Taarifa kutoka duru za walimu na madaktari zinadai kwamba watumishi hawa wa umma wapo mbioni kugoma ili kuishnikiza serikali ya CCM kuwalipa madai yao kama ilivyowaahidi miaka kadhaa iliyopita kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu:
MADAKTARI
Madaktari wanaidai serikali madai mbalimbali ikiwemo kuboresha maslahi yao na mazingira ya kufanyia kazi, kuwalipa oncall allowance na posho ya kufanyia kazi katika mazingira hatarishi, kuboresha huduma za hospitali (dawa, vitanda, vitendea kazi, nk), kuthamini taaluma ya udaktari, nk. Utaona kwamba madai yao yamejikita katika sehemu kuu mbili ambazo ni uboreshwaji wa mazingira ya kazi na vifaa vya tiba na uboreshwaji wa kipato, kinga na afya za madaktari (Mishahara, posho na Bima ya afya).
WALIMU
Walimu wanaidai serikali mabilioni ya shilingi ikiwemo posho, malimbikizo ya mishahara, kupandishwa vyeo, nk. Walimu ndio watumishi wa umma wanaolipwa fedha kidogo zaidi kuliko watumishi wote wa serikali; na pia kazi yao haithaminiwi hata kidogo na serikali ya CCM. Kumbuka siku za nyuma Waziri wa CCM, Bi Hawa Ghasia aliwahi kuwadhihaki kwamba kama hawataki kulipwa mishahara kidogo basi watafute kazi nyingine tofauti na ualimu kwa kuwa siku zote kada ya ualimu wataendelea kulipwa mishahara kidogo so long as ni wengi sana ukilinganisha na watumishi wengine wa serikali. Hivyo, kama serikali ikiwalipa vizuri, itafilisika!
WAFANYAKAZI WENGINE
Nao wafanyakazi wa kada zingine wanaoidai serikali mabilioni ya shilingi wanasubiri walimu na madaktari walibumbulie, nao waunge tela. Safari hii sioni namna ambavyo serikali itakavyoweza kuuzuia mgomo huu mtakatifu. Ni rahisi kuzuia mafuriko kwa mikono kuliko kuuzuia mgomo huu. Sisi yetu macho
wafanyakazi wa serikali wakilianzisha nasi wananchi tuunge tela. Bila kufanya hivyo, serikali hii ya CCM itaendelea kuchezea maisha ya watanzania mpaka kiyama. Tazama jinsi hospitali na shule za makabwela zilivyo taabani huku kila kukicha tunasikia mafisadi wa CCM wakikwapua mabilioni ya shilingi bila kuchukuliwa hatua zozote.
View attachment 254823View attachment 254824View attachment 254825View attachment 254826View attachment 254827
MAONI YANGU
Mimi naona kama mgomo huu umechelewa sana. Ulipaswa ufanyike mapema na maslahi yanelikwishaboreshwa kitambo sana. Wafanyakazi wan chi hii ndio itakuwa chachu ya mabadiliko. Sisi raia wa kawaida tunapaswa kuwaunga mkono wafanyakazi kwani kuboreshwa kwa maslahi yao kuna manufaa makubwa sana kwa wananchi wa kawaida. Aidha, madai yao yanajumuisha uboreshaji wa huduma za tiba kwa wananchi; na hapa kila mwananchi atanufaika kwani ubovu wa huduma katika hospitali na shule zetu unamuathiri kila raia mnyonge isipokuwa wale mafisadi wachache wasiotibiwa katika hospitali za umma na wasiosoma katika shule za walalahoi (shule za kata).
:israel: