Mgombea urais hajui mahitaji ya nchi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea urais hajui mahitaji ya nchi!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nyange, Oct 19, 2010.

 1. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Mgombea wa Urais ambaye yuko madarakani kwa sasa hapaswi kutoa ahadi kwakuwa yeye bado ni Rais hivo yeye aanze kutekeleza kwa vitendo kuwafanyia wananchi. Aanze kununua meli, aanze kujenga barabara, nk, hana haja ya kudai kuwa akichaguliwa, ataÂ…hayo ni kama maigizo, tumeyasikia sana na yamekuwa kero kwa vile hayatekelezeki na ni kama usanii!

  Mfano Ili kuondoa msongamano wa magari barabarani, ati atajenga barabara za juu!! wakati barabara za vumbi kuziwekea rami zimemshinda kwa kipindi chote alichokuwa madarakani na tangu uhuru!. Akiwa waziri wa nishati na madini ukiachilia mbali kusaini mikataba inayo tia aibu kwa nchi, alishindwa kutatua tatizo la maji ambalo lilikuwa kwenye ofisi yake. Haikuishia hapo , akapewa miaka mitano kama Rais, bado akashindwa kulimaliza. Nilimsikia eti anatakiwa apewe miaka miwili tu ili alimalize! Hii si aibu tupuya chama?.

  Wadau nimetafakari kwa kina nikimshangaa mgombea urais mtaalam wa ahadi. especially hii ya Machinga Complex.
  Kwa watu waishio Dar mnajua biashara ya kimachinga. Hawa wafanya biashara hushawishi mtu ambaye tangu mwanzo anakuwa hana nia ya kununua bidhaa. lakini kwa kukutana naye, hushawishi kwa maneno matamu na punguzo la uhakika ili hatimaye ubadili mawazo na ununue bidhaa hiyo. Si kweli mtu anaweza kutoka nyumbani kwake akitafuta bidhaa kwenye machinga complex, wakati Kariakoo anaifahamu vyema na soko jipya la bidhaa Mlimani city, hapa inaonekana jamaa ameshindwa ku-link wamachinga na matakwa yao.

  Machinga Complex iliyojengwa karibu na uwanja wa Karume, haiwezi kuwa bussy na biashara kwa kuwa mmachinga ili afanye biashara inabidi akutane na watu wakipita ndo awashawishi. Kwa jengo lile machinga hawezi kukutana na watu na hivyo hawezi ku- Make.

  Mgombea Urais Kutangaza hadharani kwamba Selikari ikishika madaraka itajenga Machinga Complex kila wilaya za Dare s Salaam, inaonesha jamaa hajui kwa undani maana ya biashara ya kimachinga, na matatizo wanayo yapata. Namshauri kabla ya kuhutubia ajadiliane na watu wenye Upeo wa kujua mambo ili wamshauri cha kuongea kwenye mikutano make kila siku zinavyozidi kusogea ndivyo watu wengi wanagundua kuwa mkulu matatizo ya nchi hayafahamu vizuri na anaongea yaliyoko kichwani peke yake. Kwa nini mbunge wa zamani wa mtera asimsaidie mawazo?. Na pengine ndo maana wanaogopa midahalo wataulizwa kwanini wasitekeleze nao wana ahidi kama vile hawako madarakani.
   
 2. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  jakaya kikwete.JPG
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,789
  Trophy Points: 280
  Hiyo namab 66 imekaaje?
  Rasi obama kuimwagia Tanzania misaada hii nayo ni ahadi?? Kweli jamani?? Tunalima mchicha halafu dibwi lipo kwa jirani leh!!!!
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Huwezi kujenga Machinga Complexes kabla ya machinga wenyewe kutambuliwa rasmi kisheria....its a phenomenon tu...inabidi ipitishwe sheria kuwatambua rasmi wamachinga ndipo utumie resources kuwawezesha....tangu uhuru na baada ya 1976 kujengwa Kariakoo hakujajengwa tena soko
   
 5. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Hayo ndo yamkuu!
   
 6. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Visit source, mi nime-pest tu
   
 7. Bangusilo

  Bangusilo Senior Member

  #7
  Oct 19, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Imekaaa kama matonya alivyorudishwa nyumbani kwao na ahadi za uongo
   
 8. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,797
  Likes Received: 6,306
  Trophy Points: 280
  AHADI no.66 : Rais wa Marekani Bwana Barack Obama KUIMWAGIA MISAADA Tanzania - Ruvuma.

  Kazi kweli kweli!
   
 9. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Aaaargh...tushachoka...wa nini!!??
   
Loading...