Mgomo wa madereva ndani ya ngorongoro conservation | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa madereva ndani ya ngorongoro conservation

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by wasaimon, Feb 21, 2012.

 1. wasaimon

  wasaimon R I P

  #1
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna mgomo wa madereva ulioanza toka saa nne asubuhi leo mpaka muda huu hakuna gari yeyote ya utalii inaweza kupita eneo la Oldupai, mpaka sasa magari zaidi ya 100 yameshindwa kuendelea na safari.

  Chanzo cha mgomo huo ni gari moja ya utalii limeanguka leo asubuhi likiwa na wageni, watu wa Hifadhi ya Ngorongoro walipewa taarifa lakini hawajajitokeza ktk kutoa msaada, madereva wa utalii wamekasirishwa na hicho kitendo.

  Sababu kubwa ya ajali hiyo kutokea ni ubovu wa barabara na hii barabara inamilikiwa na wao (Ngorongoro Conservations Area) na tambua kila gari na abiria wake wanalipia transist ambayo kwa kila mgeni ni $ 50 na Mtz ni Tsh 1500/= gari ndogo lenye 2000kg Tsh 10,000/=, gari zaidi ya 2000kg - 7,000kg Tsh 20,000/= wanahoji kama kila gari na kila mwanadamu anepita tu analipa pesa iweje washindwe kutengeneza barabara.

  Na ukipata ajali ndani ya eneo lao faini ni Tsh 50,000/= kwa gari lenye kg 2000 na zaidi ya 2000kg - 7000kg faini yake ni Tsh 100,000/=
   
 2. Chali wa Moshi

  Chali wa Moshi JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 258
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tunakwenda wapi nchi hii??

  AIBU TUPU.
   
 3. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Nchi hii ni masaburi kweli kweli.
   
 4. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Sasa wageni wa watu wamewalipa kina nani? Wapeleke wageni maana hawajaletwa na serhkali, wageni wametoka mbali kuja kuenjoy na wamelipa pesa nyingi kwenye kampuni zao waache ujinga hao madereva.
  Na ndio maana kuna sherha inawataka kuwa na gari ambayo ni 4WD, hawaelewi maana yake? Suala la hilo gari kupata ajali watalalamika wenye kampuni au kwa umoja wao wapeleke malalamiko kwenye mamlaka.
  My concern ni hao wageni wanakuja kwa ratiba na wanakuwa na fixed budget sasa sijui wakichelewa ndege watawaongezea extra fee!
   
 5. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2012
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Ni sehemu ya utalii! Tena wanafurahi kuona hivi maana picha zinapigwa kwa sana na videos, kampuni ya NYANZA feat spika wa kabla ya sita wamepalilia barabara kipande kifupi kwa 10Billion just kupalilia! Hao wageni we naona unawathamini thaaaaaanaaa eeeh!
  Je sisi tunaopoteza muda mwingi hivi kuwa na li CCM nani atatulipa muda wetu?

   
 6. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Mie naongea kama mfanyabiashara na siongelei siasa zako za cdm au ccm hazinihusu, we endelea kutoa povu tu wakati wenzio wanatengeneza hela.
  My concern kwa hao wageni ni kubwa coz wamelipa pesa kwenye makampuni binafsi ili wapelekwe kuenjoy, we unadhani Arusha kuna mzunguko wa dollar kwa sababu gani? I bet wewe kila unachofikiria ni unawaza cdm na ccm, wakati mwingine jaribu kuwaza kibiashara, najua watu wengi wanapenda kuajiriwa kama wewe, usipoteze muda kufikiria siasa kila wakati bob! Think!
  Kuwathamini wageni kama wamekulipa it is a must, suala la uzungu, ujapani, uarabu wao sio tatizo as long wamekulipa bro au hujui wao hawahusiki hapo? Narudia tena, jifunze kufikiria mambo mengine sio kila saa unawaza siasa itakutia umasikini na utakufa kwa stress while Tanzania is a land of opportunity!
   
