Mgombea ubunge Sumve sherehe uliyofanya kifo cha Ndassa sasa inakutokea puani, CCM kukosa majimbo haya Mwanza

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Mgombea ubunge Sumve sherehe uliyofanya kifo cha Ndassa sasa inakutokea puani, CCM kukosa majimbo haya Mwanza

Mgogoro unaendelea ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza kuhusu wagombea ubunge ndani ya majimbo ya mkoa huo.

Inaelezwa wagombea ubunge ndani ya chama hicho mkoa wa Mwanza wamekosa ushawishi kwa wananchi.

Kabla ya kuanza na wagombea hao kukosa ushawishi tuanze na huyu mgombea ubunge Sumve Bwana Kasalali Mageni.

Kasalali Mageni wakati wa kifo cha aliyekuwa mbunge wa SUMVE Richard Ndassa kinatokea alifanya sherehe nyumbani kwake akifurahia kifo hicho.

Mageni alifanya sherehe akifurahia kifo cha Ndassa na sasa mambo yamezidi kumwendea kombo.

Wananchi wa Sumve wameanza kumkataa kutokana na mikutano ya kampeni anayoitisha kukosa watu na kubaki akiaibika.

Pia Mageni yupo katika mgogoro na familia yake kutokana na kumkanya kufanya sherehe wakati wa kifo cha Ndassa na kugoma.

Pia Mageni ameibua mgogoro ndani ya CCM kutokana na jina lake kupitishwa licha ya kukosa nguvu na ushawishi kwa wananchi.

Mgogoro upo baina ya baadhi ya viongozi wa kamati ya siasa ya mkoa wa Mwanza ambao wanashtumiana kupitishwa jina lake na la wagombea wengine ambao hawana ushawishi.

Ndani ya kamati ya siasa mkoa wa Mwanza, wanalaumiana kumuandikia taarifa nzuri Mageni jambo ambalo lilimpa nafasi ya kapitishwa na halmashauri kuu ya CCM.

CCM Mkoa wa Mwanza wameanza kupata mashaka na mgombea huyo ambaye amekosa ushawishi kwa wananchi, wakihofia vyama vya upinzani kuchukua jimbo hilo.

Mkoa wa Mwanza una majimbo tisa ambayo ni Nyamagana, Ilemela, Magu, Ukerewe, Kwimba, Misungwi, Sumve, Buchosa na Sengerema.

Kati ya majimbo hayo, CCM Mkoa wa Mwanza baada ya kukaa na kufanya tathimini wamebaini asilimia kubwa yanaweza kwenda upinzani

Majimbo ambayo yanaweza kuchukuliwa na upinzani mkoa wa Mwanza ni Sumve ambalo mgombea wake amekosa ushawishi kwa wananchi, Nyamagana ambalo jimbo hilo kwa miaka mitano 2015 - 2020 kutokana na kukosa mtetezi na Jimbo kukosa maendeleo.

Jimbo lingine ni Sengerema ambalo mgombea wake Hamis Tabasamu ambaye amekuwa akijinasibua fedha zake ndizo zimempa nafasi hiyo licha ya sengerema kukosa maendeleo kwa miaka nenda rudi kwa kukosa miundombinu ya barabara na huduma ya maji.

Jimbo la Magu nalo CCM wamekosa imani na mgombea ubunge wao, Desdery Kiswaga kutokana na kukosa ushawishi na Jimbo hilo kukosa maendeleo ikiwemo ukosefu wa huduma ya maji safi na huduma za afya.

Jimbo la Ukerewe ambalo mgombea wake ni Joseph mkundi, wananchi wa Ukerewe wamegawanyika hususani wana CCM ambao wanadai hatamuunga mkono mkundi.

CCM wanagoma kumuuga mkono mkundi kutokana na kukatwa wafia chama hicho na kupitishwa mtu aliyehamia pamoja na jimbo hilo kukosa maendeleo miaka mingi ikiwemo wavuvi kuchomewa nyavu.

Jimbo lingine ni Buchosa ambalo lipo katika uwezokano mkubwa wa vyama vya upinzani kulinyakua hususani CHADEMA kutokana na CCM kugawanyika.

Inaelezwa CCM imegawanyika baina ya pande mbili wafuasi wa Charles Tizeba na Erick Shigongo ambao unatajwa kupunguza kura za CCM.

Makundi yaliopo ndani ya CCM Mkoa wa Mwanza yanawapa nafasi kubwa upinzani kunyakua baadhi ya majimbo.

Majimbo ambayo CCM itashindwa kwa asilimia kubwa ni Jimbo la Kwimba lenye mgombea Shanif Mansoor, Ilemela mgombea wake wa CCM ni Angelina Mabula, Misungwi lenyewe tayari mgombea wa ccm amepita bila kupingwa akisubiri kuapishwa.

CCM Mwanza jipangeni aibu hii ya 2020 sio ya mchezo
 
Back
Top Bottom