Mgombea UKAWA Kujulikana Rasmi August 4

Mgombea UKAWA Kujulikana Rasmi August 4

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Kumekuwa na sintofahamu nyingi sana juu ya hatima ya nani mgombea wa Ukawa katika uchaguzi mkuu Oktoba 25.

Na sintofahamu hii imekuwa ikitumika na CCM kama sehemu ya propaganda na kuwahadaa wananchi kuwa UKAWA inamigogoro.

Lakini ukweli wenyewe utajulikana Tarehe 4 au 5 ya mwezi wa nane,Akiongea na Sauti ya ujerumani (DW) jana mchana katibu mkuu wa CHADEMA alisema"Mgombea wa ukawa atatangwazwa tarehe hiyo tajwa hapo juu.

Na ili kuondoa uongo au upotoshwaji unaofanyika kwa makusudi na baadhi ya watu ni vema kusubiri na kuwa wavumilivu kama mwenyekiti wa
CHADEMA alivyosema mwanza na kila kitu kitakuwa wazi siku ikiwadia.

Habari zote zinazosambaa kuhusu uwepo wa Ukawa na Lowassa kujiunga
CHADEMA ni kelele za CCM baada ya mgombea wao Pombe kuanza kuchuja,Na wananchi kuanza kumwona kama ni mtu wa kukurupuka na asie na busara za uongozi.

Iwe ni Dr. Slaa,Prof Lipumba au Lowassa hilo ni jambo linawahusu Ukawa,CCM Ni vema waache kuweweseka na waendelee kutulia dawa iwaingie.

CCM Mlitangulia tu,Na kutangulia si kufika.Ukawa wapo na wanakuja kwa kasi ya kimbuka,Nchi itakaa kimya soon.
 
Hawaaminiki hawa. Kwani si walituambia kuwa mgombea wao atajylikana leo?
Haya majamaa ni mababaishaji. Mpaka yapigwe kwenye uchaguzi ndio yajue kuandaa mgombea wao mapema.
 
Dr Slaa ndio Rais Anayekuja na Ufunguo wa Kutatulia matatizo ya Watanzania.

2010 Nilivutiwa na Sera yake ya Kupunguza Kodi kwenye vifaa vya Ujenzi ili Watanzania wawe na Nyumba Bora za Kuishi waachane na Nyumba za Tembe.

Dr Slaa njoo na hii Sera Tena Huku mtaani bei ya Siment hawaielezeki.
 
Sio kweli mkuu, Dr. slaa alisema wao kama chadema wana vikao vya ndani kuanzia tarehe 3 na 4,Aug, vya kumchagua mgombea wa CDM, na sio wa ukawa, ila baada ya hapo ndio mambo mengine yatafuata. Hivi huwa RADIO moja inaweza danganya kwa wakati mmoja?? au ni matatizo ys msikilizaji??! kwani humu siku hizi unakuta labda saa 7,mchana radio dw imemhoji mtu, lakini anaibuka mtu humu, analeta habari tofauti kabisa,
 
Dr Slaa ndio Rais Anayekuja na Ufunguo wa Kutatulia matatizo ya Watanzania.

2010 Nilivutiwa na Sera yake ya Kupunguza Kodi kwenye vifaa vya Ujenzi ili Watanzania wawe na Nyumba Bora za Kuishi waachane na Nyumba za Tembe.

Dr Slaa njoo na hii Sera Tena Huku mtaani bei ya Siment hawaielezeki.

"Ikulu siyo wodi ya wagonjwa" Kibajaji
 
Kumekuwa na sintofahamu nyingi sana juu ya hatima ya nani mgombea wa Ukawa katika uchaguzi mkuu Oktoba 25.

Na sintofahamu hii imekuwa ikitumika na CCM kama sehemu ya propaganda na kuwahadaa wananchi kuwa UKAWA inamigogoro.

Lakini ukweli wenyewe utajulikana Tarehe 4 au 5 ya mwezi wa nane,Akiongea na Sauti ya ujerumani (DW) jana mchana katibu mkuu wa CHADEMA alisema"Mgombea wa ukawa atatangwazwa tarehe hiyo tajwa hapo juu.

Na ili kuondoa uongo au upotoshwaji unaofanyika kwa makusudi na baadhi ya watu ni vema kusubiri na kuwa wavumilivu kama mwenyekiti wa
CHADEMA alivyosema mwanza na kila kitu kitakuwa wazi siku ikiwadia.

