MGONJWA WETU PALE ANFIELD YUPO HOI TAABANI

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
1,989
1,179
MGONJWA wetu pale Anfield yupo hoi bin taabani. Madaktari wamemzunguka na hawajui hata waanzie wapi. Mgonjwa anaumwa kila kitu katika mwili na kinachoshangaza ni kwamba ameumwa ghafla mno. Usicheke sana wakati huu mgonjwa wetu yupo hoi bin taabani.Awali wenyewe walikuwa wanaulizana mgonjwa wao anaumwa nini. Lakini sasa imefika mahala hata sisi wenyewe tunaulizana huyu mgonjwa anaumwa nini. Kila dawa inayojaribu kumtibu inaelekea kushindikana. Muda utaamua kama kweli atatibika. Tuache masihara kando. Liverpool wana shida gani? Miezi michache walikuwa katika hatua za mwisho mwisho za kutwaa mataji yote waliyoshiriki msimu uliopita. Nusura watwae kila kitu. Hakuna ambaye angeshangaa sana kama wangeweza kutwaa kila kitu.

Miezi michache iliyopita wao walikuwa wanaturingishia sisi wengine tunatamani kuwa wao. Walikuwa na kamsemo kao wanadai ‘imagine being us’. Kwamba ‘fikiria kama mngekuwa kama sisi’. Leo ni wao wanatamani walau wangekuwa kama Newcastle United achilia mbali Manchester United, Manchester City au Arsenal. Ni wao ndio wangeringa zaidi kuwa kama hawa.Nini kimewakumba? Kwa mtazamo wangu kuna mambo mengi. Baada ya ile staili yao maarufu ya soka ijulikanayo kama Gegen Pressing nadhani Liverpool wamechoka. Wachezaji wao waliokuwa wanautumikia huu mfumo wapo hoi. Miguu imekuwa mizito na miili ipo hoi.

Jurgen Klopp aliwaletea mifumo ya ukabaji wa pamoja kuanzia juu, katikati na chini. Liverpool walikuwa hawataki ukae na mpira wao hata kwa sekunde tano. Na baada ya kuurudisha walikuwa na kasi ya kukuletea tena mashambulizi. Ni kama vile walikuwa wanatumia dawa za kuongeza nguvu kumbe hapana.Mfumo ule unakuacha hoi baada ya miaka kadhaa. Kitu ambacho Pep Guardiola alikiweza katika kikosi chake ni utajiri wa kikosi katika kila maeneo. Usingejua eneo gani anaanza nani. Kulia angeweza kuanza Bernardo Silva au Riyad Mahrez. Kushoto angeweza kuanza Raheem Sterling au Leroy Sane. Katikati angeweza kuanza Sergio Aguero au Gabriel Jesus. Hata baada ya wengi kati yao kuondoka Leo bado anaweza kuanza Mahrez au Silva, katikati anaweza kuanza Erling Haaland au Julian Alcarez. Kushoto anaweza kuanza Jack Grealish au Phil Foden. Hapa nyuma akicheza yeyote kati ya Ilkay Gundogan au Kelvin De Bruyne bado wanakuwa na ubora ule ule tu.

Liverpool katika ubora wao kila ukifumba macho na kufungua kikosi chao cha kwanza kilikuwa vile vile tu. Kushoto anacheza Sadio Mane, katikati Roberto Firmino wakati kulia ni Mo Salah. Kila wikiendi maisha yalikuwa hai. Unafahamu fika kwamba kulia atacheza Trent Alexander Arnold na kushoto Andy Robertson.Leo rafiki zetu wamechoka. Naamini hata Mane huko alipo atakuwa amechoka tu. Hamna namna. Hii miaka takribani sita iliyopita kikosi chao kimekuwa na watu wale wale. Hawakuwa na watu wawili wawili wenye ubora unaokaribiana. Leo Salah anashindwa hata kumpiga chenga mtu mmoja aliyekuwa mbele yake. Zamani alizoea kupiga chenga walinzi hata watano na kufunga.

Ugonjwa huu wa kuchoka maarufu kama fatigue unaibua ugonjwa mwingine ambao sijui unatoka wapi. Kwa nini matajiri wa Liverpool hawakutia pesa ya kuchukua wachezaji wengine wenye ubora kwa ajili ya kukisuka kikosi mbele. Wakati ule wakiwa na Fabinho mwenye moto kwa nini hawakumchukua Thomas Partey kutoka Atletico Madrid. Wakaruhusu mchezaji wa aina hii aende Arsenal. Angekuwa Guardiola angefanya hivi. Wakati mwingine nahisi matajiri ni mabahili lakini wakati mwingine nahisi inawezekana ni ujuaji wa Klopp. Si ajabu Klopp amewafanyia Liverpool kitu kile kile ambacho Arsene Wenger alikuwa amewafanyia Arsenal wakati fulani. Ogopa sana kocha ambaye ana uwezo wa kumtengeneza mchezaji wa kawaida kuwa mchezaji wa kiwango cha juu zaidi (World Class).


