CWT tafadhali toeni tamko walimu tupotayari kugoma. Mkoba mbona hueleweki? Tumesaini fomu ya kukubali mgomo na mkasema tusubiri tangazo la siku ya kuanza mgomo sasa tunasikia kauli zisizo za kiungwana mara ni kikundi cha watu kilichoanzisha vuguvugu la mgomo si CWT, mara mgogoro haukufuata sheria. Kama Mkoba na baraza mnaogopa basi mjiuzuru maana mnatuchanganya walimu. Ikiwezekana tuanzishe nasi Jumuiya ya walimu maana tumechoka kuonewa. Natoa tahadhari kwa mahakama kuacha kufanyakazi kwa maelekezo ya CCM mnapoteza uhalali wa kuwa wasimamia haki katika taifa, kila mgomo mnasema haukufuata sheria. Walimu tuungane pamoja kutetea haki zetu, sisi ndiyo tunaweza kujitetea si bunge wala si mkoba. Majaliwa aache ubabaishaji chini ya CCM. KUWA BUNGENI NA KUWA NAIBU WAZIRI ASIJIONE YEYE NI KILA KITU. NAOMBA MNYIKA UTOE HOJA KUWA NAIBU WAZIRI ALILIDANGANYA BUNGE KWA KUSEMA HAKUNA MGOGORO NA CHAMA CHA WALIMU WAKTI UPO.