Meitinyiku L. Robinson
JF-Expert Member
- Aug 29, 2011
- 412
- 90
Inasikitisha sana kwa kweli na tena ukizingatia ni kijana mdogo kabisa na tegemeo katika familia yake, ila kama tujuavyo katika nchi yetu hii kesi ikiwa inamuhusisha mkubwa wewe mdogo na mnyonge haki yako huwezi kuipata tuna mifano mingi ya mambo ya namna hiioleni sana.Mungu amlaze mahala pema peponi bwana Benjamini.
Tatizo kubwa na la msingi sana ni wajuvi wa sheria hawajui kuzitunza sheria, kama madam judge angezingatia sheria angetoa tahadhari kwa wapita njia.
Kushindwa kutoa gari ya kumkimbiza hospitali majeruhi ni katika muendelezo wa tabia za wakubwa kutoshirikiana na wananchi wa kawaida.
Watanzania hasa vivogo jifunzeni Kenya. Naibu Jaji mkuu anaburuzwa mahakamani kwa kumdhalilisha mlinzi tu wa duka. Hapa kwetu walinzi wanachapwa vibao na mameya na hakuna kinachofanyika! Jaji anagonga anaua mambo kimyaaa? Siku zaja ambapo katiba mpya itaondoa yote haya. Nakumbuka Rashid wa Kuli alivyosema "yana mwisho haya"
Ni siku ya leo majira ya saa 5 asubuhi katika maeneo ya Uzunguni aishipo Mhe Jaji wa Mahakama Kuu na vile vile ndiye Jaji Mfawidhi Mkoani Arusha, palikuwa nanmtu akikata mti bila tahadhari yeyote ile kujulisha watu kuwa kuna kazi hiyo inaendelea ndipo kijana mmoja mwendesha toyo anayepaki maeneo ya Mount Meru Hotel alipokuwa akipita maskini bila kujua lolote mti ukamwangukia na kufa papo hapo
Hili lilikuwa likifanyika nyumbani kwa Jaji kama mtu au watu makini palitakiwa kuwa na tahadhari yeyote Cha kusikitisha zaidi pia palikuwa na magari mengi yamepaki nyumbani kwa Jaji ambayo at lst wangeonesha utu kumkimbiza Kijana huyo hospitali ila jamaa wakakaa kimya. Wananchi walitaka kuchoma nyumba moto wakatulizwa na Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ni kijana wa miaka 20 tu aliyekuwa akiangaika kutafuta riziki yake kwa nguvu zake mpole, mnyenyekevu dogo ni kila kitu wazee
Sasa Mhe Jaji anatuambiaje wakaazi wa Arusha Mosi juu ya Occupiers Liability lakini pili wazazi wa hawa kijana ambao almost 85% ya maisha yao kijana ndo alikuwa anahusika please Madame Judge tell us something inauma sana!!
Rest in Peace BENJAMIN binafsi ntakukumbuka sana!!!
kaeni mbali na jaji wa watu....nyumba ni ya serikali siyo nyumba binafsi na yawezekana kabisa waliokuwa wanakata miti ni wizara ya miundo mbinu kupitia kitengo cha majengo...........sasa jaji anatoka wapi na kazi za watu wengineo?
kama ni nyumba yake biafsi hapo utamwingiza lakini kama si hivyo kilaumu kitengo cha majumba ya serikali na mwanasheria mkuu na wala siyo mpangaji wao........commonsense sometimes is not common to everyone........
Hii nayo Mpya