa anapitia kipengere baada ya kipengere
Wakati wa bunge la bajeti wabunge wa chadema hawakuwepo wakati wanatambua kuwa ni kikao muhimu kuliko vyote hivyo hawana cha kujitetea
Makamba ni naibu waziri kuna kitu kinaitwa uwajibikaji wa pamoja hivyo asijifanye yeye aznajali wananchi au ni mzuri zaidi mbona mpaka sasa ameshindwa kusimamia mtambo wa kukagua gharama za simu uletwe ili hayo makampuni yalipe kodi stahili badala yake anabwabwaja hii ndio akili ndogo kuongoza kubwa

wabunge wa chadema hata wakiwepo ni sawa na gunia la sukari kulitumbukiza baharini,kwani yale mazombie yakisema ndiyooooo.. Wanakuwa washamaliza kila kitu,dawa yao kuwaondoa kina lusinde,mwingulu na wale chakula ya boss(special chairs) aka wachumia chini
 
kama ungekuwa unapitia tweets basi ungegundua kuwa january makamba aliiongea kauli hii mapema sana kwenye mitandao ya kijamii.ila jana ilikuwa marudio tuu na aliwasihi wananchi wawabane wabunge wao kwanini walipitisha kodi hii. Pia alisema wizara yake ilipinga kodi hiyo japo baadae alikuta imepitishwa na wabunge makada

Mkuu DAVIES

Hivyo tutakubaliana kuwa Wabunge makada wa CCM wanaipeleka nchi kubaya, kwa maslahi ya Chama na siyo maslahi ya Taifa Tanzania. In maana hata bajeti inapopelekwa bungeni tayari wameshaipitisha wao. Hivyo hakuna mana ya wabunge kuongea au kujadili bajeti. Watuandikie kwenye magazeti walichoamua wao makada wa CCM. Tupo tayari kuburuwa lakini mwisho utafika tu.

Wabunge wa CCM wamekosa mwelekeo na wanachokiwaza ni posho tu na kujipendekeza kwa wakubwa na huku wanawaumiza wananchi twaliowachagua. Waelewe kuwa pale mjengoni wameenda sababu wamechaguliwana wananchi na siyo wamechaguliwa na wakubwa wanakojipendekeza.

Je, wakuu kwa mtindo huu tutafika kweli???????

Na ndio maana Wabunge wa CCM wanatetea uozo na endapo hoja hata kama ni njema ikitolewa na upande wa upinzani lazima wataipinga tu.

NAFIKIRI dAWA NI KUWAMWAGA HAWA WOTE......

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Last edited by a moderator:
Wakati wa bunge la bajeti wabunge wa chadema hawakuwepo wakati wanatambua kuwa ni kikao muhimu kuliko vyote hivyo hawana cha kujitetea

Wabunge wa CHADEMA hawakuwepo bungeni siku na kama utakumbuka mwaka huu hata bajeti ya waziri kivuli bungeni haikusomwa.

Sababu ya kutokuwepo kwao ni kutokana na Bomu lililolipuka katika mkutano wa CDM kule Arusha,

Hivyo wote walikuwa Arusha kuwafariji wahanga wa bomu na si kwamba walifanya makusudi kutokuwepo Bungeni. Na CCM walitumia nafasi ya kukosekana kwao kuipitisha faster bajeti ya wizara.

Mkuu huoni kuwa kwa hilo chadema waliteleza? Wataendaje wote kufariji ilihali wakati huo kulikuwa na jambo la muhimu bungeni? Ninavofahamu ni kwamba walitakiwa kuteua wachache wakawakilishe kule Arusha na si kuhama wote. FACT.
 
hili swala la kdi za simu naona wanasiasa wanataka kuliteka na kujichukulia umaarufu wa kisiasa kwani kauli zao za kupinga zimekuja baada ya kuona wananchi wamekuja juu ni kama wakati ule sheria za mifuko ya hifadhi ya jamii inapitishwa mpaka sasa sijaona mbunge makini kama aliyekuwa Dr Slaa kwani alikuwa anapitia kipengere baada ya kipengere
Wakati wa bunge la bajeti wabunge wa chadema hawakuwepo wakati wanatambua kuwa ni kikao muhimu kuliko vyote hivyo hawana cha kujitetea
Makamba ni naibu waziri kuna kitu kinaitwa uwajibikaji wa pamoja hivyo asijifanye yeye aznajali wananchi au ni mzuri zaidi mbona mpaka sasa ameshindwa kusimamia mtambo wa kukagua gharama za simu uletwe ili hayo makampuni yalipe kodi stahili badala yake anabwabwaja hii ndio akili ndogo kuongoza kubwa
lakini nakumbuka mdee alizungumzia hili pale mjengoni siku ya mwisho ya majumuisho ya bajeti ya wizara ya fedha!!
 
Don't Judge him until you hear him and give him time to Explain himself.
 
Ni mtazamo wako naheshimu...Ila si kila jambo ni la kutia siasa . J Makamba ni kiongozi safi.
 
Mkuu huoni kuwa kwa hilo chadema waliteleza? Wataendaje wote kufariji ilihali wakati huo kulikuwa na jambo la muhimu bungeni? Ninavofahamu ni kwamba walitakiwa kuteua wachache wakawakilishe kule Arusha na si kuhama wote. FACT.

Mkuu lile lilikuwa ni janga la Taifa. Msiba haukuwa kwa wa ARUSHA peke yao.

CDM kwa uzalendo isingelikuwa busara eti wengine wasiende kwa sababu ya bunge. Hivi unataka kunihadaa kuwa kati ya Msiba na Bunge kipi muhimu???

Wewe mfano ukiwa na msiba unaokuhusu, na pia kuna kipindi cha Bajeti bungeni;-

Je, utaenda kuangalia TV waziri akisoma bajeti au utaenda msibani kujiunga na wenzio???

Nijibu ili niendelee..................

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Back
Top Bottom