Mh. Jaji Aisha Makongoro Arusha tunataka kusikia tamko juu ya Kifo cha Mwenzetu

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Aug 29, 2011
412
90
Ni siku ya leo majira ya saa 5 asubuhi katika maeneo ya Uzunguni aishipo Mhe Jaji wa Mahakama Kuu na vile vile ndiye Jaji Mfawidhi Mkoani Arusha, palikuwa nanmtu akikata mti bila tahadhari yeyote ile kujulisha watu kuwa kuna kazi hiyo inaendelea ndipo kijana mmoja mwendesha toyo anayepaki maeneo ya Mount Meru Hotel alipokuwa akipita maskini bila kujua lolote mti ukamwangukia na kufa papo hapo

Hili lilikuwa likifanyika nyumbani kwa Jaji kama mtu au watu makini palitakiwa kuwa na tahadhari yeyote Cha kusikitisha zaidi pia palikuwa na magari mengi yamepaki nyumbani kwa Jaji ambayo at lst wangeonesha utu kumkimbiza Kijana huyo hospitali ila jamaa wakakaa kimya. Wananchi walitaka kuchoma nyumba moto wakatulizwa na Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ni kijana wa miaka 20 tu aliyekuwa akiangaika kutafuta riziki yake kwa nguvu zake mpole, mnyenyekevu dogo ni kila kitu wazee

Sasa Mhe Jaji anatuambiaje wakaazi wa Arusha Mosi juu ya Occupiers Liability lakini pili wazazi wa hawa kijana ambao almost 85% ya maisha yao kijana ndo alikuwa anahusika please Madame Judge tell us something inauma sana!!

Rest in Peace BENJAMIN binafsi ntakukumbuka sana!!!
 
Tatizo kubwa na la msingi sana ni wajuvi wa sheria hawajui kuzitunza sheria, kama madam judge angezingatia sheria angetoa tahadhari kwa wapita njia.
Kushindwa kutoa gari ya kumkimbiza hospitali majeruhi ni katika muendelezo wa tabia za wakubwa kutoshirikiana na wananchi wa kawaida.
 
Inasikitisha sana kwa kweli na tena ukizingatia ni kijana mdogo kabisa na tegemeo katika familia yake, ila kama tujuavyo katika nchi yetu hii kesi ikiwa inamuhusisha mkubwa wewe mdogo na mnyonge haki yako huwezi kuipata tuna mifano mingi ya mambo ya namna hii:poleni sana.Mungu amlaze mahala pema peponi bwana Benjamini.
 
Kweli kesi inayomhusu mkubwa dhidi ya mnyonge ni vigumu mnyonge kupata haki yake.

Kuna kesi ya Jaji Rugazia aliua mtu katika ajali ya gari barabarani hata sijui iliishia wapi!?
 
Duh Inasikitisha! hivi ni kweli ajali haina Kinga?

Mwenyezi Mungu amuweke Pahali panapo Mstahili Marehemu..

HivI ile Sheria inayosema Hakuna kukata miti imeshafutwa? au ilijaziwa na ile ya Kata mti Panda Mti!!

Miti mingine inakawaida ya Kuondoka na Mtu au Watu Matukio kama haa ni mengi Yeshatokea... Na Hapo Uzunguni hili si tukio la kwanza
 
Hadi sasa Mh Jaji amelichuliaje ... haswa yeye akiwa ndio Nguli wa Sheria hapa Nchini .... Must come out and speak out please!!!!!!!!!
 
kwa kweli inasikitisha sana.Kijana aliyekuwa mhimili wa familia kupoteza maisha sababu tu ya uzembe wa watu fulani?
lakini kama Mungu aishivyo, damu ya huyo kijana atalilia haki yake.
 