Wenger baada ya kuwafanya akina Patrick Vieira, Thierry Henry, Ashley Cole na wengineo kuwa wachezaji wa viwango vya dunia baada ya awali kuwa wachezaji wa kawaida kabisa akaanza kudhani kila mchezaji wa kawaida anaweza kumbadilisha kuwa World Class. Aliamini Abou Diaby angeweza kuwa Vieira, akaamini Marouane Chamackh angeweza kuwa Thierry Henry, akaamini Denilson angeweza kuwa Gilberto Silva, akaamini Phillipe Sendoros angeweza kuwa Sol Campbell. Arsenal ikajifia zake. Klopp aliwanuia kina Mane, Salah, Virgil van Dijik, Trent na wengineo kutoka kuwa wachezaji wa kawaida mpaka kuwa World Class. Baada ya hapo kila ukiangalia wabadala wao wa leo unaona kabisa amekuwa akijaribu kufanya kitu kile kile. Bahati mbaya haimlipi. Sijui tatizo ni Klopp mwenyewe au matajiri wabahili maana hatuwezi kuwawekea dhamana matajiri Wamarekani. Labda wangekuwa Waarabu.

Ugonjwa mwingine ambao Liverpool inaumwa ni ule ugonjwa kweli wa majeraha. Hata kama ni kweli wamepoteza ubora wao lakini bado mchezaji mmoja mmoja wangeweza kuwasaidia. Badala yake wote wapo juu ya vitanda vya hospitali. Akina Diogo Jota, Dias, Van Dijik wote wapo hoi. Wengine kwa muda mfupi wengine kwa muda mrefu.Na hapo hapo kwa sababu timu yenyewe ipo hoi kuna ugonjwa mwingine ambao umewaathiri wengine. Wachezaji wapya kikosini tunafahamu kwamba ni wachezaji mahiri lakini kwa vile wameikuta timu ipo hoi basi wanashindwa kuonyesha ubora wao. Ubora wa timu huwa unawaambukiza wengine lakini ubovu wa timu pia huwa unawaambukiza wengine.

Wote tunafahamu kwamba akina Gapko na Derwin Nunez ni wachezaji wazuri lakini wamepishana na Liverpool iliyo bora. Kama hawa akina Gapko wangekutana na akina Liverpool iliyo bora si ajabu leo wangekuwa na makali makubwa. Leo wanacheza wakiwa katika kikosi ambacho hapana shaka kinavuja na kinatumia muda mwingi kufukuza mpira kuliko kufanya mipango. Kwa mfano, bado naamini ilikuwa rahisi kwa Trent kukua akiwa kinda pale Anfield kwa sababu alikuzwa katika timu ambayo muda mrefu ilikuwa na mpira. Leo anacheza katika timu ambayo muda mwingi haina mpira na mapungufu yake katika ukabaji yanaonekana kwa urahisi tu. Zamani alikuwa anafurahia kuwa beki mbunifu mpiga krosi na pasi lakini leo hata kukatiza katikati ni shida.


Mwisho wa yote haya kuna ugonjwa wa ajabu ambao kocha wao Klopp huwa anakuwa nao. Inadaiwa katika klabu alizokuwepo msimu wake wa saba mambo yanakwenda kama hivi. Hata alipokuwa Borussia Dortmund katika msimu wake wa saba maisha yalikuwa magumu kama hivi. Wakati mwingine jinamizi linakuandama kila unapokwenda. Baada ya wiki chache zijazo kama maisha yataendelea kuwa haya tutarudi hapa hapa, ukurasa huu huu, kujadili hatima ya Klopp Liverpool. Kwa sasa tukae kimya kwa sababu kama wenyewe watu wa Anfield hawasemi ‘Klopp Out’ sisi ni nani tuwe vimbelembele vya kudai atolewe? Kwa sasa tunachoweza kufanya ni kujadili tu magonjwa ya timu bila ya kumhusisha mwenyewe. Hatujui kwa kuelekeza lawama.
Source: Mwanaspoti
 
Msimu wa Saba huwa ndio msimu wa mwisho wa klopp kwenye team yeyote ,tofauti na hapo anawashusha daraja ....

Lakin Liverpool hawataki kuamin kabisa
 
Paragraph ya tatu umetoa jibu...

Huwezi kuwa na kikosi kile kile kwa misimu zaidi ya sita na ku-mantain your status....tena hatua za mwisho unaanza kutoa wachezaji muhimu kama Mane na widjnadum na upande wa Super sub Origi unawaleta wachezaji wapya kwenye ligi na kutaka wawe kwenye "first eleven". kwa kasi eti kisa huko walikotoka walikuwa wa moto 🤕🤕....

Ok matajir wame-fail na ma-scout wetu wamechoka sasa hawana jicho la kuona wachezaji vipanga....
Kumbuka tulimuacha Halaand for 45 millions na kumchukua Nunez for 75 millions ukijumlisha baadhi ya vipengele (add ons ) anagonga 100m $.....

Final say,
Acha msimu huu wachezaji wapumzike, misimu 6 ya moto siyo lelemama tena kumbuka unapambana dhidi ya man city aliyevunja hadi masharti na vigezo vya usajiri kwa pesa 😋😋😋 , wale bata tusiwape stress mara za top four(EUFA) au top six(Europa)....wasisumbuliwe na hofu ya kufukuzwa na tena wawekezaji wapya waje tutarudi barabarani tu "We are the KOPS"..
Msimu huu tupambanie kutokushuka daraja (over kama umenisoma).........🤠🤠🤠🤠
 
Back
Top Bottom