Mgomo Kariakoo, maduka yafungwa

Juzi walikuja maafisa TRA kukagua wanaotoa na wasiotoa risiti za mashine,wakawakamata wafanyabiashara kama 30 hivi wakaondoka nao,waliokamatwa walidai walikuwa wanasubiri wapewe mashine bure kama alivyosema rais,inaonekana wenzao wanawapa company kwa kugoma leo so kama kuna yeyote anaetaka kuja kufanya manunuzi yoyote asubiri subiri angalao mpaka saa6....Nawasilisha.
 
Ngoja tusikie nini kinaendelea maanake mgomo wa kwanza ulikuwa EFD bei ghali, sasa hivi si wanapewa bure? Tusikie tatizo nini. EFD zinawa-expose hamna anaeipenda hata mmoja!
 
Hawa wanafikiria kuwa awamu hii ni ya Mkwere, wamekosea ,nyakati hizi sio za kukwepa kodi. Yatafungwa maduka yote na ikibidi watafilisiwa. Wanaona shida gani kutumia hizo mashine ambazo wanapewa bure? hahaha,ngoja watakosa hizo biashara soon.
 
tusubiri busara za makonda,
bwana mdogo kaagizwa pia afyagie wapiga debe jijini.
hapa kadhi..
tutakula ngeta mchana jua la utosini.
 
Nasikia kwa sababu ya urasimu bandarini, utokaji wa makontena umekuwa haueleweki bandarini.

Kuna baadhi ya wafanyabiashara toka mwezi wa kumi na mbili hawajatoa makontena yao. Hivyo sokoni hakuna mizigo mipya

Pili hakuna bei rasmi ya kulipia mizigo yaani wanaropoka tu bila kujali umebeba mzigo gani.

Yaani TRA ni kama wanawakomoa wafanyabiashara.
 
Hawa wanafikiria kuwa awamu hii ni ya Mkwere, wamekosea ,nyakati hizi sio za kukwepa kodi. Yatafungwa maduka yote na ikibidi watafilisiwa. Wanaona shida gani kutumia hizo mashine ambazo wanapewa bure? hahaha,ngoja watakosa hizo biashara soon.
Kwahiyo we umesahau. Ni walipa kodi mkuu wanatakiwa waheshimiwe.
 
tusubiri busara za makonda,
bwana mdogo kaagizwa pia afyagie wapiga debe jijini.
hapa kadhi..
tutakula ngeta mchana jua la utosini.
Busara za Makonda ni kuweka watu ndani kwa saa 48.
 
Back
Top Bottom