Big up Tumy, Mwita Maranya, Duduwasha, Azimio Jipya, Valid Statement etc! Had a very bad today av bn crying the whole day' kupoteza dogo wa umri ule jamani and the way he was obidient, co-operative, flexible duh it pains wazee. Halafu tatizo uzembe aaaaaaah no bana najua hakuna cha kufanya coz he is gone so far ila hatutaki tena kupoteza vijana kwa namna hiyo na ili iwe hivyo hatua zichukuliwe basi God help us!!!

Once again RIP Benjamin pamoja na Regia!!! Thnks guyz and remain Blessed
 
RIP Benjamin, wanyonge tusiponyanyuka na kupinga mambo kama haya tutaendelea kupukutishwa tu. Awajibishwe.
 
Ntatoa maoni yangu baada ya kusikia kauli ya Mhe. Jaji. Walio karibu nae wamnong'oneze kuwa nasubiri kauli yake.

RIP Benjamin!
 
Tatizo kubwa na la msingi sana ni wajuvi wa sheria hawajui kuzitunza sheria, kama madam judge angezingatia sheria angetoa tahadhari kwa wapita njia.
Kushindwa kutoa gari ya kumkimbiza hospitali majeruhi ni katika muendelezo wa tabia za wakubwa kutoshirikiana na wananchi wa kawaida.

Watanzania hasa vivogo jifunzeni Kenya. Naibu Jaji mkuu anaburuzwa mahakamani kwa kumdhalilisha mlinzi tu wa duka. Hapa kwetu walinzi wanachapwa vibao na mameya na hakuna kinachofanyika! Jaji anagonga anaua mambo kimyaaa? Siku zaja ambapo katiba mpya itaondoa yote haya. Nakumbuka Rashid wa Kuli alivyosema "yana mwisho haya"
 
Iko namna ya kumsaidia Benjamin na familia yake kwa sababu ndiye aliyekuwa mtunzaji wa familia yake. Kisheria, familia ya Benjamin ina haki ya kumshitaki Jaji na mfanyakazi wake kwa wrongful death. Atashinda na watapata fidia ya kutosha na kuiwezesha familia yake kuendelea na matunzo aliyokuwa anayatoa Benjamin. Kama kuna wakili Arusha anayetaka kufanya hiyo kazi malipo yake yatapatikana kwenye hiyo hela ya fidia as a set percentage. Watanzania tunatakiwa tuanze kuwa na ujasiri wa kufanya vitu namna hiyo pale mahali ambapo haki ya mnyonge imechukuliwa. Wenzetu Ghana, Kenya na hata sehemu kama Zambia wanafanya hivyo. Sheria inawalinda wanyonge ila mawakili wetu tunawaomba watusaidie kwenye hili as their contribution to mass education. Please help this family.
 
Dah kwakweli tutaisha maana watungasheria ndo wanao vunja sheria,kunahaja ya kupata mwanasheria hapo ili iwe fundisho kwa wenye kiburi cha madaraka kama hicho.benjamin bado alikuwa lijanja mdogo sana ambaye sitegemeo lala familia yake tu bali hata kwataifa pia.tatizo naloliona mm yawezekana huyu jaji kasha enda kuwa honga na kuwarubuni wazazi wa marehem,hivyo hawataonyesha ushirikiano wa kutosha kwa mwanasheria.hapa pia elim inahitajika kwa wananchi wa kawaida juu ya kutetea haki zao.RIP BENJAMIN.
 
Ni siku ya leo majira ya saa 5 asubuhi katika maeneo ya Uzunguni aishipo Mhe Jaji wa Mahakama Kuu na vile vile ndiye Jaji Mfawidhi Mkoani Arusha, palikuwa nanmtu akikata mti bila tahadhari yeyote ile kujulisha watu kuwa kuna kazi hiyo inaendelea ndipo kijana mmoja mwendesha toyo anayepaki maeneo ya Mount Meru Hotel alipokuwa akipita maskini bila kujua lolote mti ukamwangukia na kufa papo hapo

