Tishio la mgomo wa madaktari lipatiwe ufumbuzi haraka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tishio la mgomo wa madaktari lipatiwe ufumbuzi haraka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 12, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  [​IMG]  MGOGORO wa kimasilahi ulioibuka Januari na Machi, mwaka huu baina ya madaktari na Serikali ambao ulitulizwa, sasa unaelekea kuumuka upya. Hii ni kutokana na kauli ya madaktari iliyotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa watatangaza mgomo wa nchi nzima kama Serikali haitayapatia ufumbuzi matatizo yao, kama ilivyoahidi wakati wa kuuzima mgomo uliopita.


  Wanachama wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) walikutana jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita kujadili mustakabali wao baada ya Serikali kushindwa kutekeleza ahadi walizokubaliana wakati wa kumaliza mgomo uliyopita.


  Maafikiano ya awali yalilenga kutekeleza mdai ya madaktari ya nyongeza ya mishahara yao, kuboresha mazingira ya kazi ili yafikie viwango vitakavyowawezesha kutoa huduma nzuri kwa wananchi, marupurupu, nyongeza ya posho ya kuitwa kazini kwa dharura na posho za nyumba na chanjo.
  Madaktari wanadai kuwa Serikali kali imeshindwa kutekeleza ahadi ilizowapa wakati wa kumaliza mgomo wa awali ulichukua zaidi ya wiki moja na kusababisha huduma za afya kusimama katika hospitali nyingi nchini.


  Kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa na Rais wa MAT, Dk. Namala Mkopi, katika kikao cha ndani cha madaktari kilichofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, wanachama walikubaliana kutangaza mgogoro wa wiki mbili na Serikali kutokana na kushindwa kutelekeza ahadi zake na baada ya hapo watachukua hatua zaidi ikiwamo kuitisha mgomo wa nchi nzima.


  Hata hivyo, baada ya tishio hilo, Serikali imekubali kurudi kwenye meza ya mazungumzo ili kuepusha mgomo unaoweza kuleta madhara makubwa kwa jamii.


  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Hussein Mwinyi alisema alipohojiwa na gazeti hili Jumapili iliyopita kwamba, baada ya MAT kufikisha taarifa ya kamati iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa wanachama wake na wao kukataliwa, Serikali iliamua kurudi kwenye mazungumzo ili kufikia mwafana kwa kuwa hakuna linaloshindikana.


  Kwa ujumla, tunaipongeza Serikali kwa kukubali kurudi kwenye mazungumzo kutafuta mwafaka wa mgogoro huo wa muda mrefu kuonyesha kuwa ina nia ya kushirikiana na madaktari kuepusha mgomo ambao utaleta madhara makubwa kwa wananchi na hasa wasio na uwezo wa kujilipia katika hospitali binafsi.
  Hiyo ni hatua nzuri; hata kama utelezaji wa makubaliano ya awali yameshindikana kutekeleza kwa kile kilicholezwa kuwa ni kutokana na Serikali kukosa fedha.


  Pamoja na hayo, hatua hiyo ilitakiwa kuchukuliwa mapema kwa Serikali kuitisha kikao cha ushirikiano mwema na madaktari kuwaeleza ukweli, badala ya kungoja taarifa ya kamati ya iliyoundwa na Waziri Mkuu kupelekwa wa wanachama wa MAT.


  Tunasema hivyo kwa sababu pamoja na kuundwa kwa kamati hiyo, Serikali ilikuwa inajua kikamilifu hali yake ya kifedha kutokana na ukweli kwamba, mambo mengi ya msingi katika sekta mbalimbali nchini yamekwama kutekelezwa kutokana na mapato yake ya ndani kutofikia malengo.


  Ni ukweli usiopingika kuwa, suala la mgogoro wa madaktari ni nyeti na lina madhara makubwa kwa ustawi wa Taifa lisiposhughulikiwa mapema kwa ushirikiano wa pande zote mbili.


  Hata hivyo, tunaishauri Serikali iwe wazi inaposhughulikia masuala nyeti kama hayo kwa kutotoa ahadi zisizotekelezeka, kinyume cha hapo itakuwa inachochea watu kuchukua hatua zisizo za kistaarabu kushinikiza wapewe haki zao.


  Tunashauri kwamba, kutokana na unyeti wa huduma ya afya ni muhimu Serikali na madaktari waangalie zaidi masilahi ya wananchi ambao ndiyo msingi wa maendeleo katika nchi yetu kwa kuwa, ndiyo nguvu kazi ya taifa.


  Tunamaanisha kwamba, taifa la watu wagonjwa haliwezi kufanya kazi uzalishaji na asilimia kubwa ya Watanzania, ambao ndiyo tegemeo katika shughuli za usalishaji ni wale wa kipato cha chini na kati ambacho hakiwawezeshi kujilipia gharama za matibabu pamoja na familia zao katika hospitali za binafsi

  Tishio la mgomo wa madaktari lipatiwe ufumbuzi haraka
   
 2. Brightman Jr

  Brightman Jr JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 1,233
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Bila shaka wahusika wanayo taarifa. Tusubirie tuone.....!
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,091
  Likes Received: 6,557
  Trophy Points: 280
  Vuteni subra wakuu si wabaya wenu tayari wamepigwa chini.
   
Loading...