Elections 2015 Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

huyu mwizi wa nyumba za serikali

Ni kweli lakini ana hofu ya Mungu, waliobaki ni majizi kupindukia hata hofu ya shetani hawana! Mwenye kubisha anitajie waziri mmoja mwenye kumiliki bajeti ya wizara na kuitendea haki bajeti hiyo hata kwa 50%
 
magufuli ni mchapakazi lakini hafai kuwa kwa rais kwa sababu zifuatazo
1. intellectual arrogance - anadhan kua anajua kila kitu na akishaamua basi hakuna wazo jipya litakalokuja kuimprove alichoamua ni lazima kifanyike ivyo ivyo au hakuna wazo jipya litalomfanya abadili maamuz kwamba hicho anachokitaka kinawez kisiwe sahihi kwa mfano alivyokua anavunjia watu ovyo mpaka aliposhinwa ile kesi mahakamani wakat yy alikua anang'ang'ania kua anatimiza sheria.

2. hana uvumilivu - kiongoz bora yoyote lazima awe mvumilivu hasa anapokosolewa kwa mfano anapandoisha jazba kwa mambo madogo aliwambia watu wasioweza lipa nauli mpya ya kivuko wapige mbizi wakat kiongoz mzuri angekaa kimya tu.

3. anafata sheria kisabato - sheria hata kama ipo mda mwingine busara itumike kwa mfano anapong'ang'ania kuvunjia watu hata sehem zisizo na tija bila huruma nadhan akipewa lungu la urais watu watasaga meno kwa kigezo cha kufata sheria. ndo mana hata jesus aliuliza its ok usifanye kazi jmosi lakini ngombe wako akidumbukia mtoni hutamtoa busara ya bwana magufuli ni kwamba sitamtoa acha afe!!!

4. atakua haeshim judiciary - kitendo chake cha kujitafisira sheria anavyojua na kuzitekeleza kitamcost na kitasumbua watu akiwa rais, mara zaid ya 2 mahakama ndio imetoa nishai kwa kutengua maamuz yake ambayo yy alikua anadai anafata sheria nk

magufuli ni mtendaji mzuri nadhan kwa nafasi ya urais unaitaji caliber ya juu kidogo zaidi ya utendaji ambayo bwana magufuli hana nampenda kwa uchapa kazi wake lakini kwa urais hapana the maximum he can go up ni kua prime minister si zaid ya apo.

the ultimate glory i honestly fee should go to Dk. Harrison mwakyembe, he is composed, mchapa kazi na sheria anazijua vizur and he got the caliber kuwa mvumilivu!!!

sitta is simply lacking some know how and smartness, and he has already passed his sell by date!!!
 
Hivi CCM ndio wanatakiwa kutoa rais kila kipindi kikifika? Angalieni na pembeni kidogo tunaweza tukapata rais atakayetutoa!
 
Pasco tayari umeshahamia kwa magufuli mara hii, ile kambi yetu vipi tena kiongozi?
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha ha ha ha JUA LA UTOSI Zitto kapewa kamati ya mashirika ya umma akvuta mifedha NSSF na TANAPA akipewa wizara ya fedha atakausha hazina ya taifa.

My best combination ever:
1. Edward Lowasa (President)
2. Pombe Magufuli (PM)
3. ZZK(fedha)
4.Muhongo(energy)
5.Mwigulu (Viwanda)
6. Dr. Slaa (Minister of Propaganda)
 
Last edited by a moderator:
Rais ajae ni Wassira....
watu wa nje ya chama ndo hawajui,
refer to ndio mtu alieongoza kwa kura Kwenye CC,
jamaa ana ushawishi mkubwa sana ktk CCM Ili jina lake lipite,jamaa noma,watu tu hawajui....

