Mgombea wa urais na maneno ya ukakasi

Mgombea wa urais na maneno ya ukakasi

Josorobert

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2015
Posts
629
Reaction score
215
Miezi miwili na ushee iliyopita mgombea huyu aliulizwa na wahariri wa magazeti iwapo atahama CCM kama haitamchagua kugombea urais mwaka huu. Jibu lake lilikuwa kwamba hatahama CCM kamwe kwa sababu ilimlea, na kwamba huyo ambaye hamtaki ndani ya CCM ndiye ahame chama hicho!

Hata hivyo, kabla mwezi haujakatika mgombea huyu akakihama chama hicho na kujiunga na chama cha Upinzani, na chama hicho kikamteua kugombea urais, na sasa kuna -vijana wanamshabikia! Kimsingi aliongopa katika jibu lake lile na taswira aliyojijengea ni ya mtu asiyeaminika katika kile anachosema.

Ingekuwa ni Wazungu au sisi watu wenye kufikiri sawasawa, tusingemshabikia -katika mbio zake za urais kwa sababu ni mtu mwongo, kigeugeu na asiyeaminika, mtu asiyeweza kusimamia maneno yake mwenyewe.

Lakini kwa uwezo wetu mdogo wa kufikiri, baadhi yetu- tunamzawadia mgombea huyo kwa kumuunga mkono kwenye kampeni yake ya kuusaka urais kwa udi na uvumba!

Uongo na ukigeugeu kama huo pengine ungevumilika kama nafasi yenyewe anayowania si urais. Lakini urais ni kazi yenye heshima, utukufu, uadilifu nk. Ni kazi ambayo haimfai mtu mwongo na asiyesimamia maneno yake mwenyewe.

Vijana wetu hawajiulizi, kama huyu alidiriki kutudanganya jana, kwa nini asiendelee kutudanganya hata leo au hata baada ya kuingia Ikulu.

Tutamwamini vipi katika hayo anayodai kuwa atatutendea akiingia Ikulu kama huko nyuma aliwahi kutudanganya kwa kushindwa kusimamia maneno yake mwenyewe? TAFAKARI:
 
Hebu fupisha halafu tueleze ni kitu gani unataka kutuambia! Maana kama kipimo ni hayo maneno yake basi tuanze na maneno ya CCM tena yale ya juzi juzi tu ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania....
 
Kila mwenye kufanya kazi lazima atakuwa na maisha bora lakini kama ni kupiga makelele, kuandamana, viroba si rahisi ukapata maisha bora.
 
Lakini hamkuyasema hayo kabla! Mmetugeuka mida hii na kuja na kauli hio. Ok kwahio hata malimbikizo ya Walimu, Madaktari na wengineo nao ni wanywa viroba? Je walioweka haki ya kiandamana nao pia walikua wanywa viroba? Kwahio umaskini uliokithiri Tanzania umeletwa na viroba na maandamano? Na kama jibu ni NDIO je viroba hivyo na maandamano hayo yaliruhusiwa na serikali ya chama gani? Kama ni CCM, je nitakua sahihi kusema CCM imeunda serikali ya hovyo kupata kutokea duniani? Haahahaahaaaaaa haya umeshinda. Njooni mtuahidi tena na KAZI TU nasi tutawaonyesha hio Kazi tu hapo October 25
 
Makosa yanafanyika popote hata katika family level, but at what %. CCM imefanya kazi yake na imeonekana, kwa sasa tunahitaji kiongozi mwingine atakaelivusha taifa hili kwenda hatua nyingine, kiongozi mwenye maadili, mcha Mungu, anayependa watu wake na sio mwenye kutanguliza udini.
 
Maisha bora huku ukiwa unakaa gogo vivu kijiwen amka #hapa kazi tu
 
Makosa yanafanyika popote hata katika family level, but at what %. CCM imefanya kazi yake na imeonekana, kwa sasa tunahitaji kiongozi mwingine atakaelivusha taifa hili kwenda hatua nyingine, kiongozi mwenye maadili, mcha Mungu, anayependa watu wake na sio mwenye kutanguliza udini.

Mabadiliko yenye maendeleo ni MAGUFULI TU
 
Kumbuka CCM sio Mama yake Lowassa. Kumbuka katika medani za siasa maaamuzi ya jambo lolote muhimu kwa mustakali wa mwanasiasa mahiri unategemea zaidi muktadha wa jambo lenyewe na pia zikitegemea zaidi alama za nyakati na majira yake. Haya ni majira ya MABADILIKO na Lowassa ameona na ameitambua fursa hii.

Sasa wewe ulitaka Lowassa aendeleee kung'ang'ana na CCM mpaka lini? na ili iweje haswa?
 
.
Asiye kubali kushindwa c ........,,ata hangaika lakini October ni magufuli tu
 
Nasikia eti ule ugonjwa wake umekula kumbukumbu zote
Hata kile anachokiahidi ukimuuliza kesho hakijui

Maskin lowasa
Huyu apumzke tu
 
Lowasa anaugonjwa wa kupoteza fahamu.ugonjwa huu mara nyingi mtu hupoteza hadi kumbukumbu pia hili ndio tatizo la Lowasa alipohama chama alisahau kama alisema hata hama chama. Nice tariff sana kuwa na Rais kama huyu
 
Kila mwenye kufanya kazi lazima atakuwa na maisha bora lakini kama ni kupiga makelele, kuandamana, viroba si rahisi ukapata maisha bora.