Hili lilikuwa likifanyika nyumbani kwa Jaji kama mtu au watu makini palitakiwa kuwa na tahadhari yeyote Cha kusikitisha zaidi pia palikuwa na magari mengi yamepaki nyumbani kwa Jaji ambayo at lst wangeonesha utu kumkimbiza Kijana huyo hospitali ila jamaa wakakaa kimya. Wananchi walitaka kuchoma nyumba moto wakatulizwa na Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ni kijana wa miaka 20 tu aliyekuwa akiangaika kutafuta riziki yake kwa nguvu zake mpole, mnyenyekevu dogo ni kila kitu wazee

Sasa Mhe Jaji anatuambiaje wakaazi wa Arusha Mosi juu ya Occupiers Liability lakini pili wazazi wa hawa kijana ambao almost 85% ya maisha yao kijana ndo alikuwa anahusika please Madame Judge tell us something inauma sana!!

Rest in Peace BENJAMIN binafsi ntakukumbuka sana!!!

kaeni mbali na jaji wa watu....nyumba ni ya serikali siyo nyumba binafsi na yawezekana kabisa waliokuwa wanakata miti ni wizara ya miundo mbinu kupitia kitengo cha majengo...........sasa jaji anatoka wapi na kazi za watu wengineo?

kama ni nyumba yake biafsi hapo utamwingiza lakini kama si hivyo kilaumu kitengo cha majumba ya serikali na mwanasheria mkuu na wala siyo mpangaji wao........commonsense sometimes is not common to everyone........
 
Rutashubanyuma kama hili ungeeka kama swali na kutaka kufahamishwa kama Nyumba ni ya Jaji au ya Serikali ungekuwa umetumia busara sana lakini kwa jinsi ulivyoweka ni kama your very sure that the house belongs to the government, ila kwa kuwa nimeona na kuelewa nia yako na kwa kuwa naheshimu signature yako naomba nikusaidie,

Madame Judge brought the house wakati ule Mhe Benjamin Mkapa akiwa Rais na kuruhusu kuuzwa au kununuliwa kwa nyumba za Serikali na wakati huo Jaji huyu alikuwa ni Resident Magistrate Incharge (Arusha) ndipo alipoamishiwa Moshi kama Resident Magistrate Incharge with Extended Jurisdiction mpaka alipoteuliwa Jaji na Mhe Kikwete mwaka juzi. Hivyo ili kuweka record sawa nyumba ni ya kwake na toka karudishwa Arusha anashugulikia kuzungushia uzio nyumba hiyo na ndiyo sababu ya kukata hiyo miti, na hata kama haikuwa yake basi she is a Judge and in the court what matters always is test of reasonability...... Hata yeye au huyo aliyekuwa akifanya shughuli hiyo walitakiwa wareason out manake kama tukiachia loophole ya namna hiyo uisemayo tutapoteza wengi..... I humbly submit
 
Hii nayo Mpya

Suala la kifo haina mazoea, hasa unapofiwa na ndugu, jamaa au rafiki, lazima utapata shock. Kuhusu hili la Benjamin kunakuwa na maswali mengi juu yake, ukizingatia mti ulikuwa unakatwa kando ya barabara, nyumbani kwa jaji Aisha, na aliyekuwa anakata mti ni Mfungwa aliyekuwa anatekeleza kazi aliyopewa wakata hana utaalamu nayo. Kazi ile ya kukata miti barabarani angepewa mtaalamu nadhani madhara kama haya ya kizembe yasingetokea, ama tahadhari ingetolewa kwa watumiaji wa ile njia. Mfungwa yeye anafanya tu kutekeleza majukumu yake.
 
Mtoa maada, kwa kama unaifahamu familia yake washauri watafute mwanasheria. fidia hapa inatakiwa itolewe kwa ndugu wa marehemu.
 
R.I.P Benjamin, lakini kwa wanafuatilia vyombo vya watakumbuka kisa cha hivi majuzi ya naibu jaji mkuu wa Kenya, kwa katiba yao hakuna aliye juu ya sheria. Wanasheria watusaidie ktk hili
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom