Basi wewe pia ni mhanga wa mwalimu nyerere alikamata wahujumu uchumi,lkn na wale waliopata mali kwa jasho lao nao walifilisiwa,Pia wewe ni mhanga wa mh. Mwinyi kwani yalikamatwa mapesa mengi uwanja wa ndege na Mrema ikulu ikamnyamazisha na kipindi hicho ndo skandari za kusafirisha wanyama zilianzia, wewe pia ni mhanga wa mh, mkapa kwani uwekezaji na mikataba inayoitesa nchi hadi sasa ilianzia hapo,ya sasa unayajua sina haja ya kueleza ninachotaka kusema ni kwamba hakuna mtu perfect,tunalinganisha mapungufu yake na mema ya mtu mema yakizidi mabaya tunasema ni mwema hata kama kuna baadhi ya mabaya aliyoyatenda
Pia nikukumbushe tunachotafsiri kuwa ni kibaya ni nia ya mtendaji,alikuwa na nia gani alipotenda jambo hilo.Kuna wengine nia yao inakuwa nzuri lkn utekelezaji unazaa matokeo hasi hadi yule mtu anajutia,lkn wapo wengine tokea mwanzoni nia yao inakuwa ovu ili wapate maslahi.
Magufuri wakati anauza nyumba za serikali alikuwa anakomesha tabia ya watu kupitisha fedha nyingi kwa kisingizio cha ukarabati na hivyo kutumia hela nyingi kuliko thamani ya nyumba zenyewe,matokeo yake akajikuta ameuza na ardhi ya maeneo nyeti kama vile masaki.lAITI ANGEZIBOMOA NYUMBA ARDHI IKABAKI,INGETUMIWA KWA FAIDA.
Natamani watanzania tuwapime watu kwa uwezo wao binafsi bila kuwahusisha na vyama vyao,ukimhusisha magufuri na chama chake kweli utasema hafai,lkn akiwa mkuu wa nchi atakuwa msemaji mkuu na hivyo kutakuwepo mabadiliko.
swali langu ni je hicho chama kitamchagua awe mgombea urais? maana wengi ni wahanga wa magufuri.
ONGERA MAGUFURI KWA KAZI NZURI KAMA WATZ HAWAONI MUNGU ANAONA.
Tunachosahau tu ni kwamba utake usitake unaposhika ile nafasi kuna tabia baadhi za mtu hubadilika sababu lile ni jukumu zito sana. Mara nyingi huwa kuna mazuri na mabaya ambayo mtu huweza kuwa nayo pindi tu anapopata ile nafasi.
Iwapo vetting ya viongozi ingefanywa na JF asingepita mtu labda aje malaika!
Iwapo vetting ya viongozi ingefanywa na JF asingepita mtu labda aje malaika!
mkuu,wewe binafsi unadhani nani angeweza kuwa Rais bora kwa Tanzania baada ya Kikwete kumaliza muda wake kati ya hawa wagombea wanaotajwa au hata wasiotajwa?
..kwanza tunatakiwa tubainishe tunahitaji kiongozi wa aina gani.
..nini malengo yetu na vipaumbele vyetu ktk miaka 5, 10, 20, ijayo.
Labda mkuu wewe tupe pendekezo lako la rais mtarajiwa 2015,unaweza ukawa unatumia sheria ya dawa ya moto ni moto,ikiwa na maana ya mahali palipoharibika weka aliyeharibika. Kama unatumia sheria hii basi Dr Magufuri hafai...hatujasema tunataka Malaika.
..lakini pamoja na hayo hatuhitaji mtu ambaye tunajua ameshatutia hasara ya matrilioni kutokana na maamuzi yake.
