Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,582
- 6,627
Abiria wanaotumia njia ya makumbusho kuelekea Mwenge wakitokea Tandika na Mbagala leo wameonja Joto ya jiwe kwa takribani masaa manne baada ya mabasi yanayoptumia kituo cha ndani kugoma kupeleka abiria mwenge kutokana na ubovu wa barabara za ndani wanazotumia kupita kuelekea kituo cha mwenge.
Sakata hilo lilianza pale magari yalipofika kituo cha ndani cha makumbusho na kuwashusha abiria wote na kugoma kuendelea na safari ya kuelekea mwenge,ndipo mzozo mkubwa ulipozuka na kupelekea Sumatra na vyombo vya Usalama kufika eneo La Tukio na kuweza kuongea na madereva hao,lakini madereva hao na makondakta waliendelea kugoma mpaka pale walipohaidiwa kuwa ndani ya wiki moja barabara hizo zitakuwa zimerekebishwa na kuwa nzuri,hivyo watumie njia kuu kuelekea mwenge.