Mgomo wa Walimu wazidi kusambaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa Walimu wazidi kusambaa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MziziMkavu, Jun 27, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais wa Chama cha Walimu nchini Tanzania (CWT) Bw.Gratian Mukoba


  Wimbi la mgomo wa walimu limeendela kutandaa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na sasa mkoa mpya wa Simiyu baada ya Chama Cha Walimu (CWT), wilayani Bariadi kuanza kutoa elimu ya jinsi ya kupiga kura ya kuafiki au kukataa kwa kujaza fomu namba moja inayokusudia kuwepo kwa mgomo huo mapema mwezi ujao.

  Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Bariadi, Julius Mategemeo, jana aliiambia NIPASHE mjini Bariadi kuwa elimu ya jinsi ya kujaza fomu hizo maalum inatolewa baada ya kusambazwa kwa fomu namba moja kwa walimu wote katika shule za msingi, sekondari, vyuo na taasisi wilayani humo.

  Mwenyekiti huyo alisema upigaji wa kura unalenga kuishinikiza serikali kutimiza ahadi yake na kuitaka iwaongeze mishahara walimu kwa mwezi kwa asilimia 100 na itoe posho ya kufundishia kwa walimu wanaofundisha masomo ya Sayansi kwa asilimia 55 na walimu wa masomo ya Sanaa kwa asilimia 50.

  Pia kura hiyo ni pamoja na kuitka serikali itoe posho ya mazingira magumu kwa walimu wanaofanya kazi kwenye wilaya zenye mazingira magumu kwa mwezi kwa kiwango cha asilimi 30.

  Katibu wa CWT Wilaya ya Bariadi, Posian Gervas, alisema Mratibu na Msimamzi wa zoezi la upigaji kura ni Mwakilishi wa Chama cha Walimu Tanzania katika shule, chuo au taasisi.

  Aidha, Gervas amehimiza walimu kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo na kupiga kura zao za siri kuafiki au kutaa kuwepo kwa mgomo huo.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi, Deogratius Hella, akizungumzia utekelezaji wa madai mbalimbali ya walimu hao, alisema katika barua yenye kumbukumbu namba E.10/34/Vol.III/10 ya Mei 29 mwaka huu alifafanua kuwa walimu 367 wa shule za msingi na 118 wa sekondari walirekebishiwa mishahara yao na kubakia 164.

  Mgomo huo wa walimu unatarajiwa kuanza mwezi ujao na utahusisha walimu nchi nzima.

  CHANZO: NIPASHE

   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 3. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Ukombozi kwa mwalimu wa tz utaletwa na mgomo, cyo majadiliano, bravo teachers waigeni madaktare mpate nafuu ya maisha.
   
 4. Fekifeki

  Fekifeki JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,163
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Jana majira ya saa 22:15, nimesikia habari ktk kituo cha Radio Sauti ya Injili Moshi, ikisema walimu wilayani Hai watagoma na watakaa nyumbani bila kwenda shuleni kwa muda wa siku tatu! serikali isipotimiza madai yao watatoa tamko lingine! sijui serikali dhaifu imejiandaaje kulikabili hili!?. yetu macho!
   
 5. M

  Malolella JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 367
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Dk ulimboka kakamatwa na haijulikani kapelekwa wapi. Mukoba nae ajiandae kutekwa. Hii ndio tz. Chezea ccm wewe!
   
 6. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,812
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Kazaneni waalimu ili nasi tunaotaka kusomea ualimu tuje kupata unafuu wa maisha.
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  mimi walimu siwaamini kabisa watatishwa kidogo tu kesho yake kazini..
   
 8. MCHONGANISHI

  MCHONGANISHI JF-Expert Member

  #8
  Jun 27, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 363
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  Labda! Safari hii tutafanikiwa walimu tuna mwamko tatizo liko kwa CWT je? Safari hii hawatakuwa madalali wa haki zetu? Sisi tutapiga kura Kama fomu zinavyoelekeza na mgomo unakubalika hapo! Matokeo yakitoka hatua za mgomo zichukuliwe hatutaki kuona sarakasi za CWT, Sijui Mara ooooh mazungumzo hatutawaelewa na baada ya mgomo na AUDITING ifanyike CWT mambo yawe wazi! Hakyanani safari hii tutatiana wenyeyewe bakora mwamko ulioko Kanda ya ziwa ungeenea nchi mzima ingekuwa safi sana....... Angalizo maafisa elimu na maafisa wa TSD wasitishe walimu ni haki Yao wanafai
   
 9. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #9
  Jun 27, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  kama mgomo wao ulishawahi kusitishwa na mahakama saa 9 usiku na asubuhi yake hawakugoma ije kuwa leo. hebu tuache unafiki kama mmeamua kugoma gomeni ki ukweli.
   
 10. t

  tisa desemba JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  natangaza kutokuwa na imani na CWT, HAWANA NIA YA DHATI YA KUWATETEA WAALIMU. wapo kisiasa zaidi.
   
 11. A

  Aswel Senior Member

  #11
  Jun 27, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 114
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Fanyenii kweli walimu magamba yakune vichwa.
   
 12. S

  Slaker JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2012
  Joined: May 11, 2012
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Dain chenu ....bhana hadi kieleweke 2,......
   
 13. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Walimu bado sana!! hili ni gelesha tu!!
   
Loading...