Mgombea ubunge CUF afungwa jela miezi nane

Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,250
740
Hili jimbo naona ccm wamebaki peke yao; mgombea mwingine wa Chadema alijitoa baada ya kufanya kampeni kwa wiki chache.

Mgombea ubunge CUF afungwa jela miezi nane
Monday, 18 October 2010 08:30
Phinias Bashaya, Missenyi

MAHAKAMA ya Mwanzo Nsunga wilayani Missenyi imemhukumu mgombea ubunge wa jimbo la Nkenge kwa tiketi ya CUF, Amri Sadik Mkurumbi kifungo cha miezi nane jela kwa kosa la kujipatia huduma ya chakula na vinywaji kwa njia ya udanganyifu.

Hukumu hiyo ilitolewa Oktoba 12 na hakimu wa mahakama hiyo, Jonathan Mutalemwa baada ya mtuhumiwa kukiri kosa la kujipatia huduma hiyo yenye thamani ya Sh130,000.

Ilidaiwa na karani wa mahakama hiyo, Twaha Kakoko kuwa mtuhumiwa huyo alijipatia huduma hiyo ya chakula Oktoba 2 akiwa na wenzake 33 kwenye Hoteli ya Sophia Bashiru iliyo eneo la Mutukura na kula chakula hicho bila ya kulipa.
Mtuhumiwa, ambaye ni mkazi wa Kata ya Kasambya, alikiri kosa la kuagiza chakula na kuondoka bila kulipa na mahakama kumpa adhabu ya kifungo cha miezi nane jera.

Pia Hakimu Mutalemwa aliamuru kuwa mtuhumiwa amlipe mlalamikaji Sh170,000 pamoja na gharama za mlalamikaji baada ya kumaliza kutumikia kifungo hicho.
Hakimu huyo alisema mtuhumiwa ambaye alikuwa anagombea ubunge wa Jimbo la Nkenge alitenda kosa kwa mujibu wa kifungu cha 302 na kanuni ya adhabu sura ya 16.

Katibu wa Cuf wilayani Missenyi, Leonard Makekela alisema mahakama iliwahi sana kutoa hukumu dhidi ya mgombea wao.
Huyo ni mgombea wa kwanza kwenye uchaguzi wa mwaka huu kukumbwa na adhabu hiyo ya mahakama kwa kutenda kosa ambalo liko nje ya shughuli za uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31.


SOURCE: Mwananchi
 
acha uongo mgombea wa chadema bado yupo na slaa juzi alikuwepo kumpigia kampeni huko kanyigo bukoba
 
Huyu Jamaa angejiunga na CCM wala asngalifungwa! Haoni Lowassa na Chenge wanatesa zao!
 
acha uongo mgombea wa chadema bado yupo na slaa juzi alikuwepo kumpigia kampeni huko kanyigo bukoba

Mkuu sie tuko jimboni huku Misenyi;
Phocus alijitoa kwa barua ilyothibitishwa na mwanasheria wake, Chadema Makao Makuu waliwasiliana naye arudishe jina lakini msimamizi wa uchaguzi hapa Misenyi hakumkubalia
 
... mgombea ubunge wa jimbo la Nkenge kwa tiketi ya CUF, Amri Sadik Mkurumbi

Huyu bwana alipata msukosuko kutokana na deni la ujio wa Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Lipumba. Pamoja na chama kumtelekeza hadi akahukumiwa kifungo, aliachiliwa baada ya siku chache baada ya kukata rufaa na kulipa faini badala ya kifungo.

Hata hivi baada ya sekeseke hilo, alisumbuliwa na maradhi ya kisukari na kuugua kwa muda mrefu hadi alipofariki dunia April 2012 hakuna kiongozi wa chama aliyemtembelea hospitali au kuhudhuria mazishi yake.

Itachukua muda mrefu kwa vyama vyetu hivi kuimarika hadi mashinani badala ya kukurupuka wakati wa uchaguzi na kuwasahau wanachama wao hadi baada ya miaka mitano.
 
Back
Top Bottom