Mguu wangu! Huu ndio udhaifu wangu kwake

Mguu wangu! Huu ndio udhaifu wangu kwake

Nikhil

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2013
Posts
361
Reaction score
120
Wakuu ni matumaini yangu mko poa.
Mimi ni mvulana miaka 20 niko chuo. Nimepata ajali ya kuungua na moto kwenye mguu wa kushoto nilipokuwa na umri wa miaka mitano na kusababisha mguu wangu kupoteza mwonekano wake wa kawaida . Ninachomshukuru Mungu ni kuwa una uwezo wa kawaida kama mguu mwingine wa kawaida!

Mguu huu umeniathiri kisaikolojia kwani sipendi watu wauone imenifanya mahali popote niendako nivae viatu au sandal na soksi .

Wakuu nimempata nimpendae kwa dhati na natumaini na yeye ananipenda sana ila hajui juu ya huu mguu wangu . Wana jf inaniuma sana kwani sina comfidence kwake kwa kuwa nashindwa kuwa free na juu ya hili nahisi nikimwambia anaweza niacha na nampenda sana. NIKO SERIOUS JUU YA HILI JE NIFANYE NINI?
 
haaa ujue mapenzi yanamaanisha ayapende madhaifu yako.
Halafu huyo si wako bana kwa mwanaume bado una long way to go.
Be a man bwana mwanaume hata aweje ni mwanaume tu.
 
dah! unaogopa kuachwa? we wakiume mkuu....una option nyingi sana....mwonyeshe hakika kama anakupenda hatakuacha...kama ni golddigger atakuacha na itakuwa better kwako..
 
Jiamini kijana mwambie tu atakupenda tu kama kweli ni wako unajua unaweza ukamwambia ndio akakupenda zaidi!Wanawake ni viumbe tofauti na unavyozania, na kama si wako wala isikuume atapatikana wa kwako.Kwani nani ajuae labda baada ya kukubaliana huenda hata yeye akapoteza miguu yake yote!Wangapi wamepata ulemavu sababu ya ajali na hawakutegemea kuwa hivyo.Mke mwema huletwa na Mungu kama Adamu alivyopelekewa hawa ndivyo na wewe utakavyoletewa na Mungu huyo huyo keep on praying.
 
++
Hiyo ni silaha njema ya kupata akupendae si anaekutamani.
++
 
Kama umempenda na anakupenda hakuna shida yoyote kukubali.

Wanawake ni viumbe wa ajabu sana, they are very easy to comprimise situations especially on physical appearance of the men.

Kuna wanaume hawana hata macho(Born blind) lakini wameoa mabinti wazuri ile mbaya. Sembuse wewe na kovu la jeraha la moto mguuni?
 
Hicho sasa ndo kipimo cha kujua kama anakupenda kwa dhati au laa! Fanya umwambie haraka
 
Kama una uwezo wa kumpenda mtu mwingine ambaye hata sio kiungo cha mwili wako, unashindwaje kukipenda kiungo chako mwenyewe na kuwa huru nacho hata kama kina kasoro??

Mwambie tu huyo Bi dada na hiyo itakufanya ujue kama kweli anakupenda kwa hali uliyo nayo au lah!!
Kama ni mbwai wacha na iwe mbai!!!
 
Hapo ushauri ni kujikubali kwanza then watu wengine watakukubali, otherwise usipojikubali ni shida sana utateseka
 
Acha kuuficha ili auone akubaliane n hali halisi, utaficha mpaka lini.

Ukipenda boga lazima apende na ua lake. Maana utajua pendo la kweli au n8 mpitaji.
 
Wakuu ni matumaini yangu mko poa.
Mimi ni mvulana miaka 20 niko chuo. Nimepata ajali ya kuungua na moto kwenye mguu wa kushoto nilipokuwa na umri wa miaka mitano na kusababisha mguu wangu kupoteza mwonekano wake wa kawaida . Ninachomshukuru Mungu ni kuwa una uwezo wa kawaida kama mguu mwingine wa kawaida!

Mguu huu umeniathiri kisaikolojia kwani sipendi watu wauone imenifanya mahali popote niendako nivae viatu au sandal na soksi .

Wakuu nimempata nimpendae kwa dhati na natumaini na yeye ananipenda sana ila hajui juu ya huu mguu wangu . Wana jf inaniuma sana kwani sina comfidence kwake kwa kuwa nashindwa kuwa free na juu ya hili nahisi nikimwambia anaweza niacha na nampenda sana. NIKO SERIOUS JUU YA HILI JE NIFANYE NINI?

