Mgomo: Dodoma, Ruvuma, Songea, Morogoro, Mwanza, Mbeya wawapokea wafanyabiashara wa Dar

MLIPAKODI

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
234
88
Nimepita maeneo ya soko la Sido Kabwe na Mwanjelwa nimekuta maduka yote yamefungwa. Nimejaribu kudadisi kwa wadau wanasema kisa ni kukamatwa kwa mwenyekiti wa wafanyabiashara taifa.

Wameamua kufanya mgomo ili aweze kuachiwa kwani ni mkombozi wa wafanyabiashara nchi nzima.

Wanasema alikamatwa Dar na kuhamishwa kwa siri hadi Dodoma wamesema wadau hao. Kwa mujibu wa wadau mgomo huo utakuwa nchi nzima, sijajua maeneo mengine.

My take:
Serikali kama itaendelea na mfumo huu tutafika wapi?

Nawasilisha

Baada ya jana kukamatwa kwa Mwenyekiti wa wafanyabiashara Kariakoo jijini Dar es Salaam, Taarifa kutoka mkoani Dodoma na maeneo mengine, zinaeleza kuwa leo wafanyabiashara Mikoani nao wamegoma kushinikiza kuachiliwa na kujua hatima ya kiongozi wao Johsoni Minja aliyekamatwa na jeshi la polisi jijini Dar es Salaam kwa kosa la kuhamasisha wafanya biashara kukataa matumizi ya mashine za kieletronic za kutolea risiti za EFD.

WAFANYABIASHARA wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamelazimika kufunga maduka yao kupinga kitendo cha kukamatwa Mwenyekiti wao wa Jumuia ya Wafanyabiashara nchini David Minja na kwamba mgomo huo utadumu mpaka hapo watakapopata uhakika wa usalama wake na si vinginevyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jana Ofisini Kwake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Tawi la Ruvuma Isaya Mbilinyi Mwilamba Alisema Kuwa Tumefunga Maduka tukiwa Tunamtafuta Mwenyekiti wetu Minja kwani hatuna sababu ya kuendelea na biashara zetu wakati Kiongozi kakamatwa na Jeshi la Polisi Nchini

Mwilamba Alisema kuwa Tunasitisha Shughuli mpaka Tujue Hatma ya Kiongozi wetu ambaye Kimsingi ndiye Mtetezi wa Unyonyaji wa Serikali Kupitia Mgongo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Hata hivyo Hatufungui Maduka Mpaka Serikali ituambie kwa kina kwanini wamemkamata kiongozi huyo na endapo wakimuachia sisi tupo Tayari kufungua Maduka

Alifafanua kuwa Kiongozi wetu alikuwa ni Mjumbe wa Kamati ya Majadiliano ambayo imeundwa kwa Pamoja Kati ya Wafanyabiashara na TRA yenye lengo la Kujadili changamoto mbalimbali ambazo zinatokana na malalamiko ya wafanyabiashara kuhusu matumizi ya Mashine za Kietroniki za kulipia Kodi EFD

"Tunaitaka Serikali Izingatia Nia Njema ya kuundwa kwa kamati hiyo ya Majadiliano na itoe taarifa stahiki kwa wafanyabiashara kwani tunapata wasiwasi kuwa kukamatwa kwake kiongozi wetu kunatokana na juhudi za wafanyabiashara kupinga ongezeko la kodi kwa Asilimia mia moja na matumizi ya mashine za EFD" Alisema Mwilamba

Alisema Serikali inapaswa kutumia njia za kidemokrasia kumaliza changamoto zake na sio kutumia nguvu kuzima madai ya msingi ya wafanyabiashara hivyo ni vyema ikasikiliza kilio cha wafanyabiashara ambao kimsingi ndio wachangiaji wakubwa wa kodi za Serikali

Katibu wa jumuiya ya wafanyabiashara mkoani Ruvuma Kipara Nziku alisema kuwa serikali imekurupuka kumkamata mwenyekiti wao kwani tayari walishakuwa kwenye mazungumzo na TRA juu ya mashine za EFD na swala la wafanyabiashara kukataa kulipa kodi hivyo ingekuwa vyema kusubili muafka wa majadiliano hayo.

Alisema kuwa madai ya serikali juu ya mwenyekiti huyo ya kwamba anachochea wafanyabiashara wasinunue mashine za EFD pamoja na wafanyabiashara nchini wakatae kulipa kodi kimsingi hayana mantiki yeyote hivyo ni lazima busara itumike.

Hata hivyo amewaomba wafanyabiashara mkoani humo kuendelea kuwa wavumilivu na watulivu kwa kipindi hiki ambacho wamesitisha hutuma hadi hapo hatima ya mwenyekiti wao Minja itakapopatikana.

