DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
MGOMBEA wa Chama cha NLD, Doyo Hassan Doyo, amesema kuwa endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atatumia mbinu ya kipekee katika mapambano dhidi ya rushwa.
Doyo amesema watu wote watakaokamatwa na kuthibitika wamejihusisha na vitendo vya rushwa, watachapwa viboko 12 wakati wanapelekwa gerezani na viboko 12 zaidi watakapomaliza kifungo chao na kuachiwa huru.
Ameongeza kuwa adhabu hiyo itaoneshwa mubashara kupitia Televisheni ya Taifa (TBC) na itafanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, ili wananchi wote washuhudie hatua za wazi za kupambana na rushwa.
Soma Pia: GE2025 - Mgombea wa nafasi ya urais kupitia chama cha (NLD) Doyo amefika kuchukua fomu akiwa na Bajaj