Acha kutukana Watz ina maana ndg zetu wanao kosa matibabu kisa pesa ni malofa na wapumbavu?
 
Mmmmh,,,,,

====
user-online.png
lyanda el

Today 03:27
#8 ​
MemberArray

Join Date : 11th September 2015
Posts : 87
Rep Power : 320
Likes Received13
Likes Given​

Josorobert

Today 03:11
#1 ​
Senior MemberArray

Join Date : 14th September 2015
Posts : 115
Rep Power : 325
Likes Received46
Likes Given0

​
 
Lakini hamkuyasema hayo kabla! Mmetugeuka mida hii na kuja na kauli hio. Ok kwahio hata malimbikizo ya Walimu, Madaktari na wengineo nao ni wanywa viroba? Je walioweka haki ya kiandamana nao pia walikua wanywa viroba? Kwahio umaskini uliokithiri Tanzania umeletwa na viroba na maandamano? Na kama jibu ni NDIO je viroba hivyo na maandamano hayo yaliruhusiwa na serikali ya chama gani? Kama ni CCM, je nitakua sahihi kusema CCM imeunda serikali ya hovyo kupata kutokea duniani? Haahahaahaaaaaa haya umeshinda. Njooni mtuahidi tena na KAZI TU nasi tutawaonyesha hio Kazi tu hapo October 25

Ndg yangu sikujua kama madaraka yanalevya zaidi kuliko kilevi
 
kazi tu mama ntilie wanavunjiwa vibana na kumwagiwa biashara zao,kazi tu waalimu na madaktari mishahara yao hawajalipwa na posho zao.kama muadilifu hata rungwe na anna ni waadilifu kwani wana kashfa gani wachagueni basi....
 
Kumbuka CCM sio Mama yake Lowassa. Kumbuka katika medani za siasa maaamuzi ya jambo lolote muhimu kwa mustakali wa mwanasiasa mahiri unategemea zaidi muktadha wa jambo lenyewe na pia zikitegemea zaidi alama za nyakati na majira yake. Haya ni majira ya MABADILIKO na Lowassa ameona na ameitambua fursa hii.

Sasa wewe ulitaka Lowassa aendeleee kung'ang'ana na CCM mpaka lini? na ili iweje haswa?

Kama ccm sio mama yake na lowasa
Sasa ww n bibi yake na lowasa mpaka aje akukumbuke akiwa rais (ingawa hawez labda urais wa 4u mvt)

Au ndo Yale yale ya vijana wa ukawa kufungua kijiwe na kukiita "wabishi camp"
alafu wanaomba mikopo bank
Mkikosa mnalaum
nan awakopeshe wabish
Hagaa

Chagua magufuli kwa maslahi mapana ya nchi
 
Miezi miwili na ushee iliyopita mgombea huyu aliulizwa na wahariri wa magazeti iwapo atahama CCM kama haitamchagua kugombea urais mwaka huu. Jibu lake lilikuwa kwamba hatahama CCM kamwe kwa sababu ilimlea, na kwamba huyo ambaye hamtaki ndani ya CCM ndiye ahame chama hicho!

Hata hivyo, kabla mwezi haujakatika mgombea huyu akakihama chama hicho na kujiunga na chama cha Upinzani, na chama hicho kikamteua kugombea urais, na sasa kuna -vijana wanamshabikia! Kimsingi aliongopa katika jibu lake lile na taswira aliyojijengea ni ya mtu asiyeaminika katika kile anachosema.

Ingekuwa ni Wazungu au sisi watu wenye kufikiri sawasawa, tusingemshabikia -katika mbio zake za urais kwa sababu ni mtu mwongo, kigeugeu na asiyeaminika, mtu asiyeweza kusimamia maneno yake mwenyewe.

Lakini kwa uwezo wetu mdogo wa kufikiri, baadhi yetu- tunamzawadia mgombea huyo kwa kumuunga mkono kwenye kampeni yake ya kuusaka urais kwa udi na uvumba!

Uongo na ukigeugeu kama huo pengine ungevumilika kama nafasi yenyewe anayowania si urais. Lakini urais ni kazi yenye heshima, utukufu, uadilifu nk. Ni kazi ambayo haimfai mtu mwongo na asiyesimamia maneno yake mwenyewe.

Vijana wetu hawajiulizi, kama huyu alidiriki kutudanganya jana, kwa nini asiendelee kutudanganya hata leo au hata baada ya kuingia Ikulu.

Tutamwamini vipi katika hayo anayodai kuwa atatutendea akiingia Ikulu kama huko nyuma aliwahi kutudanganya kwa kushindwa kusimamia maneno yake mwenyewe? TAFAKARI:
Mkuu ni mtanzania gani mwenye akili timamu bado anaiamini ccm,jiulize kama tusingekuwa tunawasomba watu kwa malori kuja kwenye mikutano yetu,tungekuwa tunamdanganya nani sasa
 
Back
Top Bottom