Mgomo wa madaktari: Tunavuna tulichopanda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa madaktari: Tunavuna tulichopanda?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lole Gwakisa, Mar 8, 2012.

 1. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Tanzania imo katika kushuhudia mgomo wa madaktari Awamu ya Pili.
  Katika awamu ya kwanza Serikali iliingia kwa gia ya ukali na kuchukua sheria kuwa dhibiti madaktari lakini baadaye kupitia Waziri Mkuu,maelewano yakaafikiwa.
  Awamu ya pili ya mgomo wa madaktari , tena umekuja kwa taarifa rasmi kupitia vyamam vyao, umeshika kasi.
  Safari hiimpango mkakati wa serikali bado haujaelezwa rasmi na serikali.
  Hata hivyo madai ya madaktari safari hii ni kutokuwa na imani na sehemu ya viongozi wa serikali, hususan Mawaziri wanaoiongoza Wizara ya Afya.

  Mtu au mwananchi yeyote aliyeishi nchi hii atajiuliza : TUMEFIKAJE HAPO?
  Je haya mambo yameibuka tu?

  Tatizo ni sera,dira na misimamo isiyoeleweka katika siasa za hivi sasa katika vyama vyote nchini.
  Mimi ni kijana wa siku nyingi kidogo na miaka ya vita ya Kagera Mwalimu aliwasihi waTanzania kuielewa hali halisi ya nchi wakati huo.Akasema tutakuwa na miezi 18 ya shida, shida iliyoendelea kwa karibu miako 10.
  Watanzania tulimuelewa.
  Sera za makuzi ya vijana wetu pamoja na matatizo yanayoonekana katika jamii yamhusika sana kutufikisha hapa tulipo.
  Tujiulize kisiasa, Je haya madudu ya Richmond,EPA,MEREMETA,RADAR na hata wizi mkubwa BOT , kujiuziana nyumba za serikali,tunayachukuliaje?
  Vijana wetu ambao hata JKT hawajapitia wanayachukuliaje haya.
  Tusisahau kwamba vijana madaktari wanogoma leo ni wale wale walikuwa wangoma vyuo vikuu miaka ya karibuni na ambao they will take no-nonsense tofauti na miaka ya nyuma.

  Ni vyema tukarudi nyuma na kujiuliza , tumekosea wapi?
   
 2. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Mkuu usijichoshe kufikiria mambo ya mbele, siasa za Leo ni wewe kushiba Leo Leo.
   
Loading...