 7. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Unaongelea 10 bilion imeliwa, its ok kukasirishwa ila unapogoma unamgomea nani? We dereva na njaa yako unajua mwenye kampuni ametoil kiasi gani mpaka kuwashawishi hao wageni waje bongo na sio kenya au namibia?
  Kama barabara mbovu narudia tena kukukumbusha kuwa magari yote ya tours kisheria yanatakiwa kuwa 4WD sasa wewe endelea kulalamikia barabara na ccm yako, kama hela ishaliwa we peleka wageni tengeneza pesa yako halali, period.
  Ila naweza kuwa naongea in parables ukawa upeo wako hauwezi kutengua methali.
   
 8. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Jamani nchi hii inaliwa!
   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Yani siyo Nchi inaliwa!
  Ni kwamba imeuzwa kitambo sana!
   
 10. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  We unafikiri wamepelwkwa kwa vitz???ubovu wa barabara ni jukumu la makampuni ya tours?
   
 11. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,165
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kiasi fulani hongera!,lakini pia pole sana kama wewe mi mfanyabiashara usiyethamini mali yako
  Vilevile pamoja na raslimali watu,
  *kwa nini usijiulize binafsi kwa nini NCAA wanakuharibia biashara kwa kutotengeneza barabara?
  *Je barabara ingekuwa nzuri hawa madereva wangefikia hatua hiyo?
  *Umewahi kuja binafsi na gari lako ukiwa unaendesha umebeba familia yako huku porini? Kama ni ndio,je mke wako alijisikiaje?
  *Kwa taarifa yako ni haohao wageni ambao hufikioa mahali wakawashangaa madereva wao jinsi wanavyovumilia kufanyia kazi katika mazingira magumu kiasi hicho.
  *Kama wewe ni mfanyabiashara unapaswa kumlaumu rais na serikali yako kwa ufisadi wa NCAA wanaotutangazia kila uchao magazetini.
  *Badala ya kutangaza utalii kwenye chanel kama Animal planet na National Geographic, wao wanatangaza utalii kwenye CNN utafikiri ni tukio la vita.

  Baada ya hayo machache tafakari na chukua hatua........
   
 12. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,165
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hakika kama identity yako ingekuwa open,bila shaka ungepata shida sana kwa kauli yako isiyo ya kiungwana kwa madereva wetu, kwamba "NJAA ZAO"
  *Lakini kumbuka kwamba Tour operator,kama mfanyabiashara anamtegemea sana dereva wa utalii,nikiwa na maana kwamba ni dereva huyohuyo na njaa zake ambaye hukaa na mtalii hu sika {ingawa wewe umemuita mgeni ilhali huwa haji kwako bali kwa nyumbu} kwa 100% ya ziara yake nchini na mafanikio ya safart hufanikishwa na dereva pale anapofanikisha kuwapeleka porini salama na kurudi wakiwa wameridhishwa na huduma zake zote,akiwa si dereva tu,bali guide pia.na wewe mfanyabiashara huishia kukusanya noti na kumbusu mkeo mjini,wakati huyu dereva na mgeni wako wakirukaruka kwenye mashimo huko ngorongoro

  Je.? Hiyo ndiyo hospitality unayotaka kutuaminisha tukuamini wewe mfanyabiashara wa kitanzania?
  Unafikiri uzembe huu ungekuwa kwa majirani zetu kenya wangeuvumilia kwa kiasi hicho?
  Je umejaribu kwenda nchi zingine jirani kama rwanda ukauona utalii wao wanavyoujali?

  Mimi najaribu kuisoma taswira yako na sipati jibu zaidi ya kukuweka kundi la wale waliowahi kutwambia watanzania tule majani lakini ndege ya mkuu iletwe.wewe kwako pesa ndio kila kitu,no matter imepatikanaje.
  Nalazimika kuamini...
  WEWE NI PAKA MWEUSI ANAYEMFUKUZA PANYA MWEUSI KATIKA USIKU WA GIZA!
   
Loading...