Mgomo wa madaktari kuahirishwa leo!

Mimi naomba nukuu ya makubaliano ya kwanza baina ya madaktari na Pinda nione kama kweli Pinda aliwaahidi kuwaachisha kazi Mponda na Nkya.. Pinda anadai hapakuwepo na makubaliano hayo haya ni madai mapya kabisa, sasa isiwe hadithi ile ile ya kwanza walianza na Posho, tuliposema sana wakageuza madai na kuwa mazingira ya kufanyia kazi, Pinda alipotaka kukutana nao wakajataa wakisema hawawezi kwenda Karimjee ila Pinda awafuate wao Starlight, Haya wakutane Jumamosi wakasema ni siku ya Ibada kwao watakutana naye Jumatatu, tukasema mbona huenda kazini Jumamosi na Jumapili wakasema ooh hapana wanasubiri wajumbe wengine kutoka Bara.. haya Leo tena tunazidi kukata masiku ingawa mazungumzo yangeweza kuendelea huku mgomo wao ukiwa palepale - hawataki hadi Mponda na Nkya wajiuzuru... yaani hii sinema ya hostage taking inanoga kweli kweli utampenda kati ya The good, The bad and The Ugly - chaguo lako!

Hii ni miongoni mwa posts zako chache sana ambayo sjailewa mkuu. Hujui kwamba Mizengo kwa sasa ndiye mrithi halali wa Makamba snr, aliyekuwa na uwezo wa kusema jambo flani leo na kesho tu atadai hakusema hvyo. Hata kama makubaliano yale yasingewekwa humu jf au kutangazwa na media mbali*2 bado huitaji Phd kujua nani alisimamia ukweli baina ya PM na Drs. Siye pinda huyu huyu aliyekaribia kulia issue ya Jairo hali ya kuwa ameshasaini yale mambo!
 
JK amekiri kuwa alikuwa kwenye wakati mgumu sana na hawezi kwa sasa kuwaondoa hao mawaziri ataonekana amefanya hivyo kwa shinikizo. Isipokuwa katika kamati ya mazungumzo mawaziri hawa hawatakuwepo, na wakiona kuna mtu yeyote anahisi anakwamisha mazungumzo wamtaarifu mapema. Pia, aliwaomba watangaze jana ile kuwa mgomo umesitishwa lakini viongozi wakasema mpaka tukutane na wanachama. Ndio maana leo hakukutana na wazee, atakutana nao jtatu.

Pongezi zangu kwa JK na madaktari kwa muafaka huu uliopatikana kwa manufaa ya taifa. Hata siku zijazo mkuu endeleza njia hii kwa mambo mengine. Ila usije ukabadilika katika maamuzi yako. Ahsante sana. Mungu ibariki TZ
 
Tumehairisha mgomo ili kumpa Muda Mh Raisi Dr Jakaya Kikwete kushughulikia madai yetu,kiufupi hatuwezi kumlazimisha tukiheshimu mamlaka yake ametuelewa na leo rasmi,tunanyanyua vifaa tunarudi kazini.
Tunaamini anania ya dhati ya kuboresha afya za watanzania,sio kama mr mamba aliyetudanya pale cpl.
Mungu ibariki Tanzania
All the best fellas....moja ya mapungufu makubwa ya watendaji wa jk ni kutoa misinformation kwa boss wao JK(pamoja na mapungufu yake)....mi uwa najiuliza uwa wanafanya hivi kwa maslahi ya nani???....haya makina pinda hakika ni mizigo tu kwa jk.....miwaziri inaboronga alafu inasubiri fadhila za rais ili iwajibike.....mijtu imekaa kimaslahi tu........at least they now know that people are tired of being pushed to limits to do things.......all the best doctors.....
 
Kama Mawaziri Wenyewe ni Kama akina Adam Malima!! Mheshimiwa rais aelewe Hana msaada Mkubwa sana kutoka kwa wasaidizi Wake!! Laptop 2, dola 4,000, Mabegi 2, na vitu Kibao!! Huku katika wizara hakuna cha maana anachokifanya!!!
 
