Uchaguzi 2020 Mgombea urais CCK asema makahaba watachapwa viboko 200, jela miezi 6

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Kijamii (CCK), David Mwaijojele, amesema iwapo wananchi watakipa ridhaa chama chake kushika madaraka, serikali yake itatunga sheria ambayo makahaba, wasagaji na mashoga watakuwa wanachapwa viboko 200 na kwenda jela miezi sita.

Aidha, alisema mafisadi, watakatishaji fedha na wanaotorosha fedha nje watapewa adhabu ya kwenda jela miaka 50 na kupigwa viboko 200 baada ya kuhukumiwa.
Akizungumza katika mahojiano maalum na gazeti hili jana, alisema suala la rushwa limekuwa tatizo sugu nchini, hivyo serikali yake itahakikisha linashughulikiwa ipasavyo ili liishe kabisa.

"Mwili wa mtu si wa kufanyia biashara kingono, makahaba, wasagaji na mashoga wanaitia aibu nchi. Naomba wananchi wanikabidhi nchi nitawanyoosha," alisema Mwaijojele.
Alisema mambo mengine ambayo serikali yake itayapa kipaumbele ni elimu, afya na kuboresha sekta ya kilimo ambayo asilimia kubwa ya Watanzania wanajishughulisha na kilimo kwa ajili ya kuendesha maisha yao.

Mgombea huyo alisema serikali yake pia itahakikisha vyombo vya habari vinakuwa huru zaidi ili kutekeleza majukumu yao vizuri ya kuhabarisha wananchi.
Kuhusu kampeni, alisema chama chake kimejipanga kufika katika mikoa na wilaya zote kwa kutumia fedha ambazo zinachangwa na wanachama na watu wenye mapenzi mema na chama hicho.

"Chama chetu hakina wabunge, hivyo hatupati ruzuku, kwa hiyo fedha za kampeni tutachangisha ndugu jamaa na marafiki, ili kufanikisha kampeni. Nawaomba wananchi waniunge mkono kuchangia chama chetu ili kiingie madarakani na kuwaletea maendeleo ya kweli," alisema.

Alisema maeneo ambayo yeye mgombea urais hatafika kutokana na hali ya uchumi, viongozi wa mikoa, wilaya, tarafa, kata, kijiji na vitongoji watamnadi kwenye mikutano yao ya kampeni.

Pia alisema chama hicho kinacho ilani ambayo kitaitumia kuinadi kwa wananchi ili kukichagua na kushika dola katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28, mwaka huu.

"Uzuri chama changu kinao mtandao mkubwa wa wanachama na viongozi karibu katika kila mkoa na wilaya, nina imani watafanya kazi kubwa kukinadi chama," alisema.

NIPASHE
 
Chama kinachoenda kuchukua dola 2020.
JamiiForums39661901.jpg
 
Kweli mwaka huu wa uchaguzi tutaona na kusikia mengi.
Bwana Hashimu Rungwe anasema watatembea na masufuria kwa ajili ya kupika ubwabwa kwenye kampeni zake.
 
Sex is an art. Yawezekana huyu mgombea alinunua halafu akapunjwa utamu. Sasa anatafuta namna ya kulipa kisasi. Aachae watu wauze nyapu zao bhana. Kwani yanamhusu nn?
 
Nchi hii ina matatizo mengi yenye umuhimu kwa maendeleo wa Taifa halafu unakuja na sera za kufukuzana na machangudoa kama kipao mbele? Kwani unaliwa wewe?
2020 twende na Hashim Rungwe Spunda...
Mzee wa ubwabwa tuachane na hawa wababaishaji..
IMG-20200820-WA0066.jpg
 
Back
Top Bottom