Mgombea Urais UKAWA atatetea ILANI ipi?

Mgombea Urais UKAWA atatetea ILANI ipi?

Members wa JF, sina tatizo na mchakato unaoendelea kwenye vyama vyote vya siasa kwa sasa hapa nchini. Nafahamu na ndivyo kwamba UKAWA siyo chama kilichosajiliwa na hivyo katika kuelekea uchaguzi mkuu ujao, umoja huo hauna ILANI ya pamoja.
Naomba tu ili kuweka kumbukumbu vizuri nifahamishwe bayana ni ilani ipi mgombea wa umoja huo ataenda kuinadi na kuitetea.
Nawasilisha

..wanatengeneza ilani moja ya ukawa.
 
Niliwasikia pale Jangwani Mbowe, Prof Lipumba, Mbatia na Makaidi wakisema kwamba WATAHUISHA Ilani za vyama vyao na kupata ILANI MOJA YA UKAWA.
 
Akili mbovu ninyi, kama watu wmeungana si lazima watekeleze kile walicho kubaliana? haitakuwa muungano kama yatatekelezwa ya chama kimoja, tumieni akili muda mwingine
Mkuu nikupongeze sana kwa kuelewa nalenga nini na nadhani hiki ndo kinachosumbua sana umoja huo. Nategemea hawa wanaojinasibu kuunga mkono umoja huo wausaidie kwa dhati vinginevyo itakuwa taabu kwelikweli huko mbeleni.
 
Ilani isiwe tabu sana.

Kwa nchi maskini kama Tanzania ilani ipo wazi.
Ondoa rushwa
Piga vita umaskini,
Kusanya kodi,
Wezesha wakulima wadogo,
Vutia wawekezaji kwenye viwanda vya usindikaji (mazao ya kilimo na mifugo),
Vutia uwekezaji kwenye viwanda kama vya nguo tusiuze pamba ghafi nje ya nchi.

Vitu vyote hapo juu vitaleta pesa kwa watu binafsi na nchi, then

Wekeza kwenye elimu, afya, miundombinu

Nyingine zote mbwembwe tu.

Nazisoma hapa ilani za vyama vya siasa hasa vyenye uwakilishi bungeni picha ninayopata ni mbali kabisa na mtazamo wako.
Kwa ujumla siyo rahisi kama unavyofikiria.
 
Nazisoma hapa ilani za vyama vya siasa hasa vyenye uwakilishi bungeni picha ninayopata ni mbali kabisa na mtazamo wako.
Kwa ujumla siyo rahisi kama unavyofikiria.

Kuna vitu wanaweka (vyama vyote) ambavyo wakati mwingine ni kuvutia wapiga kura tu. Unakumbuka ya CCM na mahakama ya kadhi? Ni vitu kama hivyo. Wao wenyewe hawaamini katika hayo.

Mwisho wa siku ni ilani sio katiba!
 
Mkuu nikupongeze sana kwa kuelewa nalenga nini na nadhani hiki ndo kinachosumbua sana umoja huo. Nategemea hawa wanaojinasibu kuunga mkono umoja huo wausaidie kwa dhati vinginevyo itakuwa taabu kwelikweli huko mbeleni.

Nafikiri dunia yako imeshia Tanzania?

Have you ever asked this STD I kids question kwamba Uhuru Kenyata ya Jubilee Kenya anatetea/tekeleza ilani ya chama gani? Or the recent Nigerian president elect Mamadu Buhari anatetea/tekeleza Ilani ya chama gani?
 
Ungejibu swali tu kuliko kuruka ruka ili tuende sambamba humu ndani
 
Kuna vitu wanaweka (vyama vyote) ambavyo wakati mwingine ni kuvutia wapiga kura tu. Unakumbuka ya CCM na mahakama ya kadhi? Ni vitu kama hivyo. Wao wenyewe hawaamini katika hayo.

Mwisho wa siku ni ilani sio katiba!

Sikiliza mkuu 2010 CDM walizungumza sana kuhusu utawala wa majimbo lakini pia Elimu hapa nchini iwe bure katika kiwango flani cha elimu, aidha walikusudia kupunguza gharama za vifaa vya ujenzi ili iwe rahisi kwa mwananchi wa kawaida kumudu kuwa na nyumba bora ya kuishi.
Kwa maneno yako walikuwa wanafurahisha kwelikweli?
 
Uwe unafuatilia news, ilani mbona zimesemwa tayari. Chadema wao ni Ubepari, Cuf ni Uliberali. Nccr ni catastrophe prevention (majanga), nld wao privatization. Sasa mgombea wao maadam ni Prof. Lipumba na ni mchumi aliebobea basi atajua how to balance the equation

Hii ni kali
 
Members wa JF, sina tatizo na mchakato unaoendelea kwenye vyama vyote vya siasa kwa sasa hapa nchini. Nafahamu na ndivyo kwamba UKAWA siyo chama kilichosajiliwa na hivyo katika kuelekea uchaguzi mkuu ujao, umoja huo hauna ILANI ya pamoja.
Naomba tu ili kuweka kumbukumbu vizuri nifahamishwe bayana ni ilani ipi mgombea wa umoja huo ataenda kuinadi na kuitetea.
Nawasilisha

Kule Zanzibar CUF na CCM walishaunda serikali ya Umoja wa Kitaifa. Hivi wanatumia ilani ya chama gani kuongoza serikali mkuu?
 
Mgombea huyo atatetea ilani yenye tija,ukweli,mafanikio,kuondoa umaskini, kero zilizojengwa/kupandikizwa na watawala watangulizi.

Sikuzote mlikuwa mnajadili nini nyie?? Au mlikuwa managombea nafasi za uongozi tu?
 
CUF wanalazima kutumikia Ilani ya CCM maana hakuna namna nyingine

Hata UKAWA ni hivyo hivyo. UKAWA sio chama, bali ni ushirikiano. Sasa na wao wakishinda wataunda serikali ya Umoja wa Kitaifa, ikijumuisha vyama hivyo vinne. Kwa hiyo, nadhani majibu unayo mkuu, ila tu unafanya uchokonozi
 
Kitakacho fanyika mkuu ni kwa mgombea kunadi ilani ya chama alichotokea katika kampeni ila akiwa madarakani anamix sera za pande zote mbili.

We huna akili...sorry to say that...we unafahamu kuwa wananchi wanakichagua sababu ya sera unazowapelekea? Ukibadilisha huko mbele ya safari nani atakayekuelewa?
 
Back
Top Bottom