Mgombea Wangu Wa Urais Huyu Hapa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea Wangu Wa Urais Huyu Hapa!!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by W. J. Malecela, Jan 30, 2014.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  Jan 30, 2014
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,858
  Likes Received: 3,137
  Trophy Points: 280
  - Mgombea wangu wa Urais ni yule atakayenihakikishia kurudisha nyumba zote za Serikali zilizouziwa Viongozi na Wafanyakazi wa Serikali kuanzia na Awamu ya Tatu. I don't care what haukuwa uamuzi fair kwa Wananchi wa Taifa hili na ninasema bila kuchanganya maneno ni moja ya pungufu kubwa sana la CCM chama changu. Nilimuunga sana mkono Rais wa sasa wakati wa mbio zake za kugombea Urais nikiamini kwamba ungekuwa ndio uamuzi wake wa kwanza kuufanya akiingia Ikulu, mpaka leo nashangaa kilichomtokea mpaka kutoligusa hili.

  - I mean, nyumba karibu zote walizopewa hawa Viongozi na Wafanyakazi wa Serikali, wameishia kuuzia Wahindi na Wa-South Africa ambao sasa wanaporomosha magorofa, ikiwa na maana hawa wanapata Pesheni za walipa kodi wananchi na hela za nyumba za Serikali walizouza na wengine wameingia ubia na hawa wajengaji, kwa kitu gani cha ajabu walichokifanyia Taifa?

  - Nasema tena mgombea Urais atakayenihakikishia kurudisha nyumba za Serikali kwa Umma kama zilizvyokuwa mwanzoni, NITAMPA KURA YANGU YA URAIS NA NITAMPIGIA KAMPENI HATA KUANZIA LEO IF I HAVE TOO!!


  Le Mutuz
   
 2. Mlayjr

  Mlayjr JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2014
  Joined: May 7, 2013
  Messages: 372
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  :A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1:
   
 3. r

  rpg JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2014
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Leo umenena,

  naona siku hizi macho yamepungua utando, na umeanza kuona jinsi chama chako kilivyopoteza dira! Sio nyumba tu, madini, gesi, bandari, utendaji katika ofisi za serikali. nk

  Ni vema pia ukakumbuka Meremeta, the green, airtell vs TTCL, radar, uzio wa ikulu, jengo la bunge, malipo kwa wajumbe wa tume ya katiba, urasimu wizara ya ardhi na nyumba na mengine mengi. Hapo ndo nitakapoamini wewe ni mzalendo wa kweli
   
 4. Snipper

  Snipper JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2014
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 891
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 180
  Vipi mzee wetu J4 mgao wa mjengo ulimpita nini? Maana hii siyo kawaida ya magamba
   
 5. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #5
  Jan 30, 2014
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,858
  Likes Received: 3,137
  Trophy Points: 280
  - Unajua nyie mnahitaji kunyamaza kwa sababu kwenye haya maamuzi mlihusika sana, hayo yote uliyoyataja yanapitishwa na Kamati za Bunge kwanza halafu bunge lenyewe ambalo lina Wabunge wa chama chako so hata nyie huko mnahusika!!

  Le Mutuz
   
 6. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2014
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,588
  Likes Received: 2,934
  Trophy Points: 280
  Usihofu andaa kura yako tu wakati ukifika weka vema kwa CHADEMA yote hayo yatapatikana.
   
 7. Msingida

  Msingida JF-Expert Member

  #7
  Jan 30, 2014
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 3,882
  Likes Received: 835
  Trophy Points: 280
  Le Mutuz,
  Unaonekana upo CCM kwa sababu tu ya historia yenu na mlivyo faidi enzi hizo,lakini kiakili haupo huko.Kwa hiyo unamaanisha Magufuli Pombe hafai kuwa mgobea Urais?Pia unaonekana umekata tamaa na Rais Kikwete?
  Umechukua hatua gani kama Mccm kwenye vikao halali vya chama kuhusiana na hilo?
  Ushauri wa bure, hamia upinzani ili malengo yako yaweze kutimia.
   
