Mgombea wa CCM kwenda Kupigania Maendeleo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea wa CCM kwenda Kupigania Maendeleo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Anko Sam, Mar 26, 2012.

 1. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nimetafakari kauli zinazotolewa na viongozi wa CCM kwenye kampeni za chaguzi ndogo za Ubunge nimegundua hawana sera na huwenda wanatumia masaburi kufikiri, mfano:-

  "....Mchagueni sioi akapiganie maendeleo yenu....!"
  "....Mchagueni mgombea wa CCM akawaletee maendeleo..."
  "....Kama suruali nyeusi imetoboka makalioni usiweke kilaka cheupe...."
  nk!

  Inakuwaje mbunge wa chama tawala akapiganie..., wakati serikali yake inayotawala inatekeleza ilani ya chama ya uchaguzi? Ina maana hakuna mipango inayofuatwa bali mpiga kelele bungeni ndiye anayetekelezewa? Jambo hili nalo siyo kweli maana akina Kilango ni wapiga kelele wazuri lakini kwake bado ni shida tu! Hii inaonyesha serikali haipangilii mambo-inafanya mambo kwa kukurupuka!

  Wapiga debe wa CCM wanasahau kuwa serikali ya chama chao imekaa madarakani zaidi ya miaka 50 lakini hakuna maendeleo ya maana ukilinganisha na lasilimali za nchi, kwa hiyo kama baba yake sioi ameshindwa na alikuwa kwenye naibu mawaziri, je yeye mtoto ataweza akiwa mbunge wa kawaida? Wanadanganya watu!

  Mifano mingine kwa mwenye akili ni aibu hata kuitamka, nijuavyo mimi kwa mtanzania wa sasa, suruali ikitoboka hakuna haja ya kuweka kilaka, ni kununua nyingine japo iwe ya mtumba na kuitupilia mbali iliyotoboka. hakuna haja ya kuweka viraka. CCM imetoboka makalioni, itupwe mbali jalalani!

  Mbunge wa Chama tawala hapaswi kupigania maendeleokama serikali yao ingekuwa makini, ni ku-submit proposal na wakatekelezewa!

  Wanaoweza kupigania maendeleo ni CDM kama chama kikuu cha upinzani, na kazi ya kutetea Taifa na wananchi kwa ujumla walioifanya ndani ya muda huu mfupi, imeonekana pamoja na uchache wao bungeni!

  ARUMERU MSIDANGANYIKE chagueni PEOPLEEES POWER!
   
Loading...