Njia nzuri ya kupambana na udhaifu au tatizo ulilonalo, ni kwanza kulikubali tatizo hilo na kisha kulifanyia kazi. Wewe kwa sasa unaonekana ni kama hauikubali hali halisi uliyo nayo na ndiyo maana unahaingaika kufanya mguu wako ulioungua.

Kubali kuwa mguu wako uliungua na hakuna namna yeyote ile ambayo unaweza kuifanya ukabadili ukweli huo. Acha mchumba na marafiki zako wajue maana hiyo siyo dhambi ya kusema watu wakiona watakushangaa, ni ajali tu ilikupata sawa na ajali nyingine yeyote.

Jiamini na mwambie huyo mchumba wako live kuwa uliwahi kupata ajali ya moto na umeungua mguu. By the way, sidhani kama yeye aliipenda miguu yako, nafikiri alikupenda wewe na siyi hiyo miguu uliyokuwa umeificha.

Kama itatokea baada ya kumwambia utaona amebadilika na kiasi kapunguza mapenzi, mshukuru Mungu maana huyo atakuwa si wako, alikupenda kwa tamaa zake fulani fulani na si mke wa kukufaa.
 
Hebu jikubali na ujipende mwenyewe itakupelekea kuwa na furaha hata kama una kasoro kwa mwili wako,

kitu kingine mwambie ukweli halisi huyo mdada ili ajue kama ni kweli anakupenda utakuwa naye na km si wako
 
Wakuu ni matumaini yangu mko poa.
Mimi ni mvulana miaka 20 niko chuo. Nimepata ajali ya kuungua na moto kwenye mguu wa kushoto nilipokuwa na umri wa miaka mitano na kusababisha mguu wangu kupoteza mwonekano wake wa kawaida . Ninachomshukuru Mungu ni kuwa una uwezo wa kawaida kama mguu mwingine wa kawaida!

Mguu huu umeniathiri kisaikolojia kwani sipendi watu wauone imenifanya mahali popote niendako nivae viatu au sandal na soksi .

Wakuu nimempata nimpendae kwa dhati na natumaini na yeye ananipenda sana ila hajui juu ya huu mguu wangu . Wana jf inaniuma sana kwani sina comfidence kwake kwa kuwa nashindwa kuwa free na juu ya hili nahisi nikimwambia anaweza niacha na nampenda sana. NIKO SERIOUS JUU YA HILI JE NIFANYE NINI?
Mkuu inaonyesha huyo mwanamke unampenda kuliko akupendavyo wewe, sasa ili kujua upendo wake kwako muonyeshe na umwambie tuu!
 
Nikhil, pole sana, ila jiamini, tena wewe umeungua mguuni kiasi unaweza kuficha watu wasione, kuna dada yupo pale IFM anamalizia mwaka wa tatu sasa , inaonyesha aliungua kuanzia usoni , mpk mkono wa kulia, kiasi uso wake upande una ngozi nzuri upande umeungua, lakini ukimwona utashangaa wala haoni ni kitu cha ajabu na mcheshi na mwenye furaha kwa sababu amekubali alivyo. so nakushauri mwite huyo msichana , muonyeshe hilo kovu na mwambie kuwa uko hivyo, sasa yeye aamue kuwa na wewe au la! hapo utatambua kuwa anakupenda na kukujali au ndiyo wale wanaopenda pesa tu.
 
Kama una uwezo wa kumpenda mtu mwingine ambaye hata sio kiungo cha mwili wako, unashindwaje kukipenda kiungo chako mwenyewe na kuwa huru nacho hata kama kina kasoro??

Ushauri umetulia sana.
Natamani Moderator waiwekee sticky ili kila Nikhil akifungua thread hii aweze kuuona huu ujumbe.
 
Aah kaka, hebu jiamini, ni kovu tu hilo tena la mguuni, it will never kill you. Sasa lingekuwa usoni je, napata taabu kufikiria kwa kiasi gani 'lingekumaliza' kisaikolojia.... After all, kwa mkaka, wee jiweke smart tu everything else will flow, yaani unaogopa makovu kama mdada bwana.
 
kiongozi shukuru hata hilo! Je viwete nao watasemaje!! Jiamini! Na kubaliana na khali uliyonayo!!
 
Kuwa wazi tu umwambie kuliko kukaa bila kumwambia
 
Back
Top Bottom