Mh. Dr. Mwakyembe ushauri huu muhimu

betlehem
Ndugu helewa somo hapo kuwa kikwazo ni DPP, Itakuwa yeye kila fahili likija Ushahidi hautoshi.
Ukumbuke kwamba watumishi wote wa umma wanaweza kuwajibishwa na viongozi wakuu wa kisiasa , hivyo hata kama tatizo ni DPP; Huyo DPP kuna mtu anayeweza kumuwajibisha lakini hafanyi hivyo, unadhani ni kwa nini? kama Mwakyembe ataendelea kujitahidi kuzuia mambo haya lakini kila akipeleka vielelezo polisi hakuna majawabu unadhani jitihada zake zinaweza kuzaa matunda?
 
Ingekuwa vyema pia kwenda kukagua akaunti za staff wote waliokuwepo siku hiyo km zilijaa mpunga wa ghafla ghafla
Inasemekana kwamba ilikuwa walipwe baadae. Mwakiembe anakuambia video zinaonesha siku hiyo waliokuwa wanabeba mabegi ni polisi badala ya loaders. Anakuambia mtu aliekuwa zamu kwenye screening aliondolewa na mwenzake, na alieingia akapitisha mzigo kisha akamuachia mwenye zamu kuendelea. Anakuambia picha za CCTV, zinaonesha askari polisi na askari wa kiwanja wakiusubiri mzigo kabla hata haujafika. Anaongeza kwa kusema wengi wanaonekana wakiwa wanahaha huku na kule kuhakikisha mzigo unapita salama. Sasa ujiulize kwa nini hakuna mtu alietoa taarifa hizo hadi mzigo ukakamatwa S.Africa! na kama mzigo usingekamatwa maana yake hizo picha zote za CCTV, zingebakia kuwa Movie .
 
Mkuu kwenye taasisi kubwa kama serikali; mtu mmoja hata awe na nia nzuri kiasi gani na hata awe na uwezo mkubwa kiasi gani hawezi akafanya kazi peke yake na akafanikiwa. Ili nchi iweze kufanikisha jambo ni lazma kuwe na "Team Work". Sasa inapotokea kwamba mmoja anapambana wengine wanakwamisha ni ngumu kufanikiwa. Kadhalika ni kwa nini wanaokwamisha wasikwamishe kama wanaamini kwamba nao wataathirika na operesheni husika? Na kwa upande wa Mwakyembe; ni vipi ataweza kudhibiti hali ikiwa anaokabiliana nao ni watu anaofanya nao kazi na usikute wengene kulingana na hadhi zao, Mwakyembe anajikuta akiwa na "Horizontal relations"? Wewe jiulize tu kwamba kama Rais anasema anawajua wauza unga wakubwa halafu baada ya hapo anawaomba waache, halafu Mwakyembe yuko uwanjani anakaza kamba kukamata, Halafu askati wake wananunuliwa, na wakifanikiwa kukamata; kesi za wahalifu zinakwama halafu hamla la ziada, imagine!
 
Yeah! uko sahihi sana mkuu. Mimi kinachonipa shida kupita vyote; ni pale ninapojiuliza; Ni nani huyu anayeweza kununua vyombo vyote vya usalama tena eneo nyeti kama uwanja wa ndege? Je mtu huyu serikali kuu haimfahamu? Kama inamfahamu, inamfahamu toka lini na imechukua hatua gani hapo kabla? na kama haimfahamu kwa nini? Zaidi ya hapo kuwakamata hawa waliohongwa haisaidii sana maana huyu anayehonga atahonga tena wengine.
 


Kama siyo Mwakyembe, nani mwingine atawaokoa watanzania. Hata kuupata huu uhuru ulionao mkubwa haikuwa kazi dogo. Kaza buti na wewe Betelehemu, Acha kukata tamaa. Hakuna vita rahisi duniani.
 
Ingekuwa vyema pia kwenda kukagua akaunti za staff wote waliokuwepo siku hiyo km zilijaa mpunga wa ghafla ghafla

Wanalijua hilo soo kitambo sana.
Hawa maharamia huwa hawaweki pesa benki <<Nadhani umeona picha ya Agness 'Masogange' Gerald>>. Huwa wanawekeza katika majengo na magari. Hawaweki benki kwa sbb ni rahisi sana kuwa tracked.
 
Ushauri wako kwamba angejiuzuru haufai, nahisi umetumwa!

Acha mambo yako bna,wewe mtu akitoa mawazo yake ametumwa..kwani wewe hujawahi kumtaka kiongozi ajiuzuru. Au unafikri kujiuzuru matusi?
 

anakupotezea muda huyo jamaa,yeye kama ana mawazo yake si ayaandke
 
Kama unamshauri ahame chama basi wewe hufai. Abaki huko huko apigane nao
Mkuu; unaweza kupambana na mtu unaekula nae na kulala nae chumba kimoja? Unaweza kupambana na mtu ambaye siku ya kupanga utekelezaji mtapanga namna ya kutekeleza kumbe mwenzako ndio ana mfadhili mnae taka kumthibiti? hivi wakati mkiwa kwenye kikao cha siri cha kumthibiti muhalifu unaweza ukaamini kwamba miongoni mwa washiriki( miongoni mwenu ) hawezi kuvujisha siri katika hali hii tunayoiona na kukuunga mkono kinafiki kumbe nyuma ya pazia anakung'ong'a? katika mazingira hayo ni rahisi kutoboa? any way ni mawazo yangu tu; na mimi pia nina uthaifu wangu na ndio maana nikasema tumshauri. Inawezekana kuna ushauri mwengine bora zaidi.
 
Acha mambo yako bna,wewe mtu akitoa mawazo yake ametumwa..kwani wewe hujawahi kumtaka kiongozi ajiuzuru. Au unafikri kujiuzuru matusi?
Halafu watu hawaelewi vizuri kitu kimoja; Haina maana kwamba mtu kujiuzulu ni lazma mpaka awe na kashfa. Hivi ni kwa nini Mwl. Nyerere alijiuzulu? wakati fulani pale inapotokea ukajikuta unawajibika kutekeleza majukumu yako lakini unaofanya nao kazi wanakukwamisha na wewe huna nguvyu ya kutosha ya kuwasukuma watekeleze, basi unaweza kujiuzulu ili kusukuma mamlaka husika ichukue uamusi mgumu. Si mnakumbuka Kujiuzulu kwa Nyerere kulisaidia na baadae Nyerere akapata heshima zaidi!
 
Tatizo baraza la mawaziri limelala,inabidi hiyo kampeni iwe ya mawaziri wote,sasa jana anamsifia Nchimbi halafu anawasema polisi ndio nini sasa..? Unaweza kumtenga Nchimbi na polisi kweli?
 
Kama siyo Mwakyembe, nani mwingine atawaokoa watanzania. Hata kuupata huu uhuru ulionao mkubwa haikuwa kazi dogo. Kaza buti na wewe Betelehemu, Acha kukata tamaa. Hakuna vita rahisi duniani.
Mkuu sijakata tamaa. Nataka tupate mbinu bora kabisa ya kuweka mambo sawa ambayo inaweza ikawa na ufanisi mkubwa. Hata askari wanapopigana, kuna muda hupeleka mashambulizi lakini wakiona mbinu haijakaa sawa wanarudi nyuma kidogo halafu wakija sasa usiombee kichapo chake.pia wanaweza wakatumia mbinu ya kuzunguka na kuzingira kabla ya kushambulia.Sio woga ni mbinu mkuu.
 
Hatajiuzulu....akisha sema wengi serikalini wananuka
Rushwa na walioko chini yake ATAWASHUGHULIKIA... sijaona point yako....ushauri upi...huna...many words...so akiwa hana imani na vyombo vya usalama AWAACHEEE...?? huna point...
Mkuu ninachosema kwa ujumla wake ni kwamba tutafute mbinu ya kushinikiza mabadiliko ya mfumo mzima kwa ujumla la sivyo Mwakyembe yeye tu kama yeye hawezi kufanikiwa hata kama ana nia nzuri ikiwa waliomzunguka (anaofanya nao kazi) ni tatizo.
 
Hapana kujiuzuru, nafikiri sisi kama watanzania tunahitaji kumlinda kwa udi na uvumba waziri huyu, nimependa ulivyochambua majadiliano ya jana kati ya dr na mtangazaji. Kitu kinachoniuma mimi ni kuwa hivi viongozi wengine hawayaoni haya mabaya yanayo yotokea? hivi hakuna hata kiongozi mmja toka ccm mzalendo ambaye angejitokeza hadharani kumuunga mkono dr? Hivi ccm na viongozi wote toka uhuru wa tanzania hakuna hata mmoja ambaye ana uchungu na taifa hili? Jamani huyu raisi wetu hivi ni raisi kweli? mi mbona naona kama nchi haina viongozi? inauma sana kwa nchi kama hii watu tumenyamaza tu,,watu wanawafahamu waovu wametulia tu.

NACHELEA KUSEMA KUWA BORA YA MISRI YATOKEE TANZANIA KULIKO HALI INAVYOENDELEA TANZANIA.
 
Mkuu kwa hilo la kuombea ya Misri yatokee Tanzania Sikuungi mkono. Kinachofuatia sasa nchini Misri ni Kwamba Nchi ile inaenda kuwa nchi iliyokufa.Kuna hatari ya kuwa kama Somalia. Huo sio mfano wa kuigwa na watanzania hata kidogo. Tutafute mbinu nyengine ila kwa hiyo tutakuwa tunapambana na adui feki. Tukirudi kwenye hoja; Kuna kitu kinaitwa "State Capture" katika hali hiyo nchi hushikiliwa kwa remote control na makundi ya watu yenye maslahi flani. Makundi hayo yanaweza yasiwe yanaonekana ila matokeo yake yawe yanaonekana dhahiri. Miongoni mwa dalili zinazoweza kuonesha kwamba nchi imekumbwa na mkasa wa namna hiyo; ni pale unapoona yanatokea matukio yasiyokuwa ya kawaida, kwenye mazingira ambayo yasingetakiwa wala kufikiriwa kutokea, na ushahidi uko wazi lakini serikali haichukui hatua za wazi na za uhakika. Katika mazingira hayo ndipo unapoona hata wale wachache wenye nia nzuri kwenye system wanapata woga.Imagine mtu mmoja anaweza je kuwahonga wanausalama wa uwanja wa ndege na wakahongeka na hata wakasindikiza mzigo wa hatari badala ya kuukamata? ina maana huyo mtu anakuwa na nguvu kuliko serikali? Sasa nini Cha kufanya? ndo hapo sasa.
 
Pamoja na hayo yote aliyofanya ni muhimu wataalam wapitie mikanda iliyohifadhiwa katika computers wanaweza kugundua madudu mengi zaidi ya watu ambao wamekuwa wakipitisha madawa ya kulevya kabla hawajachoma moto JNIA
 

Umesahau na yule traffic feki kule kinyerezi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…