Mgomo wa madaktari rasmi kuanzia kesho!!!

Mgomo wa madaktari rasmi kuanzia kesho!!!

OSOKONI

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2011
Posts
10,965
Reaction score
5,344
JUMUIYA ya Madaktari imetangaza rasmi kuanza kwa mgomo usio na kikomo kuanzia kesho, huku ikidai Serikali imekataa kutekeleza madai yao yote yaliyowasilishwa katika kamati ya majadiliano iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.Wakati madaktari hao wakitangaza kurejea rasmi katika mgomo huo uliositishwa miezi mitatu iliyopita, Pinda aliliambia Bunge jana wakati akijibu Maswali ya Papo kwa Papo, kuwa mgomo huo ni batili na haukubaliki.
Saa chache baada ya Pinda kutoa onyo hilo lililorushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni na redio kutoka Dodoma, madaktari hao wakiwa jijini Dares Salaam walitangaza mgomo huo wenye lengo la kushinikiza Serikali kutekeleza madai yao.
Mgomo huo ulitangazwa kwa waandishi wa habari na Dk Stephen Ulimboka, muda mfupi baada ya kukamilika kwa mkutano wa ndani wa madaktari, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Utamaduni la Watu wa Urusi.
Dk Ulimboka alisema mgomo huo usio na kikomo utawahusu madaktari wa kada zote nchini, na unatarajiwa kuanza kesho, baada ya wiki mbili walizotoa kwa Serikali kumalizika bila ya makubaliano yoyote.

“Madaktari kwa ujumla wao wamekubaliana kuwa watarejea katika mgomo usio na kikomo, hii ni kutokana na kugundua kuwa hakuna dhamira ya dhati ya Serikali, kumaliza mgogoro kati yetu na Serikali, uliodumu kwa muda mrefu sasa,” alisema Dk Ulimboka na kuongeza,
“Serikali imetupilia mbali madai yote yaliyofikishwa katika meza ya majadiliano baina ya wawakilishi wa Serikali na madaktari na taarifa iliyotolewa bungeni na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi na pia majibu ya Waziri Mkuu leo, yamepotosha kila kilichomo katika taarifa tuliyonayo sisi.”
Alifafanua kwamba Serikali imetupilia mbali madai yote ambayo kabla ya kukubali kurudi katika meza ya majadiliano yalionekana kuelekea kupata mwafaka.
Dk Ulimboka alisema kuwa kauli iliyotolewa na Pinda bungeni, kwamba walikubaliana, si ya kweli na hata posho zilizotajwa kwenye taarifa za kamati hiyo ni za dharura kabla ya kuanza kwa vikao vya majadiliano.
Alisema msimamo wao ni kuanzisha mgomo usio na kikomo na hakuna njia ya mkato ya kuuzuia, njia pekee ni Serikali kurudi katika meza ya majadiliano.

Kuhusu ushauri uliotolewa na Pinda kuwataka waende mahakamani, Dk Ulimboka alisema jumuiya yao haiko tayari kwenda na kwamba itaendelea na utaratibu wake wa kushinikiza madai hayo kwa njia ya mgomo.
“Sisi hatuendi mahakamani na hakuna njia yoyote ya kuuzima mgomo zaidi ya kurudi kwenye meza ya majadiliano yenye lengo la kufikia mwafaka wa yale tunayotaka kukubaliana," alisisitiza.
Alisema katika madai yao ya msingi waliyotoa serikalini, hadi sasa limetekelezwa moja tu, huku wakishangazwa na Serikali kuongeza posho ya uchunguzi wa maiti kutoka Sh10,000 za awali hadi Sh100,000 kwa madai kuwa posho hiyo haikuwa miongoni mwa madai yao.
“Sisi katika madai yetu hatukuliweka dai hili la posho ya uchunguzi wa maiti, kwa sababu hilo siyo dai letu la msingi. Kazi ya uchunguzi wa maiti siyo ya kila wakati, hufanywa tu pale watu wanapokuwa na mashaka na kifo cha mtu husika, lakini pia haifanywi na madaktari wote,” alisema Dk Ulimboka.

REJEA MWANANCHI
 
Hongera Dk Ulimboka!

Nafuu hata nyie Madktari mmeona UDHAIFU wa serikali yetu!

Jk & Pinda na wabunge wao wote wa chichiem ni JANGA kwa Taifa letu!

Hawakubalikiiiiii!!
 
[FONT=Tahoma, Calibri, Verdana, Geneva, sans-serif]Awaite wazee wa jiji la dar es salaam awaeleze. Huku bunge linawaka moto madaktari nao wanagoma Namshauri Dhaifu asafiri aende Jamaica akabembee na marasta[/FONT]
 
Wache wagome wanastahili kabisa kugoma maana Serikali haiwathamini kabisa kwa sababu hao wa ndani ya Serikali fisadi wanajua wataenda kutibiwa SA, India na hata nchi za magharibi basi hawaoni umuhimu wowote wa kuboresha ujira wa madaktari, manesi na hata hospitali zetu ambazo ziko katika hali ya kusikitisha sana kuanzia majengo, usafi na ukosefu wa vifaa mbali mbali vyenye umuhimu mkubwa mahospitalini.
 
Kama Kweli Raisi wetu si dhaifu, basi atalishughulikia jambo hili maramoja Kwa ukamilifu.
 
Go go go doctors!,,mmeishika serikali dhaifu pabaya,wamezoe kujibu ujinga tu na kutegemea yataisha kama upepo upitao! ,SASA KAZENI KAMBA!
 
duh! serikali iko makini. ni imani yangu suala hili litashughulikiwa ipasavyo once and for all. may be it's about time mkulima atoswe manake hasomeki na ahadi hewa zake
 
kama kweli hospital zetu zinahuduma nzuri raisi atangaze rasmi viongozi wope pamoja na yeye mwenyewe watimiwe amana, temeke, mwananyamala na muhimbili. Kila kitu dhaifu, dhaifu, dhaifu.
 
hivi jeshi la Tz linasubiri nini kuipindua hii serikali goigoi?....... Au na jeshi lenyewe ni goigoi?
 
