Mgombea wa CCM ajinadi ana nguvu za kiume

Kijogoodi

JF-Expert Member
Mar 29, 2021
1,363
2,372
Dodoma. Mgombea wa nafasi ya mjumbe wa halmashauri ya CCM wilaya ya Dodoma amewavunja mbavu wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya baada ya kuwaomba wamchague kwa sababu ana nguvu za kiume.

Mgombe huyo, Chris Madaha ametoa kauli hiyo leo Oktoba Mosi, 2022 wakati akiomba kura mbele ya wajumbe 1,344 walioshiriki mkutano huo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.

Madaha ambaye aliomba kura kupitia kundi la vijana, amesema amekamilika kwa sehemu zote na ana nguvu za aina mbili ambazo ni za kimwili na kiume.

“Ndugu wajumbe, mimi nimepewa namba mbili ambayo ni namba ya ushindi, lakini nina nguvu za aina mbili ambazo ni nguvu za kimwili na kiume, nipeni kura zetu,” amesema Madaha.

Kauli hiyo ilisababisha vicheko vya wajumbe na kusababisha zogo lakini waliponyamaza aliyarudia maneno yake mara mbili.

Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo, Jabir Shekimweri alimuomba mgombea kipaza sauti na kumtaka akapumzike wakati watu wakiendelea kucheka.

Uchaguzi wa CCM wilaya ulihusisha nafasi ya mwenyekiti, wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa, mkutano wa mkoa na wajumbe wa halmashauri kupitia makundi ya wazazi, vijana na wanawake.
 
Apewe kura huyo
 
tuna wagonjwa wengi sana wenye matatizo ya akili tupo nao mitaani na kuna hatar wengine tukawapa uongozi watuongoze
 
Kitaalam yupo sahihi kwani alikuwa anajibu swali lisiloulizwa Kwa sauti juu ya urijali wake na kawapa jibu wajumbe wakalisambaze Kwa wauliza swali!
 
Anajinadi ana nguvu za kiume kwamba atawatoa nyegge wapiga kura au nguvu za kazi gani kwenye maslahi ya Taifa
 
Back
Top Bottom