..baya zaidi Dr.Magufuli haonekani kujutia uamuzi wake, na kufanya juhudi zozote zile kurekebisha makosa yake.
cc tz2015
NgumiJiwe, tz2015,mkuu mahitaji yetu ni mengi na yanajulikana,na hata wewe unayajua.Kwa kifupi sana,binafsi ningetamani tupate mtu wa kututoa hapa tulipo na kutupeleka pazuri zaidi kimaendeleo ya kijamii,kiuchumi na kisiasa kwa miaka mitano kwa kuanzia ie 2015-2020..kati ya hao wanaotajwa na wengine wasiotajwa,unadhani nani anafaa mkuu?naomba unitajie jina lake
Nafanya tuu rejea!.Wanabodi,
Leo nimekutana na rafiki yangu wa siku nyingi, ambaye ni mtu wa kuaminika na ni kada wa Chama cha Mapinduzi-CCM, akanieleza seriously habari za kushtusha kidogo ambazo mimi pia zimenihuzunisha, kunisikitisha na kunisononesha!, kuwa eti imeishaamuliwa mgombea wa urais wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi-CCM ni Mhe. John Pombe Magufuli!.
Kilichonistua, kunihuzunisha, kunisikitisha na kunisononesha, ni the reasons behind alizonitajia ambazo ndizo zimepelekea CCM kuamua why ni lazima awe Magufuli tuu, and no one else!.
Kwa vile sababu hizo alizonitajia, baadhi ni justifiable na nyingine sio tuu ni unjustifiable!, bali hazikubaliki kabisa katika Tanzania ya leo!. Naomba kwa sasa nisizitaje kwanza, kwa sababu habari zenyewe nimezisikia from a single source, nahitaji kwanza kufanya collaborative verification na kupata attribution ili nijiridhishe kuwa ni za kweli na kuthibitisha kuwa hivyo ndivyo CCM inavyoweza kufikia maamuzi based on hayo niliyoyasikia!, then nitaziweka hadharani hizo sababu za CCM on Why ni Magufuli!.
Kwa kawaida sisi waandishi, ukipata taarifa kama hii, huwa inaitwa "news tip", haukimbilii kuiandika mbio mbio mpaka kwanza uifanyie verification kuthibitisha ukweli wa taarifa yenyewe, lakini kwa vile sasa tunaishi kwenye "the world of information age", nimeamua kuileta hii "news tip" humu jf, hivi hivi ikiwa kwenye hatua ya "tip" kabla hata ya verification, ili wewe kama mwana jf, uipate ile advantage ya jf, "be the first to know!", hivyo nawaombeni tuu sasa mkae mkijua, "Mgombea wa CCM 2015 ni John Pombe Magufuli!"
Nikiisha "confirm" neno "tetesi" litaondolewa na kuwa replaced na neno "confirmed!", na nitaziweka hizo sababu ila sasa ndio zijadiliwe!, na nawahakikishia wale wote wenye mapenzi mema na taifa hili, mkizisikia hizo sababu za CCM!, na nyinyi pia zitawashtua, kuwahuzunisha, kuwasikitisha na kuwasononesha!. Naomba nisiwatajie jina la huyo source wangu chini ya kinga ya kihabari inayoitwa "The Confidentiality of the source".
NB. Sio kila thread ni lazima ichangiwe, saa nyingine itoshe kujisomea tuu na kujipitia bila kuchangia chochote!. Hii ni just a news tip, kwa vile nimewaahidi naifanyia verification kuithibitisha, nawaombeni msiniulize swali lolote at this stage, kwa sababu sitajibu chochote!, and if possible nawashauri na nyingi msome FYE only na sio lazime mchangie kwa sasa na badala yake mvute subira kusubiria verification.
Sababu ya kuiwahisha humu jf kabla ya verification ni ili tuu wewe kama mwana jf to be the first to know!. Information is power!, if you are the first to know, then you'll have the powers to make good things happen or not to happen if they are bad things!.
Asante.
Pasco.
Lowassa ndiye rais ajaye!
Magufuli uraisi hawezi kabisa,kiboko yake LOWASA TU,LOWASA NDO KILA KITU.
Lowasa tu hata kama mi sio CCM
Lowassa ndiye rais ajaye!
Nafanya tuu rejea!.
Pasco