Mgomo wa wasafirishaji mabibo hostel waendelea kutesa wanafunzi.

Mgomo wa wasafirishaji mabibo hostel waendelea kutesa wanafunzi.

samirnasri

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
1,388
Reaction score
217
Madereva wa magari aina ya costa zinazosafirisha wanafunzi wa chuo kikuu cha dar es salaam kutoka mabibo hostel kuelekea campus ya mlimani waligoma kutoa huduma hiyo tangu jana alhamis na kuendelea siku ya leo. Wanafunzi wengi sasa wanalazimika kupanda magari mawili mpaka kufika chuo wakianzia safari mabibo hostel hadi ubungo na baadaye kupanda gari kutoka ubungo mpaka chuoni kwa jumla ya shilingi 600. Wanafunzi wengine wnalazimika kutembea kwa miguu kutoka hostel za mabibo hadi chuoni kutokana na hali ya uchumi kuwa mbaya kwa wanafunzi wengi ambao bado hawajapata pesa za kujikimu za awamu ya pili. Sijafanikiwa kupata sababu ya mgomo huo wa wasafirishaji.
 
Back
Top Bottom