Mgomo wa daladala jijini Mwanza

Mgomo wa daladala jijini Mwanza

Joined
Jan 18, 2014
Posts
11
Reaction score
0
Madereva wa daladala wagoma kuingia barabarani na kusababisha wananchi kuchelewa makazini kwao vivyo hivyo na kwa wanafunzi pia chanzo bado sijakipata ila kwa tetesi ni kwamba hawaitaki stand ya daladala ya nyakato-buzuruga kwa madai imefinya sana kwa hiyo wanashndwa kupishana hadi aanze kitoka wambele.

Hii imetokea leo tarehe 17/02/2014,Hapa JIJINI MWANZA.

NINI MAONI YAKO KUHUSU MGOMO HUU,KWA WAMILIKI WA DALADALA NA SERIKALI?
 
Nawaunga mkono kwani siku moja nilipita pale buzuruga kweli nchii haina wasomi kabisa!! wameweka kistand utafikiri ni cha kuegesha tax 2? Yaani huyu engineer wa jiji inabidi awajibike! TOO PATHETIC!
 
Pale Buzuruga hapapaswi kuwa stendi, bali kushusha au kupakia abiria tu.
 
Pale Buzuruga hapapaswi kuwa stendi, bali kushusha au kupakia abiria tu.

Ndio lakini kisehemu walichotenga na idadi ya magari ni uwendawazimu mtupu! au ndo njia ya kuwakamata kuwa wamevunja sheria ili wapate ongo?
 
panda bodaboda, leo mgomo ndugu, tunataka stendi ya nyakato iondolewe au kuboleswa,
 
Tanzania nchi yangu,mbona wananchi wako wananyanyasika? Wafanyabiashara wanagomea EFDs...,wenye daradara wanagomea stendi....
 
wadau wa usafiri wa daladala jijini mwanza wameanzisha mgomo asubuh hii kutaka naul ipande kutoka sh 400 kituo adi kituo mpaka mia tano(500),,
hivi hii nchi inakwenda wap kila mtu akiamka asubuh anatangaza mgomo
source:mimi nipo mwanza
 
Kuna siku mgomo ulitokea magari ya mizigo hapa kijiwe cha pasiansi yakikula vichwa balaa ebu fikiria plan b mkuu, na vile mwanza kuna bajaji-roli tupu duh!!
 
napendekeza wafanya 1000

hawajagoma ili nauli ipande wamegoma kwasababu kwanza stand ya kushusha na kupakia buzuruga ni finyu sana halafu askari wa usalama barabarani wanalazimisha rushwa manake wanashindana kununua magari kwahiyo hata alieanza kazi miezi sita anataka na yeye anunue GX100 hata mie nawaunga mkono hawa trafic wamezidi juzi nimesafiri kiutoka tinde hadi mwanza mpaka nilimuonea huruma dereva mpaka inafikia sehem dereva anachukia kazi kwasababu ya trafic nakumbuka tulifika nkungumarwa trafic akaomba kadi ya gari dereva akatoa ili ampe yule trafic akamwambia tena naomba kadi ya gari jamaa akimpa anamwambia nipe kadi mwisho yule dreva akakasilika wakaanza kuzozana baadae tukaondoka nimuuliza kwanini ulikua unampa kadi bado anendelea kukusumbua akasema wamezoea ukimpa kadi unaweka pesa kwenye ile kadi sasa yeye akampa bila pesa ndio mzozo ukaanza kwahiyo kwa ujumla trafic wanasumbua sana
 
Pale Buzuruga hapapaswi kuwa stendi, bali kushusha au kupakia abiria tu.
Inawezekana kazi iliyofanywa ilikuwa sub-standard, lakini kwa uelewa wangu kile ni kituo cha kushishusha na kipakia tu, sio parking, kwa maana hiyo sioni kwa nini wakigomee. Wao wanataka kupiga debe na kutuibia tu hawana lolote hao. Upande mwingine hawa jamaa wa jiji wajaribu kuwa wanachukua maoni ya wadau kabla ya project za vile, isije kusababisha hasara ya kuweka project ambazo hazitawanufaisha walipa kodi. Hata ukiingia buzuruga stendi kuu ya basi ni muundo huo huo, gari la mbele linatangulia..
 