Doctors hongereeni sana sana sana tena sana. Nawapenda na kuwaheshi kwa jinsi mlivyokuwa Strategic. Suala lenu mmeendalo kwa ngazi husika, moja baada ya nyingine, tena kwa ustarabu wa hali ya juu kabisa. Ngazi moja ikishindwa, mnakwenda inayofuata, nayo ikishindwa mnakwenda inayofuata, mpaka mmefika ngazi ya juu kabisa ya maamuzi. Kwa hakika kuna vitu vichache watanzania wote inabidi tujifunze kwa sakata hili;

1. Kumbe watendaji wengi ktk idara na wizara mabalimbali za Serikali hawewezi kuwajibika na kutatua kero na matatizo yanayowakabli wananchi mpaka yafike ngazi ya juu kabisa. Sakata hili la Madaktari linatufundisha,

2. Kumbe tuna watendaji wengi ambao ni wababaishaji na ndio maana mambo mengi hayaendi hapa Tanzania, na kumbe kuna haja ya kufanya overhaul ya watendaji wa serikali kama tukitaka kuendelea kutokana na umangimeza, ulafi, ubinafsi na kutokuwajibika kwa watendaji waliopo,

3. Kufika kwa Mh. Rais na kukubali kumpa muda wa kufanyia kazi masuala yao, ni heshima kubwa waliompa Kiongozi wa Nchi kwamba tegemeo lao kwa sasa ni yeye tu. Lakini pia linatoa tahadhari kwake kuwa, kama naye atashindwa na kuleta siasa kama za wasaidizi wake, basi mambo yataendelea kama kawa.....

Madaktari hongereni sana na tena sana kwa mara nyingine, kama ni ujumbe umefika, na kwa mantiki hiyo, masuala yenu hakuna anayeweza kudeal nayo kuanzia wizara ya Afya, Ofisi ya waziri Mkuu wote wameshindwa na kutakiwa kufanyiwa kazi na IKULU. Ikiwa kama sector nyingi zipo hivyo na kila kitu kiende Ikulu, sasa kuna sababu gani ya kuendelea kuwa na wafujaji wa maliasili za watanzani humo maofisini bila kuwawajibisha.

Mh. Rais, bila shaka amepata ukweli kuhusu watendaji wako na uwezo wao; Kama ilivyokuwa kwa suala la KATIBA pale Bungeni na Mazungumzo yake na Vyama vya Siasa pale IKULU.

Somo hili limetulia sana! Lakini nadhani bila shaka Mkulu naye mtakuwa mmempa dose yake 3x3 kwa wiki mbili au kwa mwezi, nikiwa na maana mmempa time frame.


Very well said..I agree!
 
cha madaktari kinachoendelea Don Bosco sasa hivi kimeazimia kuahirisha mgomo wa Madaktari ili kumpa muda Mh. Presidaa aweze kushughulikia madai yao kama walivyoelewana jana Ikulu.
My Take;
-Nawapongeza sana maDr kwa kuwa na busara hizo ingawaje inawezekana wakawa wamepigwa changa la macho lakini wameonyesha heshima kwa Mh. Raisi kwani kama wasingeweza kuelewana naye ingemaanisha kwamba hata Raisi sasa kazi imemshinda kama ilivyowashinda Juniors wake..BIG UP GENIOUS DRS......
-Ieleweke kwamba UMEAHIRISHWA, Sio kwamba UMEISHA



TAARIFA RASMI YA MAT
RIPOTI KWA VYOMBO VYA HABARI.

UTANGULIZI
Baada ya kikao cha madaktari kilichofanyika leo tarehe 10/3/2012. Madaktari nchini kupitia chama cha madaktari Tanzania (MAT), tunapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:

1. Jamii ielewe kuwa daktari kama binadamu mwingine anayefanya kazi Tanzania ana mahitaji muhimu (basic needs) na mahitaji ya kijamii (social responsibility) na hivyo si chombo cha kufanyia kazi (Machine).

