Mgombea W. Malecela aendelee kufundwa!

Kibunago

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
300
122
Ukiachilia mbali uwezo wa kusimamia / kutekeleza ahadi, kuna Wapiga kura wengi ambao wanamkubali Mgombea au Kiongozi kutokana na jinsi anavyowasilisha hoja!

Kwa vile anasema amezaliwa hapa JF- Kisiasa ngoja tuendelee kumfunda namna ya kujiwasilisha ipaswavyo!

Ufunguo:


  • § Maandishi ya Willy
  • § Maandishi yangu

Wakuu wote JF,
Mbadala: Ungeweza kuandika,
“Ndg. Wana-JF” au “Wana- JF”

- Kwanza ninaomba kwa unyenyekevu sana kuwashukuru Kamati Kuu ya CCM na Mwenyekiti wake Rais, Dr. Jakaya M. Kikwete kwa uamuzi wao mzito na wa pamoja wa kunipendekeza kugombea ubunge wa EAC, ninasema ninawashukuru sana kutoka moyoni mwangu kwa kunipa nafasi hiii.

I. Mwenyekiti ni sehemu ya Kamati Kuu hivyo kuanza kutamka Kamati Kuu na kisha kutumia kiunganishi ‘na’ ni kujirudia. Pengine ulitaka kutumia maneno “ hususan, Mwenyekiti” (lakini lazima uelewe kuwa hiyo ina maana kuwa yeye alikuwa na kura ya turufu au msukumo wake ndio ulikuwa mkubwa kuliko wa wengine; jambo ambalo halina mashiko mbele ya safari!).

Mbadala: Kitekinikali, ungeweza kuandika,
“ ........ kumshukuru Mwenyekiti na Wajumbe (wake) wa Kamati Kuu......”

II. Umetumia vitambulisho vya Wadhifa & Sifa ambavyo si sahihi katika mukhtadha huu wa Kikao cha Chama. Huna haja ya kumwita Rais hapo (ingawa kweli ni Rais), huna haja ya kumwita Dr. Na kama ni lazima, basi itifaki izingatiwe, uandike,. "Dr.h.c." au "Dr.(h.c.)"


- Ninawashukuru sana JF, wanachama wote hapa ndio nyumbani kwangu ndipo nilipokarabatiwa kisiasa na kufikia uwezo nilio nao sasa, I love JF this is my home politically nilizaliwa hapa,

Mbadala: Ungeweza kuandika,
“Nawashukuru sana Wanachama wote wa JF maana hapa ndipo nimeendelea kukarabatiwa Kisiasa na pia katika nyanja mbalimbali. Hakika, JF imendelea kuchochea hisia na ndoto zangu za kuwa Mwanasiasa- Kiongozi bora.”

NA KATIKA MIJADALA HAPA TUMEPITIA MENGI SANA NINAOMBA KUSEMA TENA NINAWAOMBA RADHI WOTE NILIOWAKOSEA KWA KUWARUSHIA MANENO YASIYOFAA KATIKA MIJADALA, .........NIA NA MADHUMUNI SIKU ZOTE NI TAIFA KWANZA.

Unaibua swali lisilo la lazima. Kwa nini uombe radhi leo (sasa). Ni bayana kuwa Binadamu hapendi kutoa msamaha katika mazingira yanayoashiria muda wa mwombaji kuhitaji kitu fulani toka kwake!

Mbadala: ungeweza kusema,
“Hapa JF tunajadili hoja mbalimbali. Tuendelee kuwa wakweli na wawazi huku tukitumia lugha inayostahili kwa mujibu wa kanuni kuu za JF za ushiriki katika kutoa maoni yetu. Aidha tuendelee kuombana radhi pale tunapo sababisha usumbufu au maumivu kwa makusudi au pasipo kutarajia kwa mapungufu yetu ya kibinadamu. Siku zote, nia na madhumuni yawe kwanza, kuweka mbele Taifa letu, mengine yafuate

SIWEZI KUSEMA NILIKUWA NIMELEWA KWA SABABU SIJAWAHI KUNYWA POMBE WALA KUVUTA SIGARA KATIKA MAISHA YANGU, KWA HIYO NINASEMA YALIKUWA NI MAPUNGUFU YANGU TU KAMA BIN-ADAAM, NINAOMBA MNISAMEHE SANA,


Swali lingine linaibuliwa tena, kwamba “Je, ungekuwa unakunywa pombe, ungetumia hicho kama kisingizio?” Zaidi ya yote sioni jinsi uvutaji wa sigara unahusiana (kisayansi) na matamshi au maandiko yasiyostahili, isipokuwa kama bila kujitambua ulikuwa unataka kutuelezea sifa (endapo ni sifa) zako kuwa wewe Mgombea, huywi pombe wala huvuti sigara.
Mbadala: Kutoyaadika haya maneno.


- AGAIN, jamani nawaomba twende mbele yaliyopita sio ndwele twende kwa mbele sasa tumalizie ngwe ya mwisho, JF idumu na MBARIKIWE WOTE NDUGU ZANGU!


Utata mwingine; ni yapi hayo yaliyopita yanayotakiwa kuachwa? Hapa kuna hoja kibao za siku za nyuma sana ambazo kamwe haziwezi kuachwa maana ama hazijajibiwa au hazijapata ufumbuzi kama vile matatizo ya Ufisadi nchini, Kero za Muungano wetu Tanzania, Hoja ya Mgombea Binafsi, Serikali kutakiwa kupunguza gharama kwa kuwa na Wizara, Mikoa / Wilaya, Wabunge wachache na uwezekano wa kuunganisha baadhi ya nyadhifa (Mikoani & Wilayani) n.k na JF is where people dare to talk openly! (kama unavyoamnini). Na ngwe ya mwisho ni ipi, je unamaanisha, uchaguzi wa nafasi unyogombea Bungeni au nini?