Kwahiyo faini ya 60,000/= iko kituo cha buzuruga tu kwingine hakuna mbona vituo vingine hawachaji hicho kiwango halafu hicho kituo ni finyu kiasi kwamba zikifika gari kuanzia kumi kwa wakati mmoja inakua msongamano kama bwana mmoja alivyochangia humu kuna mambo mengine kabla ya kufanyika inabidi kushauriana na wadau lakini bado nasisitiza askari wa usalama barabarani wapo kibiashara zaidi hawatekelezi majukum yao ila sio wote kuna wengine huwa wanaelimisha ukiwa umekosea lakini kuna wengine anadiriki kijificha ili akukamate umpe rushwa mbona askari wanaolinda bank huwa wanakuepo eneo la kazi na unakuta amesimama imara na bunduki yake mpaka mda wake unapoisha kwanini huwa hawajifichi kama baadhi ya trafic wanavyofanya
 
Madereva wa daladala wagoma kuingia barabarani na kusababisha wananchi kuchelewa makazini kwao vivyo hivyo na kwa wanafunzi pia chanzo bado sijakipata ila kwa tetesi ni kwamba hawaitaki stand ya daladala ya nyakato-buzuruga kwa madai imefinya sana kwa hiyo wanashndwa kupishana hadi aanze kitoka wambele.

Hii imetokea leo tarehe 17/02/2014,Hapa JIJINI MWANZA.

NINI MAONI YAKO KUHUSU MGOMO HUU,KWA WAMILIKI WA DALADALA NA SERIKALI?

...serikali yetu sikivu, ya ccm, tuliichagua wenyewe!

"pipozzz paaawa"
 
Wana jamvi kuamkia alfajiri ya leo jijini mwanza hakuna usafiri wa daladala kutokana na mgomo wa kushinikiza kuondolewa matrafic wasumbufu jijini hapo.sasa hivi magari yanayo toa huduma ni yale yaliokuwa yanaenda nje ya mkoa kwa sh 1500/=town trip
 
Hapa Mwanza kitengo cha Usalama barabarani kuna 'ka-sheria' kao ambako sio officially: kila trafiki kwa siku lazima ukamate gari 3 ambazo ni za boss, yaani hizo lazima zifike sentro ili wenye hizo gari wamalizane na bosi! Kumbuka afande aliyepo barabarani naye anahitaji zake! Source: nyumba ndogo yangu ni trafiki!
 
Tz bila migomo mambo hayaendi kabisa! Kesho utasikia bodaboda nao wamegoma wakisha goma wote watawala lazima watajuwa nn maaana ya kuongoza watu!!
 
Hapa Mwanza kitengo cha Usalama barabarani kuna 'ka-sheria' kao ambako sio officially: kila trafiki kwa siku lazima ukamate gari 3 ambazo ni za boss, yaani hizo lazima zifike sentro ili wenye hizo gari wamalizane na bosi! Kumbuka afande aliyepo barabarani naye anahitaji zake! Source: nyumba ndogo yangu ni trafiki!
Hii ndio maana halisi ya maneno kuwa nchi haitatawalika. Mafisa wa serikali wavamzisha usumbufu wa kiaina ili wajinufaishe huku utawala wa ccm unaangalia tuu bila kuchukua hatua. Angalia sasa migomo ya madereva na ma Rc wanaongea hawasikilizwi. Wfanyabiashara wanagomea machine za kodi Waziri na serikali wanatoa matamko hawasikilizwi,bado tutasema nchi inatawalika? Hapana haitawaliki na raia ndio wanapata shida zote hizo.
kiujumla lazima tukubali kuwa CCM imeshindwa kuongoza nchi na sasa tuko kwenye Autopilot na kudra za mwenyezi MUNGU tuu. Kwa vile hatuna utamaduni wa anayeshindwa kazi kujiengua basi CCM haiwezi kujiengua bali tuitoe madarakani ikae pembeni na kujifunza kutoka kwa wengine.
 
Hao ni wanafiki tu. mbona alfajiri na jioni majira ya saa 1 wengine walifanya kazi?. Polisi fanyeni kz yenu. Msiyumbishwe kama wanasiasa. Na kesho endelezeni mgomo hakuna atakae waombeni. Ila nailaumu polisi kuwaachia hz gari zenu zitembe asbh bila abiria na huku zikpia kwenye vituo na kuzihaki abiria. Msije mkashangaa zikianza kuchomwa moto chezea raia mwenye hasira akichoka utajuta
 
Back
Top Bottom