Kuna tetesi (rejea mahojiano ya Ismail Jussa na idhaa ya kiswahili ya ujerumani siku ya Jumanne tarehe 13/12/2011) pia kuwa Mhe. Hamad Rashid anatumiwa na CCM kuanzisha mgogoro CUF na ameahidiwa kuwa mgombea mwenza wa urais kwa ticket ya CCM mwaka 2015. Analizungumziaje hili?
Hili usiulize Yahya, za mbayuwayu changanya na za kwako!
Mjadala wa Kipindi cha TUONGEE ASUBUHI upo hewani na Sinai Shaka undani kuhusu mgogoro unaofukuta ndani ya cuf utatolewa sura ya upande wa pili kwa kina. Fuatilia mjadala
Ndugu yangu mi mwenyewe namshangaa Maalim Seif... hana muda wa kufanya mambo ya chama kutokana na kutingwa na shughuli za ikulu ya zanzibar na hilo analijua,lakini bado anang'ang'ania aendelee kukishikiliwa cheo hicho ambacho kimekaa kiutendaji zaidi ndani ya chama.Mimi ni mwanaharakati wa mageuzi na naomba kumpa pongezi Mh. Hamad kwa kutetea heshima ya chama chake.
Naomba niseme waziwazi kwamba sioni tatizo kwa yeye kutamka nia ya kugombea uongozi ili ajaribu kukiimarisha CUF kinachoonekana waziwazi kupoteza mwelekeo. Tatizo ninaloliona hapa ni ulevi wa madaraka wa viongozi ndani ya vyama vya kisiasa na uoga wa kuwaachia wengine madaraka.
...Yahya, undani kuhusu huo mgororo haukuweza kutolewa, zimeletwa siasa zile zile za kinafki. Hamad Rashid hajataka kuwa mkweli, kuhusu hasa kinachoendelea CUF -anasema anamweshimu sana Maalim Seif, wakati huo huo akimchimba chini kwa chini- na ameendelea kujichanganya kuhusu msimamo wake juu ya mambo mbalimbali yaliyotokea mwaka huu. Amejichanganya juu ya kambi ya upinzani bungeni -ati sasa, Mbowe afikirie kuhusisha na vyama vingine katika kambi, muswaada wa katiba, suala la posho -kama mfumo mbovu, wao walikuwa wapi wenzao walipotaka kurekebisha mfumo?Mjadala wa Kipindi cha TUONGEE ASUBUHI upo hewani na Sinai Shaka undani kuhusu mgogoro unaofukuta ndani ya cuf utatolewa sura ya upande wa pili kwa kina. Fuatilia mjadala