MGOMO DAR: Wafanyakazi wa Pepsi wagoma kufanya kazi

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
Wafanyakazi wa Pepsi wamegoma leo kufanya kazi wakidai kupewa mikataba ya ajira, nyongeza ya mishahara. Polisi wamefika kwenye tukio.

Hii news item ya maslahi ya wafanyakazi wa Kiwanda cha Pepsi imenigusa, kwamba wamepunguziwa mshahara, sasa mama mmoja anaeleza namna alivyotumikia kiwanda kwa muda mrefu, amenishangaza kwa kudai eti alianza kazi hapo wakati maziwa (matiti) yamesimama na sasa yamelala.

Sasa sijui hii ina maana gani?
 
Pepsi wameshusha bei soda zao halafu wanapunguza mishahara ya wafanyakazi,

walidhani wakishusha bei watauza volume kubwa zaidi hivyo kupata mapato makubwa zaidi,

ila wafanyabiashara soda hawajashusha kwa maduka mengi japokuwa pepsi wanawauzia kwa bei ya chini, wanatamaa ya kupata faida zaidi

gamble ya Pepsi imefeli, inabidi washushe nishahara kufidia hasara.....

fundisho tunalopata hapa ni mzalishaji usishushe bidhaa yako bei ili uuze zaidi hata kama gharama za uzalishaji zimepungua, vitu huwa havishuki bei
 
Na wafanyakazi na vibaru wa Coca Cola yawapasa kuiga mfano wa wenzenu wa PEPSI.

Wahindi wa PEPSI wamezidi kwa unyonyaji.

After all, kugoma ni haki ya msingi kabisa ya mfantakazi.
 
Back
Top Bottom