2. Pia Daktari ana haki ya kupata ujira unaomfaa kutokana na kazi anayofanya na ana haki ya kuacha kazi muda wowote iwapo ataona kazi hiyo ya udaktari haimpi ujira wa kutosha na heshima ya kuendesha maisha yake.

3. Pia jamii itambue kuwa daktari anaweza kulazimishwa kurudi kazini lakini hawezi kulazimishwa kufanya kazi. Matokeo ya kulazimishwa yanaweza yasiwe mazuri kwa wale watakao hudumiwa.

4. Jamii itambue kuwa madai na hoja kuu za madaktari ni kwa ajili ya faida ya Watanzania wote,yakiwemo mazingira bora ya kufanya kazi mjini na vijijini, na kuboresha afya za watanzania kwa ujumla. Pia vifaa na dawa ziwepo mahospitalini zinakohitajika.

5. Pia tunawashukuru madaktari wote kwa mshikamano wetu tulioonyesha na tunaomba mshikamano huu uendelee daima.

TAMKO LETU:

JANA TAREHE 9/3/2012, TULIKUTANA NA MH. RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE. TULIMWELEZA HOJA ZETU, AMBAZO ALIZIELEWA NA ALIAHIDI KUZISHUGHULIKIA KIKAMILIFU. TUNA IMANI SANA NA MH. RAIS KWAMBA HATATUANGUSHA.

KUTOKANA NA HILO, TUNAPENDA KUUTANGAZIA UMMA WA WATANZANIA KUWA TUNARUDI KAZINI RASMI KUANZIA LEO TAREHE 10/3/2012, WAKATI MHESHIMIWA RAIS AKISHUGHULIKIA MADAI YETU.

PIA WAKATI MADAI YETU YAKISHUGHUKLIKIWA TUNAPENDA KUSEMA KUWA HATUNA IMANI NA WAZIRI WA AFYA MH. DR. HAJI MPONDA NA MH. DR. LUCY NKYA, NA KUWA TUNAMSIMAMISHA RASMI UANACHAMA WA MAT MH. DR. LUCY NKYA.

MADAKTARI TUNATAMKA WAZI KUWA WAZIRI WA AFYA DR. HAJI MPONDA NA NAIBU WAKE DR. LUCY NKYA NI MAADUI WA MADAKTARI NA SEKTA YA AFYA KWA UJUMLA HAPA NCHINI NA TUNAAHIDI KUTOKUWAPA USHIRIKIANAO WA AINA YOYOTE WA KIBINAFSI AU WA KIUTENDAJI.

SOLIDARITY FOREVER.
RAIS(MAT)
God Bless you doctors......Una firmus et fidens!!
 
Hii ni miongoni mwa posts zako chache sana ambayo sjailewa mkuu. Hujui kwamba Mizengo kwa sasa ndiye mrithi halali wa Makamba snr, aliyekuwa na uwezo wa kusema jambo flani leo na kesho tu atadai hakusema hvyo. Huitaji Phd kujua nani alisimamia ukweli baina ya PM na Drs. Siye pinda huyu huyu aliyekaribia kulia issue ya Jairo hali ya kuwa ameshasaini yale mambo!
Kama unavyosema ni kweli, basi kwa nini hawa madaktari wasiombe Pinda ajiuzuru maana kaonyesha walichodai madaktari ni uongo na madai ni mapya hayakuwepo ktk makubaliano ya kwanza..
Wao kama kweli walikubaliana naye hivyo watuonyeshe makubaliano hayo na waombe Pinda ajiuzuru maana hii ni chini ya ukanda kabisa. Nukuu za maneno ya Pinda kukataa kwamba hawakuwa na makubaliano ya kujiuzuru kwa Mponda na Nkya TUNAYO hivyo hawezi kupinga.. Ila hatuna kutoka kwa madaktari kuthibitisha kweli Pinda aliwaahidi hivyo, tupeni hiyo nakala yenu tatizo liko wapi?
 