Kwa upande wake Meneja wa TRA Mkoa wa Ruvuma Apili Mbaruku akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake alisema kuwa mgomo wa wafanyabiashara ahuhusiki kabisa na TRA bali jambo hilo linahusika na jeshi la polisi ambalo ndilo linajuwa mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Minja amekamatwa kwa sababu gani.

Hata hivyo Meneja huyo alipohojiwa na waandishi wa habari juu ya athari gani ambazo wanazipata juu ya mgomo huo alisema kuwa kwa sasa ni mapema mno kujuwa hasara kwani TRA wamekuwa wakikadilia mapato ya wafanyabiashara kwa mwaka na sio kwasiku hivyo ni vigumu kuelezea.

Nae kaimu Afisa biashara Mkoa wa Ruvuma Furaha Mwangakala alisema kuwa swala kwa sasa wapo mbioni kumfikishia mku wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ili aweze kutoa kauli ya mwisho ya serikali ya Mkoa.

Katibu mtendaji wa Chemba ya wafanyabiashara ,Kilimo na Viwanda (TCCIA)mkoa wa Ruvuma Philimon Moyo alisema kuwa kwa sasa hana cha kusema kwa sababu jumuia hiyo ya wafanyabiashara mkoani humo imeonesha kutowatambua TCCIA.

Jitihada za kumpata Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ziligonga mwamba baada ya Katibu wake Revokatus Kasimba kuwaambia waandishi kuwa mkuu wa Mkoa yupo kwenye kikao hivyo hataweza kuongea na waandishi wa habari hadi hapo atakapomaliza kikao.

MWISHO.
 
Kama ilivyotokea kwa wakazi wa dsm jana,wafanyabiashara wa dodoma hawajafungua maduka yao kushinikiza kuachiliwa huru kwa mwenyekiti wao bwana Johnson Minja.

Taarifa za ndani zinaeleza mwenyekiti huyo alisafirisha jana kutoka dsm kuja dom kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka ya kushawishi wafanyabiasha kugomea kuchukua mashine za TRA.

Tutaendelea kujuzana.


Updates
Morogoro,
Iringa na mwanza pia nimepata taarifa wapo katika mgomo huo pia.
 
Wabunge tusaidieni jamani. Hizi mashine ni biashara ya wakubwa.

Mimi niliinunua 1.5m mashine ambayo leo inapatikana kwa chini ya 800k. Mbaya zaidi, kabla tulipewa semina na maofisa wa TRA pamoja na suppliers wa mashine hizo na tukaahidiwa kuwa suppliers wangekuwa wanazifanyia regular service.

Tangu 2010 niliponunua mashine hiyo sijamuona mtu wa kuja kuifanyia service, na imenigharimu mara mbili kuipeleka Mwanza toka Musoma niliko kwa vitu vidogo eti software updates, kwanini mfanyabiashara abebeshwe mizigo hii?

Tusaidieni wabunge tafadhalini.
 
Habari zilizonifikia hivi punde tu kutoka Iringa zinasema,wafanyabiashara wa huko Iringa nao wamegoma kushinikiza kuachiwa huru kwa kiongozi wao. Maduka yamefungwa
 
Ingependeza kama ungeandika na dondoo za muktadha wa habari manake hii habari inatakiwa na jamii
Sakata la mashine sio jipya ndugu yangu,ni muendelezo wa kudai usawa katika jambo hili, walianza dar,leo dom.
 
Serikali wanatakiwa kukaa chini na kutafakari kuhusu hizi machine za TRA.

Inaonyesha kama kuna harufu ya mkono wa mtu kuhusu suala la kuletwa hizi machine

Matumizi ya nguvu daima yanaumiza nyasi na siyo mafahali wanaopambana.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Hili swala serikari inatakiwa ikae chini na wafanyabiashara wakubaliane kwa amani la sivyo linaweza kuchafua hali ya hewa
 
Duh?

Ama kweli mnaikalia Serikali kooni. Jkt imesitishwa kwa sababu za. Kukosekana fungu. Wakandarasi wamesimamisha ujenzi. Kisa hawajapatia stahiki zao, wahisani wamegoma kutoka fungu waliloahidi.

Mmbaya zaidi pale paliposalia kwa Serikali kupata fedha nanyi mnawagomea kutofungua biashara watapata wapi kodi waweze endesha Serikali yao?

Mwigulu Nchemba a.k.a Sokoine wa Pili
a.k.a Simba wa vita a.k.a Mzalendo a.k.a mtetezi wa wananchi uko wapi?
 
Hizo kodi tunazolipa huwa zinaenda wapi?
maana naambiwa nchi inaongoza kwa kukopa na kupewa miaada na ni ya pili baada ya Iraq..
_mbaya zaidi deni la taifa linatishia uhai wa kutokukopeshwa...



kodi zetu zinaenda wapi?
 
Back
Top Bottom