Rais ni Dhaifu na waziri mkuu wake na wizara ya Afya, wabunge ni Wazembe na CCM ni Wapuuziiiii. Nasimamia msimamo wangu mkitaka ushahidi nitawaletea
 
JUMUIYA ya Madaktari imetangaza rasmi kuanza kwa mgomo usio na kikomo kuanzia kesho, huku ikidai Serikali imekataa kutekeleza madai yao yote yaliyowasilishwa katika kamati ya majadiliano iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.Wakati madaktari hao wakitangaza kurejea rasmi katika mgomo huo uliositishwa miezi mitatu iliyopita, Pinda aliliambia Bunge jana wakati akijibu Maswali ya Papo kwa Papo, kuwa mgomo huo ni batili na haukubaliki.
Saa chache baada ya Pinda kutoa onyo hilo lililorushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni na redio kutoka Dodoma, madaktari hao wakiwa jijini Dares Salaam walitangaza mgomo huo wenye lengo la kushinikiza Serikali kutekeleza madai yao.
Mgomo huo ulitangazwa kwa waandishi wa habari na Dk Stephen Ulimboka, muda mfupi baada ya kukamilika kwa mkutano wa ndani wa madaktari, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Utamaduni la Watu wa Urusi.
Dk Ulimboka alisema mgomo huo usio na kikomo utawahusu madaktari wa kada zote nchini, na unatarajiwa kuanza kesho, baada ya wiki mbili walizotoa kwa Serikali kumalizika bila ya makubaliano yoyote.

"Madaktari kwa ujumla wao wamekubaliana kuwa watarejea katika mgomo usio na kikomo, hii ni kutokana na kugundua kuwa hakuna dhamira ya dhati ya Serikali, kumaliza mgogoro kati yetu na Serikali, uliodumu kwa muda mrefu sasa," alisema Dk Ulimboka na kuongeza,
"Serikali imetupilia mbali madai yote yaliyofikishwa katika meza ya majadiliano baina ya wawakilishi wa Serikali na madaktari na taarifa iliyotolewa bungeni na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi na pia majibu ya Waziri Mkuu leo, yamepotosha kila kilichomo katika taarifa tuliyonayo sisi."
Alifafanua kwamba Serikali imetupilia mbali madai yote ambayo kabla ya kukubali kurudi katika meza ya majadiliano yalionekana kuelekea kupata mwafaka.
Dk Ulimboka alisema kuwa kauli iliyotolewa na Pinda bungeni, kwamba walikubaliana, si ya kweli na hata posho zilizotajwa kwenye taarifa za kamati hiyo ni za dharura kabla ya kuanza kwa vikao vya majadiliano.
Alisema msimamo wao ni kuanzisha mgomo usio na kikomo na hakuna njia ya mkato ya kuuzuia, njia pekee ni Serikali kurudi katika meza ya majadiliano.

Kuhusu ushauri uliotolewa na Pinda kuwataka waende mahakamani, Dk Ulimboka alisema jumuiya yao haiko tayari kwenda na kwamba itaendelea na utaratibu wake wa kushinikiza madai hayo kwa njia ya mgomo.
"Sisi hatuendi mahakamani na hakuna njia yoyote ya kuuzima mgomo zaidi ya kurudi kwenye meza ya majadiliano yenye lengo la kufikia mwafaka wa yale tunayotaka kukubaliana," alisisitiza.
Alisema katika madai yao ya msingi waliyotoa serikalini, hadi sasa limetekelezwa moja tu, huku wakishangazwa na Serikali kuongeza posho ya uchunguzi wa maiti kutoka Sh10,000 za awali hadi Sh100,000 kwa madai kuwa posho hiyo haikuwa miongoni mwa madai yao.
"Sisi katika madai yetu hatukuliweka dai hili la posho ya uchunguzi wa maiti, kwa sababu hilo siyo dai letu la msingi. Kazi ya uchunguzi wa maiti siyo ya kila wakati, hufanywa tu pale watu wanapokuwa na mashaka na kifo cha mtu husika, lakini pia haifanywi na madaktari wote," alisema Dk Ulimboka.

REJEA MWANANCHI

Duh Dr. Stephen Ulimboka tena?
 
Mamaa madaktari tenaa? Hawa jamaa nawapenda wakigoma wanakaa tu home we ndo utawafata!
 
Dawa hapa nikuwanyolosa wananchi walio iweka madarakani serikali dhaifu
 
Ngoma inogile,mpaka tugawane sawa na hawa mafisi-adi hiki kilichobaki kwenye inji hii,nyambaaaaf
 
hivi hatuna watalaam wa mambo ya jamii hapa Tz? mbona mm na kadegree kangu uchwara nimewahi kufundishwa history and impact ya vitu kama hivi ktk jamii...serikali haion kwamba kutokutatua migogoro kwa wakati hupelekea msisimko mpya wa mawazo (evolutionary ideas) ndani ya jamii...mdhalau mwiba....
 
Rais ni Dhaifu na waziri mkuu wake na wizara ya Afya, wabunge ni Wazembe na CCM ni Wapuuziiiii. Nasimamia msimamo wangu mkitaka ushahidi nitawaletea

hahaha kijana futa kauli yako ama la tutamwita bi kiroboto asome kile kifungu chetu.....
 
Wananchi dhaifu wataichagua serikali hii hii dhaifu 2015 !... Watanganyika tumerogwa ????!
 
Back
Top Bottom