Mbadala: Ungeweza kuandika,
Ikiwa wewe ni mmoja wa wapiga kura au una ndugu / rafiki atakayekuwa mpiga kura katika ngwe iliyobakia Bungeni, ninayo heshima na taadhima kuwaombeni kura ili yumkini niweze kuwawakilisha ipaswavyo; ahadi ninayoitoa kwenu.
Pamoja na wengine wote, daima, tuzidi kuombeana yaliyo mema.

- MUCH RESPECT!:cool2:

William.


Hongera sana Willy, nakutakia kila la kheri. Hatuna haja ya kuanza kuogopa sijui kundi la nani n.k hiyo ni phobia tu, kitakacho kuinua ni uwezo wako ikiwa ni pamoja na jinsi unavyo jiwasilisha (presenting yourself) na huu ni mfano mmoja tu wa kukusaidia. Tafadhali uwe makini sana unapotaka kuongea kwenye kadamnasi.

Bado kitambo kidogo, pengine tutakuwa pamoja!:hand:
 
Ninachomshangaa W.Malecela ni kitendo cha kubadili signatures na yale maneno ya kitoto aliyokuwa anayaweka kila baada ya post yake...!
Huenda anadhani kuondoa maneno yale kutatufanya tumuone keshakuwa na busara na utuuzima wa kutosha kumwamini kama mwakilishi wa level ya crossboarder!
Ref:Le Mutuz, Baharia, @NYC
 
Acheni mambo ya ajabu nyie Magamba! Tabia ya Kurithishana uongozi na kulea ufisadi mpaka lini?
 
Huyu Jamaa simuamini kabisa.
Muda si mrefu Jioni hii nimemkuta kwenye Mgahawa mmoja mtaa wa India katika mazungumzo yake hakuna kabisa ile radha ya uongozi, haipo kabisa yaani ni mtu fulani hivi ambaye kaiukumbuka Siasa ukubwani yaani sio kabisa material ya kurepresent kundi la watu katika misingi ya Kisiasa.

Huyu alitakiwa aanzishe chama cha mabaaria wastaafu wawe wanakwenda kucheza mpira leaders baada ya apo wanaendeleza unywaji basi.
 
sitaki kuamini unataka kutuaminisha kuwa eti william ni kiazi kiasi cha kuhitaji kufundwa kwa vitu ambavyo ni so basic kama hivi.
kuna mawili......you dislike the guy for some reason or xxxxxxxx (no, i will let this one fly by!)
 
Gamba ni gamba tu; unachukua ubungi ili ukatukane watu; maana mbunge wenu ndio anatoa matusi ya nguoni ; sina neno zuri ila nawachukia sana Magamba (CCM)
 
Hapa sio sehemu ya kufundishia magamba hebu nendeni jukwaa lingine mkafanyie hiyo misifa yenu

Pp mpaka leo hujajua kuwa hili si jukwaa la chama fulani. Nitarudi nikufunde nawe!
 
sitaki kuamini unataka kutuaminisha kuwa eti william ni kiazi kiasi cha kuhitaji kufundwa kwa vitu ambavyo ni so basic kama hivi.
kuna mawili......you dislike the guy for some reason or xxxxxxxx (no, i will let this one fly by!)

At times, common sense is very uncommon! I like him but I dislike those common mistakes! Nimempa hongera na nimemtakia kila la kheri. Kama ulifikiri hivyo ni vitu basic mbona wewe hukuwa umeona tatizo lolote alivyoji present hapa katika tukio hili, akishukuru kuteuliwa na zaidi akiomba kura ( indirectly).
 
Mimi silipendi hili jamaa kwani halina hoja, tupo nalo huko kwenye makundi mengine yakijamii linapost maisha yake binafsi na picha linazo piga na wakuu wa magamba.hata hivyo hivi huu uongozi ni kipaji cha familia zenu tu? ukitaka ubunge nenda ukashindane na Lusinde. mimi siwataki wote wanao tumia majina ya wazazi wao.hivi @williamu unasifa yoyote ya ziada ukiachana na kuwa sehemu ya familia ya Tinga tinga lililo angushwa na Bajaji? Laaa baharia, Laa familia, Laaa Mikocheni, na anacho niuzi ni kule kuajili tumagamba tudogo tudogo na tuchache kwa ajili ya kumpamba ***** wewe.
 
hakuna mwanamme ukamkuta na cheni kubwa kama mnyororo na mipete kama nati ya treni ukategemea kuongoza nchi.

ingekuwa hip hop anafaa sana, ila uongozi hell no. Mtu unajiita majina ya kipapaa unata kumuongoza nani?

Ni aina ya mtu ukimwambia Manyara kuna njaa, ana kuuliza kwani friji zao hazina juisi na keki.

Afu hayuko 'real', eti unachaguliwa kugombea ndo unaanza kuwaambia watu 'pole au nawapendeni au nisamaheni'
unawaziba mdomo kitu gani??

Unadhani viongozi wengine hawana mapungufu kama binadamu? Na bado watu wanawapenda sababu wana quality za uongozi
Nothing personal, but my sincere obervations.

He is not a leader and he will never be.

Na 2005, watu walichemka na smile wakapiga KuRa.
 
Back
Top Bottom