Mh. Anne Kilango Malecela analalamika nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Anne Kilango Malecela analalamika nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andrew Nyerere, Jun 22, 2010.

 1. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #1
  Jun 22, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,026
  Likes Received: 1,196
  Trophy Points: 280
  Nimeona sasa hivi katika Mlimani TV Mh. A.K. Malecela anasema kwamba anahujumiwa na magazeti,kwamba haya mambo amesema toka zamani lakini Speaker hakumsikiliza ''lakini leo wote mmeshuhudia, watu wengi mitaani ,walikuwa wanayachana magazeti,kwa sababu wamechoshwa na uongo.''

  Sasa,ninaloona katika magazeti yote ya leo ni habari kwamba,''Jakaya Kiwete anapendwa sana na watu kiasi kwamba ameamua kuchukua fomu kugombea urais tena.'' Sasa Ndugu Anne Malecela anasema kwamba wananchi hawakupendezwa na hizi habari?

  Kwa sababu kama kuna watu wameonekana wanampinga Kikwete kugombea tena Urais,tunawasihi waandishi wa habari wasizifiche hizi habari. We adjure them to write the truth.

  Na huyu Mama Malecela sijui analalamika nini? Kwa nini watu wasilinyemelee jimbo 'lake'? Huu ni Uchaguzi,lazima watatokea watu watalinyemelea jimbo lake la Uchaguzi. Anna anayo malalamiko yoyote ya msingi,au anayo tu naturally hysterical temperament?

  Lakini muhimu ni hili swala la kuchana magazeti. Nani kachana magazeti na kwa sababu gani? Tunaomba anayefahamu atueleze. Kwa sababu haifai mtu yoyote aingie Ikulu kwa njia za ulaghai.

  Unakumbuka Aristotle alisema dictators wanawachukua watu,watoto wa wakulima maskini,kufanya kazi ya ubodyguard, wanawalipa hela nyingi,halafu hawa watu wanaleta fujo sana katika nchi.
   
Loading...