Kama unavyosema ni kweli, basi kwa nini hawa madaktari wasiombe Pinda ajiuzuru maana kaonyesha walichodai madaktari ni uongo na madai ni mapya hayakuwepo ktk makubaliano ya kwanza..
Wao kama kweli walikubaliana naye hivyo watuonyeshe makubaliano hayo na waombe Pinda ajiuzuru maana hii ni chini ya ukanda kabisa. Nukuu za maneno ya Pinda kukataa kwamba hawakuwa na makubaliano ya kujiuzuru kwa Mponda na Nkya TUNAYO hivyo hawezi kupinga.. Ila hatuna kutoka kwa madaktari kuthibitisha kweli Pinda aliwaahidi hivyo, tupeni hiyo nakala yenu tatizo liko wapi?

Haaahaaaa! Some of us great thinkers, tunafikiria mpaka kupitiliza kama 'Hem" as a character kwenye kitabu cha "who moved my cheese?",lol
 
madaktari hongereni sana,mmeonyesha utu,uzalendo,kujali,na kuwajibika,sasa zamu ya ikulu tunangoja utekelezaji.
 
Kama unavyosema ni kweli, basi kwa nini hawa madaktari wasiombe Pinda ajiuzuru maana kaonyesha walichodai madaktari ni uongo na madai ni mapya hayakuwepo ktk makubaliano ya kwanza..
Wao kama kweli walikubaliana naye hivyo watuonyeshe makubaliano hayo na waombe Pinda ajiuzuru maana hii ni chini ya ukanda kabisa. Nukuu za maneno ya Pinda kukataa kwamba hawakuwa na makubaliano ya kujiuzuru kwa Mponda na Nkya TUNAYO hivyo hawezi kupinga.. Ila hatuna kutoka kwa madaktari kuthibitisha kweli Pinda aliwaahidi hivyo, tupeni hiyo nakala yenu tatizo liko wapi?
Mzee wa ligi ya mabishano...Pinda aliwasimamisha katibu mkuu na mganga mkuu. Kuhusu waziri na naibu waziri alisema hilo liko juu ya mamlaka yake kwa hiyo atalifikisha kwa rais. Suala la kuwajibishwa kwa waziri na naibu wake lilikuwepo tangia awali tofauti na alivyosema Pinda lately kwamba ni madai mapya...Issue hapa ni je , kweli Pinda aliyafikisha hayo madai kwa rais ndani ya time frame waliyopewa? Ni nini kilichomfanya pinda abadilishe maneno yake mwenyewe aliyoyasema mbele ya vyombo vya habari alipokutana na madaktari na kusema upya hayo ni madai mapya na kwamba Mponda na Nkya wanaonewa tu kwa sababu hayo matatizo wameyakuta kwenye wizara...alishindwa nini kuwaambia madaktari hayo maneno wakati walipokutana naye awalli?
Maswali ni mengi lakini hiyo ndiyo nchi yetu ....rais bogus...waziri mkuu bogus na mawaziri karibu wote...!
 
Solidarity forever. Inaonekana Mponda na Nkiya waliwashika pabaya. Hii ndiyo taabu ya kuongozwa na watu wa kada moja.
 
Baada ya kupata taarifa kuwa drs wanakikao na JK nilijuala zima mwafaka utafikiwa.
na nina uhakika utakuwa ule ambao unatekelezeka hata CDM walipoenda kuonana na JK baadaye tuliona utekelezaji wake, ninauhakika katika hili pia raisi atavunja balaza la mawaziri na kuunda lingine ambalo litawa exclude mponda, nkya, sita, mwakyembe, na mwandosya.
pia hiyo taarifa kwa vyombo vya habarii metulia safi sana
 
cha
madaktari kinachoendelea Don Bosco sasa hivi kimeazimia kuahirisha
mgomo wa Madaktari ili kumpa muda Mh. Presidaa aweze kushughulikia
madai yao kama walivyoelewana jana Ikulu.
My Take;
-Nawapongeza sana maDr kwa kuwa na busara hizo ingawaje inawezekana
wakawa wamepigwa changa la macho lakini wameonyesha heshima kwa Mh.
Raisi kwani kama wasingeweza kuelewana naye ingemaanisha kwamba hata
Raisi sasa kazi imemshinda kama ilivyowashinda Juniors wake..BIG UP
GENIOUS DRS......
-Ieleweke kwamba UMEAHIRISHWA, Sio kwamba UMEISHA
TAARIFA RASMI YA MAT
[h=6]RIPOTI KWA VYOMBO VYA HABARI. UTANGULIZI Baada ya kikao cha
madaktari kilichofanyika leo tarehe 10/3/2012. Madaktari nchini kupitia
chama cha madaktari Tanzania (MAT), tunapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:
1. Jamii ielewe kuwa daktari kama binadamu mwingine anayefanya kazi
Tanzania ana mahitaji muhimu (basic needs) na mahitaji ya kijamii
(social responsibility) na hivyo si chombo cha kufanyia kazi (Machine).
2. Pia Daktari ana haki ya kupata ujira unaomfaa kutokana na kazi
anayofanya na ana haki ya kuacha kazi muda wowote iwapo ataona kazi
hiyo ya udaktari haimpi ujira wa kutosha na heshima ya kuendesha maisha
yake. 3. Pia jamii itambue kuwa daktari anaweza kulazimishwa kurudi
kazini lakini hawezi kulazimishwa kufanya kazi. Matokeo ya kulazimishwa
yanaweza yasiwe mazuri kwa wale watakao hudumiwa. 4. Jamii itambue kuwa
madai na hoja kuu za madaktari ni kwa ajili ya faida ya Watanzania
wote,yakiwemo mazingira bora ya kufanya kazi mjini na vijijini, na
kuboresha afya za watanzania kwa ujumla. Pia vifaa na dawa ziwepo
mahospitalini zinakohitajika. 5. Pia tunawashukuru madaktari wote kwa
mshikamano wetu tulioonyesha na tunaomba mshikamano huu uendelee daima.
TAMKO LETU: JANA TAREHE 9/3/2012, TULIKUTANA NA MH. RAIS WA JAMUHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA MH. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE. TULIMWELEZA HOJA
ZETU, AMBAZO ALIZIELEWA NA ALIAHIDI KUZISHUGHULIKIA KIKAMILIFU. TUNA
IMANI SANA NA MH. RAIS KWAMBA HATATUANGUSHA. KUTOKANA NA HILO,
TUNAPENDA KUUTANGAZIA UMMA WA WATANZANIA KUWA TUNARUDI KAZINI RASMI
KUANZIA LEO TAREHE 10/3/2012, WAKATI MHESHIMIWA RAIS AKISHUGHULIKIA
MADAI YETU. PIA WAKATI MADAI YETU YAKISHUGHUKLIKIWA TUNAPENDA KUSEMA
KUWA HATUNA IMANI NA WAZIRI WA AFYA MH. DR. HAJI MPONDA NA MH. DR. LUCY
NKYA, NA KUWA TUNAMSIMAMISHA RASMI UANACHAMA WA MAT MH. DR. LUCY NKYA.
MADAKTARI TUNATAMKA WAZI KUWA WAZIRI WA AFYA DR. HAJI MPONDA NA NAIBU
WAKE DR. LUCY NKYA NI MAADUI WA MADAKTARI NA SEKTA YA AFYA KWA UJUMLA
HAPA NCHINI NA TUNAAHIDI KUTOKUWAPA USHIRIKIANAO WA AINA YOYOTE WA
KIBINAFSI AU WA KIUTENDAJI. SOLIDARITY FOREVER. RAIS(MAT)[/h]

Busara imetawala. Mungu ashukuriwe. Mbarikiwe madaktari.
 
Back
Top Bottom