Mgomo mkubwa wanukia nchini

Mgomo mkubwa wanukia nchini

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,950
Reaction score
25,327
Taarifa kutoka duru za walimu na madaktari zinadai kwamba watumishi hawa wa umma wapo mbioni kugoma ili kuishnikiza serikali ya CCM kuwalipa madai yao kama ilivyowaahidi miaka kadhaa iliyopita kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu:

MADAKTARI
Madaktari wanaidai serikali madai mbalimbali ikiwemo kuboresha maslahi yao na mazingira ya kufanyia kazi, kuwalipa oncall allowance na posho ya kufanyia kazi katika mazingira hatarishi, kuboresha huduma za hospitali (dawa, vitanda, vitendea kazi, nk), kuthamini taaluma ya udaktari, nk. Utaona kwamba madai yao yamejikita katika sehemu kuu mbili ambazo ni uboreshwaji wa mazingira ya kazi na vifaa vya tiba na uboreshwaji wa kipato, kinga na afya za madaktari (Mishahara, posho na Bima ya afya).

WALIMU
Walimu wanaidai serikali mabilioni ya shilingi ikiwemo posho, malimbikizo ya mishahara, kupandishwa vyeo, nk. Walimu ndio watumishi wa umma wanaolipwa fedha kidogo zaidi kuliko watumishi wote wa serikali; na pia kazi yao haithaminiwi hata kidogo na serikali ya CCM. Kumbuka siku za nyuma Waziri wa CCM, Bi Hawa Ghasia aliwahi kuwadhihaki kwamba kama hawataki kulipwa mishahara kidogo basi watafute kazi nyingine tofauti na ualimu kwa kuwa siku zote kada ya ualimu wataendelea kulipwa mishahara kidogo so long as ni wengi sana ukilinganisha na watumishi wengine wa serikali. Hivyo, kama serikali ikiwalipa vizuri, itafilisika!


WAFANYAKAZI WENGINE
Nao wafanyakazi wa kada zingine wanaoidai serikali mabilioni ya shilingi wanasubiri walimu na madaktari walibumbulie, nao waunge tela. Safari hii sioni namna ambavyo serikali itakavyoweza kuuzuia mgomo huu mtakatifu. Ni rahisi kuzuia mafuriko kwa mikono kuliko kuuzuia mgomo huu. Sisi yetu macho…wafanyakazi wa serikali wakilianzisha nasi wananchi tuunge tela. Bila kufanya hivyo, serikali hii ya CCM itaendelea kuchezea maisha ya watanzania mpaka kiyama. Tazama jinsi hospitali na shule za makabwela zilivyo taabani huku kila kukicha tunasikia mafisadi wa CCM wakikwapua mabilioni ya shilingi bila kuchukuliwa hatua zozote.


huduma bora.jpg huduma safi.jpg View attachment 254825 ambulance ya CCM.jpg wanafunzi chini ya mbuyu.jpg

MAONI YANGU
Mimi naona kama mgomo huu umechelewa sana. Ulipaswa ufanyike mapema na maslahi yanelikwishaboreshwa kitambo sana. Wafanyakazi wan chi hii ndio itakuwa chachu ya mabadiliko. Sisi raia wa kawaida tunapaswa kuwaunga mkono wafanyakazi kwani kuboreshwa kwa maslahi yao kuna manufaa makubwa sana kwa wananchi wa kawaida. Aidha, madai yao yanajumuisha uboreshaji wa huduma za tiba kwa wananchi; na hapa kila mwananchi atanufaika kwani ubovu wa huduma katika hospitali na shule zetu unamuathiri kila raia mnyonge isipokuwa wale mafisadi wachache wasiotibiwa katika hospitali za umma na wasiosoma katika shule za walalahoi (shule za kata).

:israel:
 
mbona habaari za kiindelijenzia hazija tufikia sisi watawala?
 
Pamoja na hii migomo ambayo inaletaga tija flani,
mwaka huu unapaswa kuhitimishwa na Mgomo wa kuipigia kura ccm kwenye ngazi zote.
Kwa huu mgomo wa Octoba,tayari mimi nimegoma na hakuna wa kunibadilisha,hata mahakama.Sitoipigia kura ccm hata wamsimamishe Malaika.
Kwa huu mgomo wa wafanyakazi,nimetega sikio tayari!
 
Waandamane waende kwa fisadi EL atawalipa zote akiwapigia simu rafiki zake wamfanyie rambi rambi
 
Watawala wako slow by nature. I.e.BoT, MoF. Wako reactive instead of proactive.
 
safari hii sioni CCM watakapoponea. huu mgomo utakuwa mkubwa na wenye athari mbaya kuliko mgomo wa madereva.
 
Last edited by a moderator:
Nijuavyo mimi waalimu na madaktari walishagoma zamani ila migomo
yao ipo mioyoni,kwa macho haya wanaonekana wapo kazini ila mioyoni wamegoma.

selikari inalijua hilo ndo maana ikaanzisha division five almaarufu kama BRN
kuna mtoto anapata division 4 ya point 48,na wazazi tunashangilia kama mazuzu.
kwamba watoto wetu wamefaulu.

Upande wa madaktari toka kuteswa kwa Dr Ulimboka
anayeenda hospitali za umma atanielewa ninachokisema hapo.
Hali ni mbaya kama huna mtu unayefahamiana naye,ua labda upate bahati
wakshtukie kuwa labda wewe ni mtu fulani miongoni mwa wenye mamlaka hapo utahudumiwa.

Binafsi naona walishagoma labda kama wameamua kuweka hadharani japonajua watashindwa
kama walivyoshindwa hapo kwanza walipojaribu.Raia ndo tujiandae kuumia zaidi
na matokeo ya hiyo migomo.Asante bima ya afya ya serikali angalau sasa wengi
wana pa kukimbilia.

Kwa andiko hili siwezi kuwalaumu,maana nao walisoma ili wahudumie familia zao
pale wanapokuta elimu zao haziwasaidii kutunza familia zao
wanatumia njia mbadala,ili kutufikishia ujumbe sisi raia tujifunze kufanya
maamuzi sahihi pindi tupatapo nafasi ya kuchagua viongozi wa kuliongoza taifa.
 
Kama katibu mkuu wa CWT bado ni yule yule Oluochi niliyemuona wakati wa bunge la katiba, naweza ku bet kuwa mgomo utashindwa kabla ya kuanza.
 
Ila mkuu kinachonifurahisha,karibu madaktari wote wana magari ya kutembelea.
Pia ukipita kwenye mashule hata yale ya msingi hapa Dar unakuta magari ya waalimu yamepark.
Nadhani hili linaipa serikali imani kwamba wanalipwa vizuri
au wanautumia muda wao wa kuwa kazini vizuri kupata kipato kingine

Ndo maana idara zote za ukaguzi hazifanyi kazi,shule hata zile za katikati ya jiji,Ukiuliza wanasema hawana usafiri.
Matokeo ya mitihani kwa wanafunzi ni mgogoro,anayefaulu ni jitihada binafsi za kwake
na wazazi,Tuition centres kama mchikichini,pale external na mwenge ndo zinasaidia wanafunzi kufaulu.
 
Hizo ni habari za udaku

hizo kauli zenu za kejeli ilhali maisha ya watanzania yanateketea tulishazizoea. hata dr kafulila alipoanzisha hoja ya ESCROW mlimbeza na kumuita TUMBILI lakini mwisho wake watanzania wanamfahamu tumbili ni nani. endelea kukenua tu lakini kiama chenu chaja.
 
Back
Top Bottom