Mgombea

Mgombea: mkinipa kura zenu nitahakikisha darisalam kunamwagika Snow.
Wananchi: Khaaa!
Mgombea: msishangae, hata London kabla Tony Blair kulikuwa hakuna snow.
 
Mgombea: Nikikabidhiwa ofisi rasmi nitahakikisha kila nyumba inakuwa na washing machine.
Wanakijiji: Mheshimiwa huyo (washing machine) ndio nani ?
Mgombea: Basi nitaleta mwalimu wa kiingereza kabla washing machine
Wanakijiji: Mheshimiwa huo ni ubaguzi sasa.
 
Mgombea:Nita hakikisha shule zote zinakuwa na compyuta
Wanakijiji:Hata umeme hatujawahi kuwa nao tutazifanyia nini?
Mgombea:Msiwe na wasi wasi mtaanza kujifunza kwa nadharia kwanza
Wanakijiji:Mbona sisi hatumfahamu huyo nadharia?au umekuja nae kutoka mjini?
 
Mgombea: Tutaagiza helikopta za kupelekea wagonjwa hospitali.
Wananchi: Mheshimiwa uchaguzi uliopita ulituahidi ambulances lakini hatujaziona mpaka leo.
Mgombea: Zipo njiani, zimekwama kwenye Traffic hapo msumbiji na hili tatizo la traffic ndio limetufanya tuje na mbinu ya Helikopta.
Wananchi: sasa tumekuelewa mheshimiwa.
 
Mgombea: Ndugu wananchi hivi sasa ni vita, na mnajua tutakwenda vipi vitani?
Wananchi: Wewe mbele sisi nyumaaaaa!
Mgombea: mabasha wakubwa nyinyi! tutakwenda bega kwa bega.
Wananchi: khaaaa!
 
Mgombea: Ndugu wananchi hivi sasa ni vita, na mnajua tutakwenda vipi vitani?
Wananchi: Wewe mbele sisi nyumaaaaa!
Mgombea: mabasha wakubwa nyinyi! tutakwenda bega kwa bega.
Wananchi: khaaaa!
hahhahahh mgombea mwoga
 
Back
Top Bottom