Mgonjwa wa sukari ale nini?

superfisadi

JF-Expert Member
May 22, 2009
553
52
Naomba mnisaidie nina ndg yangu amepimwa last wk kaambiwa anatatizo la sukari ilikuwa 7 jana kaenda kupima kaambiwa 18 ninaomba mnisaidie atumie vyakula vya aina gani isiendelee kupanda ?
 
hivi humu jamvini hamna madr au watu wanaojua namna ya kukabiliana na gonjwa hili
 
chumvi kwa sana.
sukari aachane nayo.
mi si dr natumia common sense.
pole sana
 
Insulin ,imeshindwa kazi yake ,kwa hali hiyo kongowe linashindwa kudhibiti sukari mwilini. Aepuke hasira,asifanye kazi bila kula muda mrefu,aepuke mishituko. Usitumie sukari ,usitumie wanga mwingi . Pendelea ndizi ,za kuchemsha .ugali wa mtama na ulezi .punguza nyama.kula sana mboga za majani. Usitumie beer sana .kwa kifupi kula vitu visivyo na quality.

Pia jiande kupoteza weight ya mwili .punguza mawazo. Utapoteza nguvu za kiume kama ni mwanamme. Bao moja ni shida .kama una mke kibinti una kazi. Nimeandika yote through experience from ma dady .anaishi mzima wa afya toka aupate 1996
 
Kisukali soooo,dingi anacho toka 2002 ila kwa sasa yuko level mitishamba ndo imemsaidia pamoja na sala za apa na pale
 
Tembelea hospital na upate ushauri wa kitaalam. Kwani siku hizi kuna mabadiliko ktk ulaji wa vyakula.[wanaruhusiwa kula chakula chochote]
 
Njia tano za kufuata kama mwongozo wa kukabiliana na ugonjwa wa Sukari

Mara tu unapoambiwa kuwa una huu ugonjwa, linaweza kuwa ni jambo ngumu kulikubali na kukabiliana nalo. Hisia za kushtuka, hasira, kutamauka, kuogopa na kuwa na majonzi ni za kawaida kwa yeyote baada ya kupata habari kuwa ana ugonjwa wa sukari. Hata hivyo una maisha yako ambayo ni muhimu uyaokoe. Fuata hizi njia tano, kwa uangalifu ili ujue la kufanya wakati wa kukabiiana na hiyo hali yako mpya ya kuwa mgonjwa wa ugonjwa wa sukari.

Hatua ya 1: Jifunze yote yanayokupasa kuhusu ugonjwa huu.

Jifunze na uelewe kila kitu ili ujue unachoshughulikia. Muulize daktari ambaye anajua yote kuhusu ugonjwa huu na aliye na uwezo wa kujibu maswali yako yote. Tambua aina ya ugonjwa wa sukari unaokusumbua. Ni hali gani inayokufanya ujipate hatarini?

Jua vyema kiwango cha sukari kilichoko mwilini mwako na aina ya dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini mwako itakayokufaa maishani mwako. Ni shida gani zinazotarajiwa iwapo utashindwa kuuthibiti ugonjwa huu kwa kiwango kinachotakikana, kulingana na mhudumu wako wa kiafya. Utafiti wako umekusaidia kupata maarifa unayostahili. Kuweza kukabiliana na ugonjwa huu kikamilifu.

Hatua ya 2: Badili mtindo wako wa ulaji

Ili kuweza kukabiliana na kiwango cha sukari mwilini mwako ni muhumu upunguze uzani usiofa, kiasi cha chakula unachojipakulia ni lazima kipungue usifikirie kwa misingi ya utaratibu na ulaji bali njia bora ya kutunza afya yako kwa kula chakula kifaacho vyakula vifuatavyo, visikose kwenye orodha ya vyakula unavyohitaji katika taratibu wako wa ulaji; mboga, matunda, chakula cha kutunza mwili na cha kupatia nguvu mwili wako. Zungumza na daktari wako wa utarativu wa ulaji bora kuhusu mpangilio mwafaka wa mlo utakaouzingatia kwa wakati huu.

Hatua ya 3: Panga mpangilio wa kila siku wa kudumu

Watu wengi walio na ugonjwa huu mara nyingi huwa wanene kupita kiasi na wenye uzani mzito. Hivyo basi ni muhimu, ufanye mazoezi ya kila mara kama njia mojawapo ya kukabiliana na ugonjwa huu. Ni lazima kuwa daktari wako atakupa ushauri utakaoutaka upunguze uzito. Mazoezi mwafaka zaidi ni kuwa na mpangilio utakaokufanya uwe na nguvu za uthibiti wa moyo wako kwa kufanya mazoezi yanayolenga hayo mambo mawili. Baada ya ushauri wa daktari unaweza kuamua kujiunga na chumba au kiwanja cha michezo ya kuzoeza viungo vya mwili ama ujiunge na kundi la YMCA/YWCA ili upate msaada unaohitaji kuendelea kuyathibiti maisha yako na hali yako ya wakati huu. Kama sivyo, kuna namna nyingi za kujipangia mazoezi ya kibinafsi pale pale tu nyumbani.

Hatua ya 4: Meza dawa zako inavyotakikana

Watu wengine walio na aina ya pili ya ugonjwa huu huhitaji kumeza tembe zao inavyostahili ama kujidunga dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini ili miili yao itumie sukari iliyomo katika matunda na mimea kupata nguvu. Aina hii ya sukari huvunjwavunjwa tena wakati wa kuyeyusha chakula kinywani na tumboni ili kifae kuchukuliwa na damu mwilini kama ifanyikavyo na chakula cha namna kilichomo katika nyama, ute wa yai na samaki (chakula cha kutunza mwili) Dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini haipatikani kwa hali ya tembe. Yaliyo chini ya ngozi yako ili ingiie mara moja ndani ya damu yako.

Hatua ya 5: Tafuta usaidizi (msaada)

Huenda ikawa, utaweza kukabiliana na huu ugonjwa bila shida lakini ni muhimu utambue kuwa unahitaji msaada wa watu wengine ili mzigo ukuwie mwepesi kidogo. Tegemea jamaa na marafiki wakutegemewa ambao watakuwepo kila mara utakapohitaji msaada wao, katika hiyo hali yako mpya ya kisasa. Jishughulishe na vikundi vya watu walio na hali sawa na yako, pia jihusishe na shughuli za kijamii na kutafuta pesa na kuelimisha watu wanaoishi karibu nawe kuhusu ugonjwa huu.

Usisahau kubonyeza hapo palipo andikwa hivi (Thanks)
 
DAWA YA UGONJWA WA KISUKARI

Dawa ya Sukari ! Wabilahi Taufiq


Dawa ya Sukari (Diabetes)

Sheikh Saleh Mohammed Tuwaijiri (May Protection of Allah be on him),

Qadhi Mkuu wa korti ya Tabuk kafanya uchunguzi mkubwa kwa kuvumilivu

na kwa subira kubwa mpaka kupata hii dawa ya magonjwa ya sukari.


Siku hizi watu wengi khususan watu wazima, wanaume na wanawake

wanataabika sana kwajili ya ugonjwa wa sukari.



Ingredients
:



1 – Unga wa ngano 100 gm


2 – Gundi (umefanan na ubani wa kiarabu lakini hauna harufu) 100 gm


3 - Shaair 100 gm


4 - Habba Soda 100 gm



Namna ya kutengeneza



Chemsha hivyo vitu juu katika vikombe 5 vya maji kwa muda wa dakika

10.
Zima moto na wacha ipowe. Ikisha kupowa chuja na utie katika chupa.



Matumizi



Kunywa kikombe kidogo kila siku asubuhi kabla ya kula chochote kwa

muda wa siku 7.
Wiki ya pili kunywa siku moja na uwache siku moja.

Insha-Allah baad hizi wiki mbili utapona na utaweza kula chakula kama

dasturi.
Sheikh anaomba muwapelekee wenzune wapate na wao

kunufaika.
Insha Allah Allah atajaalia iwe dawa kwa kila mwenye haya

maradhi. Aameen.
Kwa hisani zenu musiwasahau kwenye dua zenu Sheikh,

alieye tarjum kwa Kiswahili na kila anaye ipeleka mbele.
 
Back
Top Bottom