Habari zote zinazosambaa kuhusu uwepo wa Ukawa na Lowassa kujiunga
CHADEMA ni kelele za CCM baada ya mgombea wao Pombe kuanza kuchuja,Na wananchi kuanza kumwona kama ni mtu wa kukurupuka na asie na busara za uongozi.

Iwe ni Dr. Slaa,Prof Lipumba au Lowassa hilo ni jambo linawahusu Ukawa,CCM Ni vema waache kuweweseka na waendelee kutulia dawa iwaingie.

CCM Mlitangulia tu,Na kutangulia si kufika.Ukawa wapo na wanakuja kwa kasi ya kimbuka,Nchi itakaa kimya soon.

Final n vital punch...A sudden upper cross can be lethal n extremely dangerous.....! ccm is caputed
 
Ilikua Julai na sasa ni Agosti, nawaambia hawa jamaa watafika Novemba,Magufuli yuko Pwani anakatiza! Akiendelea na msisitizo wake wa MTUMISHI WA WATU, WA KUWATUMIKIA WATU BILA UBAGUZI WA DINI KABILA RANGI WALA VYAMA.
 
2010 walichelewa kwa kumsubiri Sitta mwaka huu vile vile bado wanambembeleza Lowasa inamaana ukawa nzima hakuna mwenue mvuto kwa wananchi wa kugombea urais.
 
And these are the people we want to run the country?

If they pick Lowassa they will lose all credibilty, not that they have much left. :sad:
 
Sumu haionjwi

Hii ni hatari kubwa!
Watu wanaonadiwa na mamluki wa kibiashara inaelekea watainunua UKAWA wakati wowote ule na ni kwa nia moja tu, kukamata dili zote za dola ili wanufaike kiuchumi.

Lakini wananchi makini wanaendekea kugutuka.
Tunajua kuwa hata wapinzani ni watanzania na huko kuna watu makini kitaifa.
Simpigii debe Dr Skaa lakini haingii akilini Dr Slaa kumtangaza Lowassa kuwa fisadi, halafu kula matapishi yake bila maelezo na kumkaribisha fisadi huyo huyo kukipigia debe chama chao.

Maendeleo ya Tanzania ni kuwa na upinzani makini utakao sahihisha kama sio kupiku chama tawala.

Kwa ujinga huu wa kukumbatia ufisadi ulio temwa na chama tawala, UKAWA unawakaribisha kina Rosta na Karamagi and co. iliwagawane rasilmali za nchi hii.

...... mpaka hivi sasa ndani ya UKAWA ni mtafaruku wa kukaribia kusambaratika kwani hawajui wanaenda Ikulu kufanya nini na kwa madhumuni gani kwa mwananchi wa kawaida.

Sumu haionjwi wanaukawa mutakufa bure!!!
 
Tumeshazoea kusikia maneno kama hayo! Yawezekana tarehe hiyo viongozi waandamizi wa ukawa wakaja na tamko la kuongeza siku 5,6 hadi 7 kama ilivyokuwa mwanzo.
 
Hawaaminiki hawa. Kwani si walituambia kuwa mgombea wao atajylikana leo?

Nilijua tu lazima urukie yasiyokuhusu halafu mlivyokuwa mazuzu kuuutwa nzima mmeshinda huku kujaza uongo badala ya kuimarisha chama lenu watu wa ajabu sana nyie.
 
Sasa kama umeshapata mgombea wako wa rais uliye na imani naye tatizo liko wapi la kukaa kimya ukisubiri tarehe ya kupiga kura badala ya kushinda Jf unapika majungu? "kama vya ukawa vinanuka tema mate uchape ndala"
 
Huu UKAWA ni shida! Ilipaswa mgombea ajulikane zaidi ya mwezi mmoha kuelekea kampeni ili kupunguza tofauti za kiitikadi, 'kumuuza' mgombea kwa wananchi, na kuratibu kampeni vyema, hasa masuala ya bajeti, timu, .... CCM wanapiga kam?peni kwa kusema wanamtambulisha mgombea. Urambuisho huo utafanyika nchi nzima. Nausikitikia upinzani wa Bongo usio na mwelekea sahihi na imara.
 
Back
Top Bottom