Mgomo wa Vyombo vya Usafiri; Mabasi, Coaster na Hiace kati ya Uvinza na Kigoma

Rusumo one

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
3,077
3,609
Kichwa cha habari hapo juu kinajieleza.

Sisi wananchi wa Uvinza na viunga vyake tunaomba Serikali yetu tukufu iingilie kati suala la mgomo wa vyombo vya usafiri Kigoma-Uvinza toka juzi usafiri haupatikani tunashindwa kufanya shughuli za kimaendeleo ambazo zinatufanya kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine na chanzo kikubwa tunaambiwa na madereva pamoja na wamiliki wa vyombo vya usafiri kuwa Rushwa imekithiri kwa kila geti kuanzia pale Uvinza, Kibaoni, Basanza, Maragarasi, Kazuramimba relini.

Kila uchwao wanataka pesa kuanzia elfu 5 kwa kila geti la ukaguzi polisi wanataka pesa na migambo nao wanataka pesa yaani gombania goli vyombo vya usalama, TAKUKURU vipo na vinajua huu upuuzi ukifanyika alafu wananchi tunateseka sasa kamanda Mutafungwa anza na hili kuanzia leo Toa DTO na vijana wake unda upya kikosi cha trafiki Uvinza ukishindwa kufanya hivyo majina ya askari wako wachafu wanaotukwamisha tutawataja majina hadharani wananchi wamechoka na kero hii Uvinza.

Haya mageti/barriers ni chanzo kikuu cha Rushwa na ujambazi katika hii Wilaya magendo nyingi zinapita kwa magari na pikipiki mchana kweupe kuna mgambo alikuwa mtiifu kwa Mola wake alitaka kuchoma uozo huu kwa JPM pindi amefika kwa kampeni walimtoa kibaruani haraka sasa ngoja tumwage mboga na ugali maana uozo umezidi.

CC
RC KIGOMA
IGP
DG PCCB
DG TISS
 
Rushwa tena?! Na wakati tunaambiwa kuwa hii ndiyo serekali pekee tokea ukoloni ambayo imefanikiwa asilimia 100 kudhibiti rushwa!

24577890.jpg
 
Huu ni uongo wa dhahiri, awamu ya 5 kwa sasa hakuna rushwa kabisaa.

Nasema uongo ndg zangu, mniombeeeeeeeeee.
 
Back
Top Bottom