Mgomo wa madaktari una ajenda ya siri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa madaktari una ajenda ya siri?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nyetk, Mar 7, 2012.

 1. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Sote tunakubaliana kuwa madaktari wanayo madai ya msingi wanayotaka serikali iwatekelezee, ila kinachoanza kijikita sasa katika fikira zetu ni namna ya kudai haki zao na uhalali wa kila njia watakayotumia kudai haki hizo. Swali kubwa hapa ile “Principle of double effect” ina-aply namna gani katika hili au kuna kitu kinachokinga tusitumie fikra hii sahihi? Najaribu kutegua kitenawili hiki.

  Miaka ya nyuma katika nchi yetu (kama ilivyo bado katika nchi nyingi duniani) sheria zetu zilizuia mwajiriwa kuanzisha na kumiliki biashara yenye ushindani na ile ya mwajiri wake. Mfano Mwalimu mwajiriwa asifungue shule binafsi inayofanana na ya mwajiri wake, muuza duka la spea asifungue la kwake kama hilo, daktari mwajiriwa asifungue biashara kam ya mwajiri wake, nk. Aliyetamani kufanya hivyo basi ilimbidi kwanza kuacha kazi ya kuajiriwa ndipo afungue shuguli kama ya mwajiri wake wa zamani. Sababu za sheria hii ziko wazi; kukwepa masahibu yanayotokana na mgongano wa maslahi.

  Sheria hii iliondolewa bila tathmini ya kutosha na sasa waajiriwa wengi nchi hii wanamiliki biashara kama za waajiri wao. Mfano madaktari bingwa wa Muhimbili na Oshean Road – akina Massawe, Marro, Mgaya, Lymo, Macha, Kamugisha....... wote wanamiliki kliniki/zahanati za kwao na sote ni mashahidi ya kinachoendelea. Serikali haijafanya tathmini kuona athari za uwajibikaji wa watumishi wake wanaomiliki miradi inayofanana ya ajira zao. Sasa hivi imeshapanda zaidi ya kupungua uwajibikaji. SASA NI HUJUMA YA WAZI MCHANA KWEUPEE!
  Maswali ambayo watu hawajiulizi katika migomo hii ni kama haya:
  1. Kwa nini mgomo wa madaktari umesimamiwa kidete zaidi na madaktari bingwa wa Muhimbili?
  2. Kwa nini madaktari hawa wanakwepa sana muafaka na wako tayari kufukuzwa kazi na mwajiri wao?
  3. Mnadhani wakati wa mgomo mabingwa hawa wanakuwa wamekaa majumbani kwao wanapulizwa na feni?
  4. Nani atakubali afe kama kuna uwezekano wa kumwona daktari yuleyule mahali pengine?

  Ungefanya tathmini ya mapato wanayoingiza madaktari binwa hawa kwenye kliniki zao wakati wa migomo kama hii hata wewe ungependa migomo iwe kila siku laiti ungekuwa mmoja wao!

   
 2. d

  dav22 JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,902
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  ebana naskia Waziri kawasilisha rasmi barua ya kujiuzuru wadhifa wake hii habari ina ukweli wanajamvi??
   
 3. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  Tutatathmini mangapi? hata ubovu wa mfumo mzima na miundombinu katika utoaji huduma za afya ni tatizo kuliko hata huo mgomo wa madaktari.. kwa taarifa yako miundombinu katika afya ndio no 1 killer kuliko hata huyo daktari anayegoma...
   
 4. K

  Kaburia New Member

  #4
  Mar 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na mchango wa ndugu yetu Nyetk kwa sehemu kubwa lakini kwamba mgomo huu unasimamiwa na madaktari bingwa sio sahihi. Tungesema madaktari bingwa nao wanaukubali mgomo huu kwani nao watapata stahili zao utatuzi wa matatizo wa madaktari kwa ujumla utakapozaa matunda. Madaktari bingwa hawajitokezi moja kwa moja kama nao wako kwenye mgomo. Haya ndiyo mawazo yangu.
   
 5. K

  Kaburia New Member

  #5
  Mar 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo sio miundombinu kwa sasa.wanagoma kwa sababu hawana motisha na wanajisikia vibaya pale wanapo ambiwa kazi za huduma ni wito na sio masilahi wakati sekta nyingine wanapeta. Tuwaonee huruma
   
 6. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  Acheni Propaganda! Hatuwezi kufika kokote kwa kuweka siasa katika kila jambo.. Mgomo wa madaktari haukuanzishwa na wala haujawahi kuongozwa/kusimamiwa na madaktari bingwa! na ni kinyume chake kwani madkatari bingwa siku zote za migomo wamekua wakitoa huduma za dharura mpaka Mponda alipolidanganya bunge na Taifa kwamba hali ni shwari mahospitalini wakati hali ilikua kinyume, hapo ndipo mabingwa wakaona ili serikali iache upuuzi na kuanza kufanya kazi yake nao wasitishe huduma...

  Kabla ya kuweka mada jukwaani ni vizuri ukafanya utafiti kwanza
   
 7. m

  moshingi JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Natafuta kitufe cha "like" nimekikosa...wewe ni Great Thinker kweli, aikambe!!!
  Wale wanaofikiri kwa kutumia mas**ri watakushambulia na kukutukana, cjui wananufaikaje na mgomo wa ma-dr??!!
   
 8. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Nilitaka kumjibu exactly hivyo...unajua watu wanakurupuka tu kubandika mawazo yao hapa JF bila kuyatafiti hata kidogo. Mgomo wa January - February madaktari bingwa waligoma kwa siku 2 tu wakati junior Drs walikuwa kwenye mgomo kwa wiki 2 tayari, na ndio hao madaktari bingwa waliobaki wakifanya kazi waliwapa kiburi Waziri Mponda kudanganya bungeni kuwa huduma zinaendelea kama kawaida, waliwapa kiburi viongozi wa serikali na afisa habari Muhimbili Eliaisha kusema hakuna mgomo....leo ndio wamekuwa wanasimamia 'kidete' mgomo? na sio junior Drs waliojitoa kukaa njaa na kupukutisha mifuko yao kulipia kumbi za mikutano! Angalia picha zote za solidarity wakati wa mikutano zilizo kwenye internet kama kuna daktari bingwa!

  Kitu kingine, ni maDaktari wangapi wamegoma...na wangapi kati yao wanamiliki hospitali binafsi? Kamugisha umemtaja hapo ana hospitali wapi! Kamugisha kutokana na uchapa kazi wake ana wagonjwa wengi ambao anawaona kwa fast track Muhimbili, sijawahi hata kumuona kwenye hospital ya private ya mtu achilia mbali ya kwake! Nyetk acha uongo na umbea...mtoto wa kiume hashikwi umbea bana, unatutia aibu!
   
 9. MANI

  MANI Platinum Member

  #9
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Mkuu unajua wengi wanasahau wajibu wa serekali na ndicho kinawafanya waandike wanavyojisikia.
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaani sasa hivi watasema mgomo huu umesababishwa na CHADEMA
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,455
  Likes Received: 19,826
  Trophy Points: 280
  pinda akijiuzulu mi najinyonga
   
Loading...