 8. C

  Chikaka Sumuni JF-Expert Member

  #8
  Jan 30, 2014
  Joined: May 16, 2013
  Messages: 1,339
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa Kanisani tungesema umeanza kuokoka, sasa Karibu kwenye harakati za kupigania haki za za wanyonge, suisahau kumwamsha na Lukosi, Riz1, HamyD, na wale ambao wamepigwa uzezeta hawaoni masuala wanadiscuss personalities, hapa mdogo wangu sasa nimekupata "You have made my day today"
   
 9. kwamtoro

  kwamtoro JF-Expert Member

  #9
  Jan 30, 2014
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 4,815
  Likes Received: 780
  Trophy Points: 280
  Looohhh!! Amna Rais ajaye yeyote atakaye weza fanya hilo. Yalio marahisi sana yamewashinda walio mtangulia na aliyopo madarakani. CCM ni janga la kitaifa kama siyo kimataifa. Kaka @W. J. Malecela njia pekee bila ya kupepesa macho ni kabadili mfumo mzima wa utawala, CCM walipotufikisha panatosha waachie wengine waongoze nchi. Mybe tutaweza fika angalau robo huko tukutakako.
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Jan 30, 2014
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 160
  Mgombea wa hivyo hayuko CCM...

  Uko tayari kumtafuta kwenye pool ya wazelendo wasio na mawaa ya ufisadi wa kupindukia kama wa ndugu zako wa CCM?
   
 11. m

  mungo JF-Expert Member

  #11
  Jan 30, 2014
  Joined: Mar 27, 2008
  Messages: 212
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  That is very good. hakuna kitu huwa kinaniuma kama kuuzwa kwa hizo nyumba, tena kwa bei ya kutupa wakati nyumba nyingi ziko kwenye prime area.
   
 12. kajirita

  kajirita JF-Expert Member

  #12
  Jan 30, 2014
  Joined: Jul 27, 2013
  Messages: 1,579
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Naona kadri siku zinavyokwenda unakua KI-AKILI badala ya KIMWILI!

  Hongera kwa kuanza kujitambua!
   
 13. Msandawe Halisi

  Msandawe Halisi JF-Expert Member

  #13
  Jan 30, 2014
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Kweli vidonge vya mirembe vinafanya kazi watu wanapona mahaba ya chama.
   
 14. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #14
  Jan 30, 2014
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,470
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Umenena vizuri kijana. Lakini unajua kabisa CCM hakuna mtu atakayethubutu kutengua ya watangulizi wake maana naye ana yake anaogopa kuumbuliwa. Je, utamuunga mgombea huyo hata kama si kutoka CCM? Kama laa, basi kijana unatuuzia chai tu hapa.
  2015 ni mwakani tu, thread hii tutaweza kuirejea wakati utakopkuwa unamuunga huyo mgombea tuoene kama kweli unatenda unayosema. Wasiwasi wangu ni vijana wengi CCM mnasumbuliwa na tamaa ya kuwa madarakani, kwa hiyo mnayumbishwa na makundi ya wagombea watarajiwa 2015.
   
 15. Iyokopokomayoko

  Iyokopokomayoko JF-Expert Member

  #15
  Jan 30, 2014
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 1,806
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Wazo zuri sana hili, hongera mleta mada
   
 16. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #16
  Jan 30, 2014
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,765
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu,

  Unachokisema wewe hakiwezi kutekelezwa na Mtu mgombea atakayetoka CCM, kwa sababu walishiriki moja kwa moja na uuzwaji ule na wengi wao ndiyo walionunua zile nyumba kwa bei ya Kutupa.

  Je unataka kutuambia Mgombea wako atazirudisha zile nyumba vipi??? Je kama wanaCCM karibu wote wlinufaika na Zile nyumba huenda akiwemo Mzee Malecela, atakubali kumpigia debe? Nyumba nyingi zilichukuliwa na Wafadhili wakubwa wa CCM, je CCM ina ubavu wa kuwatosa, hasa ukizingatia kwa sasa CCM iko hoi kiuchumi?

  Sidhani kama kuna mtu au Kiongozi ndai ya CCM ana huo ubavu labda baada ya CCM kuwa Chama cha Upinzani kwa miaka isiyopungua 30-40 ndiyo itakuja generation ambayo haijachafuka.
   
 17. t

  twende kazi JF-Expert Member

  #17
  Jan 30, 2014
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,497
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Bonge nyanya anytime utasikia yupo chadema.Time will tell.Big up kamanda
   
 18. msema_kweli

  msema_kweli Senior Member

  #18
  Jan 30, 2014
  Joined: Nov 6, 2013
  Messages: 138
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Haya ndiyo maneno hambayo watanzania wengi tunatamani kusikia kutoka kwa watu kama nyie
   
 19. BJEVI

  BJEVI JF-Expert Member

  #19
  Jan 30, 2014
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 1,360
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  kwa mara ya kwanza nipo upande wako.hongera kwa mtizamo chanya.
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Jan 30, 2014
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 160
  Siyo rahis kutoka huko ndugu....

  Ulishaona wapi msukule ukajinasua wenyewe?? Ila ukitoka mmoja kama huyu Le Mutuz nadhani mingine inaweza kutoroka pia!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...