VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Taarifa za kiintelijensia nilizonazo ni kwamba madereva wa mabasi na malori wanatazamiwa kugoma nchi nzima kuanzia Ijumaa. Madereva hao wana malalamiko lukuki yakiwemo mikataba ya ajira,ubovu wa miundombinu,sheria kali za barabarani na nyinginezo.
Taarifa nilizonazo ni kuwa Madereva wa mabasi na malori nchi nzima watamaliza kufanya kazi zao Alhamisi. Watasubiri Ijumaa kujua hatma ya malalamiko yao. Ijumaa,madereva wote wa mikoa ya Dar na Pwani watakutana na ujumbe wa Serikali na wengineo Ubungo
Madereva wamewataka Mawaziri wanne:Sitta-Uchukuzi,Magufuli-Ujenzi na Kabaka-Ajira na Chikawe-Mambo ya Ndani wafike Ubungo saa moja asubuhi,siku ya Ijumaa tar 10 mwezi wa 4 kutoa majibu ya malalamiko ya madereva hao. Pamoja nao,wanatakiwa viongozi wa Polisi,TABOA,TAKUBOA na TBS.
Majibu yao yatazuia au kuchochea mgomo wa madereva wa mabasi na malori nchi nzima.
Mimi tu,kuwaletea habari!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam