Mh. Dewji iokoe Mwenge sekondari Singida! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Dewji iokoe Mwenge sekondari Singida!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by babayah67, Apr 30, 2012.

 1. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wiki mbili zilizopita nilikuwa Singida Mjini kikazi, nikiwa miongoni mwa Wanafunzi waliosoma Singida kati yaa mwaka 1980 hadi 1984 (Form I - IV) nilikuwa na hamu ya kuitembelea shule yangu, ili kuangalia mandhari yake na pia kuwasalimia walimu wangu kama wangekuwa bado wapo.

  Baada ya kumaliza shughuli zangu za siku, jioni moja nilitembea kuelekea Mwenge Sekondari. Nilianza kupatwa na mshtuko mara tu nilipofika pale kwenye mawe mawili ya barabarani karibu na guest ilokuwa ikijulikana kama Victoria, au Mmassy Bakery (alokuwa akisupply mikate na matunda shuleni). Shock yenyewe ni kuwa shule siku hizi haina tena uzio uliokuwa ukizunguuka shule na kupunguza vibaka. Pamoja na hilo, siku hizi hakuna ulinzi wowote magetini, yaani geti A lili linaloingilia ofisini na madarasani, au Geti B, lile linaloingilia nyumba za walimu.

  Nilijisikia kutoa machozi nilipotembelea mabwenini. Ukiingia bweni la Jamhuri, Azimio na Kujitegemea hali inatisha sana. Vitanda vibovu, kuta chafu hazijapakwa rangi nafikiri sijui toka sisi tunamaliza shule. Kwa ujumla hali ni mbaya saana. Sehemu tulizokuwa tunafulia na kuogea, siku hizi hazitumiki kabisa, maji hayatoki basi ni taabu tupu.

  Nikatembelea bwalo la chakula, ambalo wakati wetu lilikuwa na meza karibu 90 na kila meza ikiwa na mabenchi mawili, sasa hivi niliona meza moja tu. Nilipowauliza wanafunzi wanakaa wapi wakati wa kula walisema wanakula wakiwa wamesimama tu. Kwa ujumla jamani hali ni mbaya saana.

  Kwa wanafunzi wanaosoma pale, sitarajii matokeo yao kuwa mazuri.

  NB: Namwomba Mbunge wa Singida Mjini MH. AZIM DEWJI aitazame kwa jicho la huruma shule hiyo. Ninaamini anaweza japo kuwapakia rangi ndani ya Mabweni yao vijana wale. Na kuwarekebishia japo Taa za kusomea Madarasani na bwenini.
   
 2. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Mkuu pole kwa huzuni iliyokukuta.
  Hali hiyo hiyo hutukuta sisi wengine tuliopita hapo.
  Siungi mkono ushauri wako wa kumtaka MO aisaidie hiyo shule...
  Hiyo ni shule ya SERIKALI KUU na serikali ina wajibu kuikarabati.
  MO kama ana ubavu aibane serikali ndani na nje ya bunge itimize wajibu wake huo.
  Pesa ambayo angetumia kuisaidia shule akaitishe mikutano na wana CCM awalishe pilau,soda na maji kama alivyozoea.
  Akiamua kuisaidia shule afanye kama raia mwenye mapenzi mema...atambue hayo si moja ya majukumu ya mbunge.
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Serikali imeshindwa, wananchi chukueni hatua wenyewe.

  Wasake wote waliosoma hapo, mfanye maarifa ya kutoa usaidizi endelevu shuleni hapo

  Haba na haba hujaza kibaba
   
 4. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,435
  Likes Received: 2,310
  Trophy Points: 280
  Huyo MO yupo kwenye hiyo nafasi kwa maslahi yake mkuu. Ufisadi na ujambazi wooote unaofanywa hapa Tanzania sasa ulishawahi kusikia hata anafanya usanii wa kukemea? Hata kama akipaka rangi asipokemea ujambazi unaoendeshwa na viongozi wa serikali ya sasa ni kama mgonjwa wa maleria kutumia asprin.... hatapona. Wabunge wa aina hii ni kiama cha walalahoi tu.
   
 5. ummu kulthum

  ummu kulthum JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 2,791
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  dah tuko wengi lakini hatujuani yaan hiyo sio shule tena hata matamasha ya mziki huwa yanafanyika hapo.mwenge ilikuwa zamani sasa hivi imebaki jina tu kama ccm
   
Loading...