Elections 2015 Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Wanabodi,

Leo siku ya Machi 17 ndio siku Taifa tulipotangaziwa kifo cha Shujaa wetu JPM, hivyo katika kumkumbuka, na kumuenzi, mnaonaje tukijikumbusha baadhi ya mabandiko ambayo tulimshauri JPM na ushauri huo ukafanyiwa kazi, kwa kutaja Bandiko, ulishauri nini, na nini kilikuja kufanyika kwa ushauri huo, na jee kulisaidia JPM?. Kulisaidia nini?.

Kwa vile JPM alikuwa ni mbabe kwa kufanya baadhi ya mambo kibabe, hadi kutafsiriwa ni dikiteta, hivyo baadhi ya ushauri kwa JPM pia ulitolewa kibabe kwa kumpiga Spana za kutosha, ila tukubali tukatae, Spana za JF zilimsaidia sana JPM na kulisaidia taifa.

Kumuenzi JPM, naomba tujikumbushe baadhi ya mabandiko, tuliwahi kushauri nini kwa kuandika nini na kutoa ushauri wa nini kifanyike, na kufuatia ushauri huo, nini kilifanyika na jee kilimsaidia JPM?kilimsaidia kivipi?. Jee kililisaidia taifa?, kililisaidia kivipi?.
  1. Naanza na bandiko hili la August 2014 kutangaza ujio wa JPM nikieleza kwanini ni JPM Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli bandiko hili liliwaandaa Watanzania kwa 2015 with what to expect kwa JPM, hivyo ilipokuja kutokea kweli, it was not a surprise.
  2. Inaendelea....

Na mwisho kwa vile sasa Samia ndie Rais wetu, JF tunapaswa kuendelea kutimiza wajibu wetu kwa kumsaidia Samia, kwa vile JPM alikuwa ni rais mbabe vivyo hivyo ushauri ulitolewa kibabe, lakini Samia no Mtaratibu, mstaarabu, jee licha ya utaribu na ustaarabu, Mama Nate tumpige Spana kama za JPM? au twende naye taratibu kama alivyo, kwa Mama iwe ni kumkuna tuu, na tusimpare kama alivyo shauri mwenyewe, kuwa ukinikuna vizuri nitakukuna ila ukinipara, nitakuparua?

Mabandiko mengi ya kuwakumbuka marehemu huishia kwa RIP kumuomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi kwavile wanakuwa hawajui marehemu yuko wapi,, lakini mimi kwa vile tayari nimeisha kulishwa JPM yuko wapi Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani bado kuna haja ya kuendelea kumuomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi huku tayari najua yuko peponi?.

Pumzika Magufuli Pumzika!, Tutakukumbuka Daima!.
Paskali!.
 
Acha unafiq we mzee😅mbona huleti sred zamautabir kwa Samia? vp walokuwa wanakupa info wametolewa kwenye circle?😅😅
 
Ila Pascal Mayalla .We Mzee Ni Mnafiki Sana.

Na Nilichogundua Unaishi kwa kwenda na upepo na siyo Mkweli Ata Kidogo.

Maneno Yako Ya Mwanzo Katika Uhandishi huu Ndiyo Yaliyokuwa Yamebeba Ukweli wa Magufuli.

Lkn Ulipokuja Kugeuka Fasta .Daaaahh???!!
 
paschal,
Usiku huu wa manane hapa Tanzania,nimekutana na kupitia bandiko lako la miaka hiyo na ,japo unaitwa 'Mzee wa njaa', with due respect,POKEA MAUA YAKO,Kwani ulichoandika,ndo kilichotimia.
Hivyo,Nina sababu ya kuamini hata Hilo bandiko lako lingine kuwa Rais ajaye 2025 ni mwanamume litatimia ,ukitafakari matukio mbalimbali likiwemo la DPW
 
.....akanieleza seriously habari za kushtusha kidogo ambazo mimi zimenitisha, zimenisikitisha, kunihuzunisha, kuniogopesha, kunisononesha na kuninyongonyeza!....
Ungezitaja hizo sababu watanzania wengi tusingenyong'onyea ...!

Mkuu Kwa kipande Hiki cha uzi wako nakuongeza kwenye orodha ya walaumiwa mpaka hapo nitakapojiridhisha kuwa haustaili kulaumiwa.
 
Simba mwovu akitaka kula nyama anajinyenyekesha.

Bajeti haandiki yeye anasoma tu, hana utaalam wa kuandika bajeti.

Kuna watu wenye ajira hiyo ya kuandika na kuandaa bajeti.

Mramba aliwahi kushindwa kusoma tarakimu za jumla ya bajeti ya wizara yake ya viwanda na biashara akaishia kumuomba Mhe. Spika kwamba tarakimu hizo ziingie kwenye Hansard kama zilivyoandikwa na siyo kama anavyozikosea kusoma.

Kusoma bajeti hata chizi aliyefundishwa 3Ks (KKK) anaweza kusoma.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…