Kulikuwa na mtu mwenye ushawishi CCM kama Malecela?Mbona Mkapa akaja mchinjia baharini tu..Sasa hivi siyo CCM peke yake yenye uwezo wa kutuchagulia Rais,kuna vyama vina nguvu ya kutoa Rais pia..CCM watakuwa wajinga sana kama wata risk kumsimamisha Wasira
 
magufuli ni mchapakazi lakini hafai kuwa kwa rais kwa sababu zifuatazo
1. intellectual arrogance - anadhan kua anajua kila kitu na akishaamua basi hakuna wazo jipya litakalokuja kuimprove alichoamua ni lazima kifanyike ivyo ivyo au hakuna wazo jipya litalomfanya abadili maamuz kwamba hicho anachokitaka kinawez kisiwe sahihi kwa mfano alivyokua anavunjia watu ovyo mpaka aliposhinwa ile kesi mahakamani wakat yy alikua anang'ang'ania kua anatimiza sheria.


the ultimate glory i honestly fee should go to Dk. Harrison mwakyembe, he is composed, mchapa kazi na sheria anazijua vizur and he got the caliber kuwa mvumilivu!!!

sitta is simply lacking some know how and smartness, and he has already passed his sell by date!!!

kuna mwenye intellectual arrogance Tanzania hii kumshinda Mwakyembe?
 
Tunahitaji rais kama magufuli,nchi hii imechoshwa na siasa na sasa inataka utendaji na vitu vionekane kwa mipango,watu wanafanya nchi kama idara ya zimamoto, nchi imekuwa na slogani nyingi,mara ari mpya,maisha bora,kilimo kwanza, big result now,mabilioni ya kikwete...magufuli hana upuuzi huo,yeye anafanya kazi japo ana mapungufu, mapungufu hayo yanafunikwa na utendaji,usimamiaji.KAMA HAMTAMPA WA MUUNGANO,NI BORA TANGANYIKA IRUDI TUTAMPA URAIS WA HUKU
Inaelekea unamjua sana!
Lakini, usisahau kuwa mtu aliyeaminika ccm kamwe hawezi kutuondoa hapa tulipo!

 
NIMEANZA KUHISI SITENDEWI HAKI HUMU.NAKUMBUKA MARA BAADA YA MKUTANO MKUU WA CCM MWAKA JUZI NILIWEKA UZI HAPA KUWA WAJUMBE WENGI WAMEAMINISHWA KUWA MGOMBEA NI MAGUFURI.ALIYEANZA KUWAAMINISHA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU NI JK MWENYEWE KWA NAMNA ALIVYOMFAGILIA MAGUFURI KATIKA MKUTANO ULe.
SaBABU AMBAZO WAJUMBE WALITOKA NAZO NI KWAMBA MAGUFURI HANA MAKUNDI,ANATOKA KTK ENEO LENYE WAPIGA KURA WENGI ZAIDI,KWA MACHO YA WATANZANIA WENGI BADO MWADILIFU NA MCHAPA KAZI.
IKUMBUKWE KUWA NI KATIKA MKUTANO HUO LOWASA ALIPAPASA SEHEMU NYETI ZA FAMILIA YA JK KUPITIA KWA BASHE ALIPOTAKA KUMZUIA MWANAFAMILIA YA JK,MEMBE,ASIPATE uNEC.
WAKATI HUO HATA MIMI NILIUNGA MKONO MAGUFURI ATEULIWE NA CCM KUGOMBEA URAIS KWA KUWA CCM NI KAMA MEISHIWA WATU WANAOFAA,BAADA YA KUIBUKA MWAKYEMBE NAONA MAGUFURI NI CHA MTOTO.MWAKYEMBE ANATOA MAAMUZI SAHIHI KABISA AKITUMIA VEMA ELIMU YAKE YA KISHERIA.
 
Msiwe kama wanawake wanaotongozeka kwa urahisi hasa wakiona chips, be thoughtful person, greater thinkers. Huyu mtu ana hulka ya kupenda masifa, alisema atalibomoa jengo la Tanesco ubungo kwa kujengwa kimakosa, kama yeye ni mtu asiye biased kwanini alifyata mkia na hadi leo wameliacha?huo ni mfano tu
 
Magufuli yuko Team-Mamvi au Team-Membe? Maana Urais wa Tanzania ni wa ubia, huwezi kusimama peke yako ugombee. Lazima ubebwe na mtandao wa kutoa rushwa kwa wapiga kura ambao unafadhiliwa na wafanyabiashara mafisadi.
 
