Mgonjwa wa ajabu ambaye hakuwa binadamu

Mgonjwa wa ajabu ambaye hakuwa binadamu

Military Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2019
Posts
761
Reaction score
1,480
IMG-20200505-WA0016.jpg


Ilikuwa mwezi Juni 1972 ambapo mwanamke mmoja alionekana katika hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center huko Los Angeles, California US. Hakuwa na chochote zaidi ya gauni lake jeupe alilovaa lililokuwa limetapakaa damu, hii haikuwa ajabu, kwasababu ni tukio la kawaida tuu kutokea katika hospitali nyingi.

Ajabu ilikuja pale mwanamke huyu alipoonekana kuwa na mambo kadhaa ya ajabu.

Moja ni mwonekano wake usio wa kawaida, hakuonekana kama binadamu wa kawaida, kila kitu alifanana na Mannequins, sura yake ilikuwa kama ya Mannequin, hakuwa na macho ya kawaida, uso wake ulikuwa umepakwa rangi.

Mannequins ni ile midoli inayowekwa nje kwenye maduka ya nguo, inavalishwa nguo ili kuvutia wateja kununua nguo hizo.

Kuanzia alipoingia, akapokelewa na kuingizwa katika chumba maalumu, hakuongea chochote, madaktari hawakupata jibu lolote la maswali waliyomuuliza, hawakuwa wakiskia amani kumuangalia usoni hata kwa sekunde mbili tuu, hakuwa wa kawaida ndio, lakini waliona ni vyema wampokee na kuutaarifu uongozi wa juu wa hospitali hiyo.

Daktari mmoja alipotaka kumuongelesha kwa nguvu ghafla akapambana na nguvu ya ajabu, wafanyakazi wenzake wakamshikilia huku mwili wake ukiwa unataka kunyanyuliwa juu na nguvu isiyoonekana, mwanamke huyo akamgeuzia macho yake yaliyokuwa kama ya mdoli na kisha akatabasamu. Wakakimbia.

Kama ambavyo daktari huyo alikimbia, hata wale walimshikiria pia walikimbia, mwanamke huyo hakuwa na meno ya kibinadamu mdomoni, alikuwa na Sharp Spikes ndefu zinazotisha, yaani ni kama yale meno ya kwenye msumeno hivi.

Wakati madaktari wote wamekimbia, dokta mmoja wa kiume alisimama kwa mbali na kumuuliza "wewe ni nani?", Mwanamke huyo akageuza shingo yake akimtazama huku akiwa bado anatabasamu, kulibaki kimya kwa dakika kadhaa bila kujibu, wakati huo taarifa zilikuwa zishatolewa kwa vyombo vya usalama.

Baada ya muda akajibu, "I...am...God"

Hakuna maelezo ya uhakika ya ni nini kiliendelea baada ya hapo, lakini taarifa ilisema kuwa baada ya madaktari wote kukimbia na kumuacha mwanamke huyo ndani, akatoweka, hakuwahi kuonekana tena.

Written by Military Genius

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Picha haioneshi kama kweli alitapakaa damu,iko wapi damu.

Au alibadilishwa nguo ?

Ukisema picha haina rangi sio kweli kwa sababu kama ni damu ungeonekana uweusi fulani hivi.
 
Hakuna Mungu wa ajabu vile labda miungu
 
Kuna thread moja ilikuwa inasema KUNA WATU WALIKUWA WANALIPIA VITI BAR. Something like that.
Mjadala wenu ulikuwa ni mtamu hakika
Thanks nimekumbuka, dada yako alikuwa anasema wanalipia viti mimi nikampinga kuwa kinacholipiwa ni Huduma, services only, hicho Kiti ni just Reservation’s tu to secure your normal sitting space or position
P
 
Fiction ni noun hivyo kwenye stories kuna fiction na non fiction. Fictitious ni adjective ya verb ya fiction.
P
"Fiction - Noun" + "Story - Noun", kama ulivyoandika "Fiction story". A noun can not qualify another noun, only an adjective, can! Kilangila.
 
"Fiction - Noun" + "Story - Noun", kama ulivyoandika "Fiction story". A noun can not qualify another noun, only an adjective, can! Kilangila.
Wengine tumesoma shule za St. Kayumba, enzi za Mwalimu, tukifundishwa na waalimu wa UPE, hivyo mambo mengine sio zaizi yetu itakuwa ni kutuonea bure. Kuna stories za aina mbili tuu duniani, Fiction na Non Fiction. Hii story ni fiction.
P
 
Back
Top Bottom