Mgombea wa CHADEMA jimbo la Chalinze awekewa Pingamizi

pinguli

Senior Member
Oct 12, 2010
122
14
Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia (CHADEMA) amewekewa pingamizi na Chama Cha wananchi CUF kutokana na kutotimiza mashariti katika fomu yake ya Ugombea aliyoichukua tume ya Uchaguzi (NEC).

Viongozi wa CUF jimboni humo wamedai kuwa kulingana na sheria na kanuni za NEC mgombea anatakiwa kuwa na wadhamini wasiopungua 25 ambao ni wapiga kura halali wa jimbo hilo. Ambapo imegundulika mgombea wa Chadema amepeleka fomu yake ikiwa na wadhamini 28 ambapo imefahamika kuwa miongoni mwao 7 sio wapiga kura halali wa jimbo hilo kwa maana hawamo katika orodha ndani ya Daftari la wapiga kura wa jimbo hilo la Chalinze hivyo kubaki na wadhamini 21 hivyo kutotimiza kanuni.

Tayari viongozi hao wameshawasilisha pingamizi lao kwenye ofisi ya NEC ya wilaya na wamepanga kufanya press Conference kuelezea hatua yao hiyo waliyoichukua dhidi ya mgombea wa Chadema.

TAARIFA YA PINGAMIZI LA MGOMBEA WA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE .

FABIAN LEONARD SKAUKI – MGOMBEA CHAMA CHA WANANCHI –CUF

DHIDI YA

MATHAYO MANG'UNDA TORONGEY – MGOMBEA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO -CHADEMA

13.03.2014

Mimi FABIAN L. SKAUKI, mgombea ubunge wa uchaguzi mdogo jimbo la CHALINZE kwa Ticket ya THE CIVIC UNITED FRONT (CUF) ninamwekea Pingamizi mgombea wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwamba amepoteza sifa za kuwa mgombea kwa sababu zifuatazo.

1. Ndugu MATHAYO. M. TORONGEY amejaza Taarifa za uongo kwenye Fomu yake kwamba kazi anayoifanya ni BIASHARA. Sio kweli, kwa sababu hajaweka vielelezo vya yeye kufanya hiyo kazi. Hajulikani anafanya kazi gani.

2. Ndugu MATHAYO .M. TORONGEY amejaza katika fomu kwamba anajua kusoma na kuandika Kiswahili na kiingereza. Taarifa hizi ni za uongo, mgombea huyu hajui kusoma wala kuandika Kiswahili wala kiingereza, na kwamba amedanganya na amepoteza sifa za kuwa mgombea.

3. Ndugu MATHAYO .M.TORONGEY amedanganya kwa kughushi/kufoji sahihi za wadhamini,ambao amewaorodhesha kwenye fomu ya kuomba kuthibitishwa kuwa mgombea. Ambapo katika fomu hizo wadhamini wote sahihi zao zimefojiwa na hazifanani na zile zilizokuwepo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kwamba sahihi zote hizi zimesainiwa na mtu mmoja ambaye sio muhusika. Hivyo anapoteza sifa ya kuendelea kuwa mgombea.

4. Ndugu MATHAYO.M.TORONGEY ameshindwa kutimiza mahitaji ya kisheria ya kuwa na wadhamini wasiopungua 25, badala yake amedhaminiwa na wadhamini 28 ambao kati yao wadhamini 7 sio wapiga kura halali wa jimbo la CHALINZE, na kwamba Taarifa zao na namba zilizojazwa hazifanani.

Hivyo anabakiwa na wadhamini halali 21 ambao kisheria hawatoshi kutimiza matakwa ya kisheria


Majina ya wadhamini hao ambao hawakidhi matakwa ya kisheria na namba zao ni

JINA LA MDHAMINI na NAMBA YA KADI KURA

1. HABIBU ALLY SAIDI - 16886275
2. MOHAMMED RAMADHANI - 30376567
3. ABDULKADIR ALLY - 49264905
4. SHABANI SULEYMAN - 16984045
5. JUMA MRISHO - 48759563
6. RAJABU ALLY - 16872368
7. MANENO MIRAJI - 16872059

Wananchi wenye namba na majina hayo hapo juu waliojazwa kama wadhamini kuanzia namba 1 hadi 7 kwenye fomu yake hawana sifa za kupiga kura kwenye maeneo ambayo wamejazwa wanatokea.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba idadi halali ya wadhamini wanaobaki ukiwaondoa hao saba watabaki 21, hawakizi vigezo vya kuwa wadhamini.

5. Ndugu MATHAYO.M.TORONGEY amedanganya Uraia wake, na kwamba yeye si Mtanzania wa kuzaliwa ndio maana hana vielelezo halali vinavyohusu uraia wake. Hivyo anakosa sifa ya kuwa mgombea.

Hivyo ninaomba Tume ya Uchaguzi kutengua uteuzi wa mgombea wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ndugu MATHAYO.M.TORONGEY kwa kuwa anakosa sifa za yeye kuendelea kuwa mgombea.

Wako katika ujenzi wa Taifa

FABIAN LEONARD SKAUKI

……………………………………………………..

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE.

THE CIVIC UNITED FRONT
 
Hao siyo CUF, bali ni Ridhiwani na chama chake wamepitia mlango wa nyuma kwa kuhofia kushindwa.
 
Nasikia pia ana uraia wa uingereza...

Uliambiwa na Dr A. Paurine kuwa dozi ni kidonge kwa siku wewe unakunywa mara tatu.......haya ndio madhara yake!

a0c4824059f67abc18188a3627e3e875.jpg
 
Hao siyo CUF, bali ni Ridhiwani na chama chake wamepitia mlango wa nyuma kwa kuhofia kushindwa.

Sitaki kuamini kama kweli Ridhiwani Bin Jakaya Halfan Mrisho Kikwete anahofia kweli eti kushindwa na MATHAYO OLE TORONGEI katika jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo katika mkoa wa Pwani. Wangekuwa wanagombea Arumeru hapo sawa.
 
Hawa cafu ni wachumia tumbo wamekubali kulamba miguu ya riz1,mtoto wa dhaifu la magogoni.
Dah! Ama kweli hawa cuf ni c.c .m b!
 
Back
Top Bottom