Au wewe ni mhanga wa magufuli? maana jamaa ameumiza wengi,ukianzia waliojimilikisha magari ya umma,njoo kwa wezi wa viwanja, malizia na samaki alizozikamata na meli ikazama.
Kimsingi tunamhitaji heri alaumiwe kama nyerere lkn nchi isonge mbele

..yes, mimi ni mhanga wa Magufuli.

..kwa wizi wake na hujuma zake alipouza nyumba za serikali.

..Magufuli alidai zoezi hilo litailetea serikali mapesa mengi kiasi cha kuiwezesha kujenga nyumba nyingi zaidi.
 
Tafiti zilizofanywa na watanzania ni kuwa Tanzania na vijana wengi kwa sasa wanamuhitaji Rais msomi zaidi kama professor. Wengine walifikia hitimisho kuwa kwa sasa Watanzania wanamuhitaji Prof. Anna Tibaijuka aichukue nchi hii. anafaa ni mchapakazi, msomi mwenye uzoefu wa kimataifa.

Nchi haimuhitaji huyo mama, kuwa na uprofesa siyo kigezo cha kutuongoza, tunahitaji Rais mwanasayansi au Engineer lakini siyo Kawambwa, maana hao wengine wenye hadhi kama za ualimu na uchumi na uandishi wa habari wameshaongoza na bado tunalalmika, hivyo Magufuli ni mtu sahihi kabisa maana tunataka rais mwenye kutamka 1+1=2 siyo 1 na 1=11 ie atakayekwambia direct na siyo kuzunguka au kuwaonea aibu watendaji amabo kawateua yeye.
 
..yes, mimi ni mhanga wa Magufuli.

..kwa wizi wake na hujuma zake alipouza nyumba za serikali.

..Magufuli alidai zoezi hilo litailetea serikali mapesa mengi kiasi cha kuiwezesha kujenga nyumba nyingi zaidi.
Basi wewe pia ni mhanga wa mwalimu nyerere alikamata wahujumu uchumi,lkn na wale waliopata mali kwa jasho lao nao walifilisiwa,Pia wewe ni mhanga wa mh. Mwinyi kwani yalikamatwa mapesa mengi uwanja wa ndege na Mrema ikulu ikamnyamazisha na kipindi hicho ndo skandari za kusafirisha wanyama zilianzia, wewe pia ni mhanga wa mh, mkapa kwani uwekezaji na mikataba inayoitesa nchi hadi sasa ilianzia hapo,ya sasa unayajua sina haja ya kueleza ninachotaka kusema ni kwamba hakuna mtu perfect,tunalinganisha mapungufu yake na mema ya mtu mema yakizidi mabaya tunasema ni mwema hata kama kuna baadhi ya mabaya aliyoyatenda

Pia nikukumbushe tunachotafsiri kuwa ni kibaya ni nia ya mtendaji,alikuwa na nia gani alipotenda jambo hilo.Kuna wengine nia yao inakuwa nzuri lkn utekelezaji unazaa matokeo hasi hadi yule mtu anajutia,lkn wapo wengine tokea mwanzoni nia yao inakuwa ovu ili wapate maslahi.

Magufuri wakati anauza nyumba za serikali alikuwa anakomesha tabia ya watu kupitisha fedha nyingi kwa kisingizio cha ukarabati na hivyo kutumia hela nyingi kuliko thamani ya nyumba zenyewe,matokeo yake akajikuta ameuza na ardhi ya maeneo nyeti kama vile masaki.lAITI ANGEZIBOMOA NYUMBA ARDHI IKABAKI,INGETUMIWA KWA FAIDA.

Natamani watanzania tuwapime watu kwa uwezo wao binafsi bila kuwahusisha na vyama vyao,ukimhusisha magufuri na chama chake kweli utasema hafai,lkn akiwa mkuu wa nchi atakuwa msemaji mkuu na hivyo kutakuwepo mabadiliko.
swali langu ni je hicho chama kitamchagua awe mgombea urais? maana wengi ni wahanga wa magufuri.
ONGERA MAGUFURI KWA KAZI NZURI KAMA WATZ HAWAONI MUNGU ANAONA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom