Mgomo haukuficha Ghost Doctors | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo haukuficha Ghost Doctors

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Timtim, Feb 2, 2012.

 1. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Natafakari huu mgomo wa madaktari ulioanza kumi la mwisho wa mwezi uliopita (January) ki ukweli hauna mahusiano na Ghost Workers?
  Vile mazungumzo yalivyoanza kwa interns kisha MAT kupenduliwa na sijui Jopo la Madaktari yote hayo hayajanikalia vizuri kichwani mwangu. Sijui nimuulize nani swali linalo nisumbua 'Jee Madaktari walikuwa wameshahakikiwa' hamna madaktari hewa? Ama huu ulikuwa ujanja wa Wajanja ili kuvuruga juhudi za serikali kuhakiki wafanyakazi wa Wiz ya Afya? Waziri Mkuu nakumbuka alimtaja Dr. Ulimboka kuwa si mtumishi wa serikali bali ni Dr katika NGO. Ikawaje naye aongoze kwenye maslahi ya madokta wa serikali.

  Inabidi wote tutafakari kwa undani pamoja na kuwa madai ya madaktari yana ukweli ulowazi.
   
 2. wizaga

  wizaga Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mazungumzo yalivyoanza kwa interns kisha MAT kupenduliwa na sijui Jopo la Madaktari yote hayo hayajanikalia vizuri kichwani mwangu. Sijui nimuulize nani swali linalo nisumbua 'Jee Madaktari walikuwa wameshahakikiwa' hamna madaktari hewa? Ama huu ulikuwa ujanja wa Wajanja ili kuvuruga juhudi za serikali kuhakiki wafanyakazi wa Wiz ya Afya? Waziri Mkuu nakumbuka alimtaja Dr. Ulimboka kuwa si mtumishi wa serikali bali ni Dr katika NGO. Ikawaje naye aongoze kwenye maslahi ya madokta wa serikali.

  Inabidi wote tutafakari kwa undani pamoja na kuwa madai ya madaktari yana ukweli ulowazi.


  inavyoonekana hujui ulinenalo unapoitwa dr haimaanishi ni yule aliyepo muhimbili au serikalini tu,jumuia ya dr(MAT) haina mipaka na kunakanuni zake ,viongozi wake wanatokana na mkutanano wao wa mwaka hivyo huchagua viongozi wanaowapenda kidemocrasia.uanachama huu haimanishi upo NGO au ikulu au mbunge wote ni madr na wanawajibu wa kutii constutional yao.
   
 3. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Swali bado lipo palepale Jee Madaktari walikuwa wameshahakikiwa? Pengine yapo yalionipita juu ya harakati za mgomo. Na nakubaliana nawe juu ya mgomo kuwa ni maazimio ya MAT kikao cha dharura. Hivyo mbona mgomo umeelekezwa kwa hospitali za serikali na baadhi ya hospitali za Dhehebu la Kikristo? Mbona madokta hao hao wameendelea na kazi katika hospitali binafsi? Jee hamna agenda ya siri ndani yake?
   
 4. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kamuulize Pinda maana naona ndiye mwalimu unayemsikiliza vizuri na kumwelewa. Umejibiwa pale juu, ugumu uko wapi? Hujiulizi wanapoletwa wanajeshi Muhimbili, wanatawanywa nchi nzima kwenye hospitali za serikali. Na hospitali zao wanajeshi wakati huo zinahudumiwa na nani? Hicho ni kiini macho cha serikali kuonyesha wanaweza. Kila mara wanapotaka kutumia ubabe huwapeleka wanajeshi Muhimbili ambao hata ukiwauliza wenyewe wanajeshi wanaunga mkono madaktari lakini kwa vile ni amri moja kwa kazi zao kufuatwa wanalazimika, kwani wanajeshi sio wtumishi wa serikali? Sikilizia sasa episiotomy inafungwa moja kwa moja pamoja na nanihii yenyewe, nimeisikia Muhimbili japo sijui kama ni kweli. Kiasi kwamba wagonjwa wanajiuliza, mtu aliyejifunza kuua na kisha kutibu majeraha ili apate habari za adui, au atibu mwenzake na kisha arudi mstari wa mbele kuangalia majeruhi wengine, inakuwaje sasa na acute abdomen na episiotomy? O.K, hayo wanauliza wasiojua sana kwamba mafunzo ya udaktari hayabagui na discipline ni zilezile isipokuwa magwanda tu, tena saa nyingine nchi za wenzetu madaktari wa kijeshi wamejizatiti zaidi kulikoni uraiani na ni wabobea hasa katika mambo ya upasuaji ambao unahitaji ujasiri wa ziada. Habari za Ghost doctors zinasemwa na watu wanaofanana na hao wanaojiuliza maswali ya upeo wa madaktari wa kijeshi. Tatizo hapa sio nani anatibu kutoka wapi, lakini je, coverage ya wanajeshi kweli inakidhi hospitali zote nchini wakati huu serikali inapojenga kiburi? Inawfanya watanzania guinea pigs.
   
 5. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Madaktari wa Jeshi ni wazuri tena sana. Hata wao hawapendelei kuja hospitali za kiraia bali wamefuata amri. Kwa uelewa wangu mdogo ni kuwa Madaktari wa Jeshi wameitwa na serikali angalau kuziba pengo la wale waliogoma. Tujuwe kuwa mwajiri mkuu wa wote hao ni serikali ya JMT. Mazungumzo ya mgomo ukisha na hawa wanajeshi watarudi kwao kambini. Hali ingezidi kuwa mbaya naamini wangeomba msaada kwa hospitali binafsi na hata wa kuazima kutoka nchi jirani.

  Wiki hii madaktari 10,000 wa India waligoma na hao hao jeshi la kwao likatoa msaada kwa wagonjwa japo sio kwa kiasi kikubwa lakini wapo wamesaidia.

  Unadhani na Manesi wangegoma ingekuwaje? Kesheshe kubwa zaidi. Wangeletwa wa jeshini na wa Red Cross wasaidie kuziba pengo tu. Ukweli ni kwamba Madokta watarudi wataokubali na hali ya nchi ilivyo watarudi kazini na hali itarudi ya kawaida.
   
Loading...